Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 15 February 2015

Wapendwa natumai Jumapili inaendelea vyema;Tumshukuru/nina mshukuru sana Mungu;Burudani-Kijitonyama,Amenitendea na...!!!!!!


Wapendwa/Waungwana, Nimatumaini yangu Jumapili hii inaendelea/Imekuwa njema kwenu..
Bila shaka mmemaliza juma/ wiki hii vyema na mmejiandaa vyema kwa Juma/wiki lijalo.
Mimi nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mengi sana aliyonitendea na anayoendelea kunitendea,
Mungu amekuwa nami katika yote...
Sina budi ya kuzidi kumtukuza na kumrudishia utukufu kwake..
Ndugu yangu Mungu anatenda Bwana..usikate tamaa wala usife moyo..kama si leo kesho utapokea tuu..
Tena kwa Mungu hakuna Rangi,Kabila,Mfupi/Mrefu,Haijalishi umetokea wapi/Taifa gani,Kila kitu kina sababu yake.
Yeye akisema ndiyo nani aseme hapana/siyo?
Anaweza kukuweka sehemu ambayo hukutegemea akakuchanganya na watu usiowajua vyema mila/Tamaduni zao.
Lakini yeye akiona panakufaa basi mtaelewana/kuendana/vyema.
 Mtaishi kwa Upendo,Furaha,Amani,Umoja na kuheshimiana.
Na hapo kuna mengi ya kujifunza,kila mmoja atajifunza ya mwingine.
Sasa utabeba unaloliona linafaa kwako na lisilo na manufaa/faida,Ulazima utayaacha hapohapo....
Mungu amempa kila mtu karama yake...Tumuombe sana Mungu azidi kutupa maono/ndoto.
Asante pia kwa siku hii...nilikuwa nina kibarua/nafanya kazi sehemu...
wakati/muda aliyonipa Mungu kufanya kazi/kuwa na wapendwa hawa umekwisha..
Nikasema kwaherini..ilikuwa ni vigumu sana kusema kwaherini...lakini kila jambo lina mwanzo na mwisho
Mwisho wake ulifika.Maisha lazima yaendelee..
Niliwapenda/Nitaendelea kuwapenda..
Kuna mengi nimejifunza kupitia wapendwa/waungwana hawa...
japo nilikuwa mweusi/mwafrika peke yangu lakini sikuwa mpweke.
Nina imani Mungu aliniweka hapo kwa sababu zake.
Ninamshukuru sana Mungu wangu nanimeuona utukufu wake..
G.H.Mkae salama na Mungu azidi kuwabariki.


Thank god for this day i was working somewhere, 
the  time god has given me to work with these lovely people has come to and end 
it was hard for me  to say goodbye 
but everything has a begging and an end 
i loved them and i always will 
i have learned lots from them 
i was the only one from africa, however  i was not alone becuse they showed me such love that ive never witnessed before
i know god put me there for a reason 
i thank God  i have seen the amazing things he can do, 
and i would like to say thank you so much to these amazing people from GH
Stay safe and ppeaceful may God bless you !! 

 3Je, huyu si yule seremala, mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?” Basi, wakawa na mashaka naye.Neno La Leo;Marko:6:1-53
Yesu anakataliwa huko Nazareti
(Mat 13:53-58; Luka 4:16-30)
1Yesu aliondoka hapo akaenda katika kijiji chake, akifuatwa na wanafunzi wake. 2Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya? 3Je, huyu si yule seremala, mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?” Basi, wakawa na mashaka naye. 4Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” 5Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya. 6Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao.

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Nawapenda wote.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Naoana sijachelewa na hata kama basi napenda kusema kuwa Hongera kwa kuishi na watu vizuri ndo maana walikupenda. Kila wakati mtu kuwa kama ulivyo. Na nina imani jumapili yako ilikuwa njema.

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana Kadala wa mimi...jumapili ilikuwa njema kabisa..
Asante kwa Neno.