Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 9 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili;Emu-Three-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 5!!!!!


Maua alikuwa katulia kwenye chumba huku akimuomba mungu wake, mwanzoni alikuwa anashindwa hata aombe nini. Akawa anajiuliza je nimuombe Mungu  anisamehe kwa hayanmakosa niliyofanya, lakini akajiuliza kichwani makosa gani, na kama ni makosa mbona ni yeye peke yake ndiye anayeadhibiwa, mbona mwenzake waliyeshirikiana naye , hayupo, je na yeye hastahili kuadhibiwa.

Alipowaza hilo akamkumbuka mwenzake, akakumbuka jinsi walivyokuwa wakiandikiana barua, lakini ghafla akawa hamjibu barua zake tena, hasa pale alipoandika kumuelezea jinsi gani anavyojisikia,na kumwambia anaogoa isije ikawa ni mimba. Ilikuwa barua ya mwisho kumwandikia, na hakuweza kupata jibu, na hata alipoandika nyingine, na nyingine, hakiweza kupata jibu kwa mtu aliyetokea kumpenda sana.

‘Hivi huyu mtu yupo aua kapotolea nchi gani, nakumbuka mara kwa mara anakwenda Arusha kwa mjomba wake, ambaye ni tajiri mmoja wa madini,na nia na lengo lake na yeye ni kujiunga kweney biashara hiyo, lakini kwanini asimwambia, au kumjibu baraua zake,lazima nimtafute tusaidiane hili tatizo’akasema huku akiangalia nje kwa kupitia dirishani.

Akawa bado anawaza ni mambo gani kwasasa anahitajika kumuomba Mungu wake, `Au  nimuombe Munguwangu anisaidie nisiweze kuangukia kwenye mikono ya baba, baba ambaye anataka kuitoa roho yangu, bila makosa, ‘ akasema na alipofikia kuwaza hili akatikisa kichwa na akili yake ikawa anajiuliza ‘Ina maana kweli mimi sio mkosaji,hivi kweli sistahili kuadhibiwa kwa kosa hili?’akatulia na kujarabi kutafakari zaidi. Hapo akakumbuka kauli ya baba yake, ambaye kila mara wakiwa naye alipenda kumuasa nayo;

‘Binti yangu nakupenda sana, na jinsi ninavyo kupenda,  nisingelipenda ukaja kuvunja huu upendo nilio nao juu yako, nakuomba  sana usije ukaniangusha, maana kila mtu hapa kijijini anakuona kama mtoto wa mfano, na mimi huwa natamba kwao kuwa  wewe ni binti mwenye akili, binti mwenye nidhamu, binti ambaye hakuna anayeweza kumfikia kwa jinsi ulivyo hapa kijijini’ilikuwa sauti ya baba yake.

Baba yake kweli alikuwa akimpenda, lakini sio ule upndo wa kumdekeza, kwani akifanay kosa alikuwa akiadhibiwa, mpaka anawaza vibaya kuwa baba yake anataka kumuua, na sio kweli anampenda kiasi hicho. Lakini kaam hajafanay kosa, baba yake alikuwa akribu sana na yeye na kila mwaka wakifanya sherehe za shule anakwenda kushuhudia mtoto wake akipewa zawadi ya kuwa mtoto wa kwanza, na wakirudi nyumbani huchinjiwa kuku kama zawadi maalumu. Na alipofaulu kwenda sekondari, baba alimnunulia zawadi nyingi sana.

`Sasa huyu ndiye binti , binti ambaye baba alikuwa akitamba kuwa ndiye binti wa mfano..’, Maua akajikuta akifuta machozi, akaliangalia tumbo lake, ambalo bado lilikuwa halijaonyesha dalili yoyote kuwa kuna kiumbe ndani , akakunja uso na kuanza kujpiga piga tumboni huku akilaani,i hicho kiumbe kilichopo tumboni,utafikiri ndicho chenye makosa akasema;Inaendele ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Diary 

Yangu

Yakeeeeeeeee!!!!!

"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima...

2 comments:

emu-three said...

Mmmh, ndugu wa mimi kweli tupo pamoja daima shukurani kwa moyo wako huo,unarikiwe saana

Rachel siwa Isaac said...

Mmmhh Pamoja Daima ndugu wa mi!!!!!!!!!!