Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 29 March 2012

MAZISHI YA MAREHEMU DENIS OSWALD KAPINGA


Ndg. Joseph Oswald Kapinga

Ndugu Joseph Kapinga pichani hapo juu anapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwa Ratiba ya mazishi ya mpendwa mdogo wetu Denis O. Kapinga yatafanyika leo Tarehe 29/03/2012 katika makaburi ya Sinza karibu na ukumbi wa mwika.

Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Mwili wa marehemu utafika Nyumbani maeneo ya Sinza karibu na New White Inn Bar bara bara ya Sinza uzuri mnamo saa 6.00 Mchana kutoka Hospitali ya Mwananyamala.

Mwili utaagwa nyumbani saa 7.00 Mchana na baadae utapelekwa kanisa la Roman Catholic Sinza kwa Ibada.

Baada ya hapo Saa 8.30 Mchana mwili wa marehemu utapelekwa Makaburi ya Sinza kwenye nyumba yake ya milele.

"BWANA ALITOA NA BWANA 

Poleni sana Familia ya Kapinga.
Swahili na Waswahili tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu kwenu.

Mungu awatie Nguvu.
Ulale kwa Amani kaka Denis.O.Kapinga.

No comments: