Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 1 October 2011

Siku kama ya Leo dada Rabia,Nyembo Alizaliwa!!!!

Familia ya Bibi na Bwana A.Jumaa wa Dar-es-salaam,Siku kama ya leo walipata mtoto wa kike na Wakamwita  RABIA.


Ujumbe kutoka kwa Rabia.J.Nyembo;Anapenda kuwashukuru sana wazazi wake kwa malezi mema naya upendo waliyompa, mpaka pale alipoolewa.
Shukrani kwako Mume wangu kipenzi bwana Nyembo,na Mungu atubariki siku zote za maisha yetu,pia Asante  Mungu kwa kunijalia watoto wazuri,Naomi na Nadia.
Namshukuru sana Mungu kwakunifikisha hapa.
Mungu Tubariki Sote.


:Swahili na Waswahili wanakutakia kila lililo jema kwako na Familia pia.
 Mungu akuongezee miaka mingine mingiiiiiiiii.


4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Hongera sana, Mrs Nyembo, kwa mawazo yako mema ya kuthamini na kushukuru.


Wengi tunaweza kufikiri ndoa na vitu vingine vingi vyenye thamani maishani mwetu: kama malezi bora vile...ETI NI HAKI YETU!


Tutawakashfu wazazi wetu; tutamdharau mwanandoa mwenzetu; na tutaona kosa kwa kila kitu dunia ya Mungu ilietupatia. Kifupi, tunatafuta kila kisa na mkasa ili tuonyeshe namna maisha yetu yasivyoridhisha!


Kwa hiyo Rabia, ujasiri wakutoa neno Shukrani kama hilo lakwako kweli ni adimu sana.


Mimi binafsi kama Manyanya neno lako limenifikisha hadi kwenye madeni tele nilienao kwa binadamu wenzangu wote walieniwezesha kuishi hadi dakika hii! Kusema ukweli sijui nitapata lini moyo wa kushukuru!

SIMON KITURURU said...

Rabia Hongera MWANAKWETU!

Mija Shija Sayi said...

Yaani Rabia unazidi kuwa kama mtoto mchanga...hebu tupe siri ya urembo wako.....lol!!

Hongera sana kwa kutimiza miaka na salamu kwa wote

Mama Mija.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera Rabia!!