Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 11 April 2011

Jikoni leo ni Pilau!!!!!Kinapendwa sana,unafikiri kwa nini???

 Kitu Pilau kipo jikoni hapa, harufu  yake mpaka mtaa wa tatu!!!!!!
 Leo tunakula kwa Kachumbari si Saladi,mimi hupenda kula na Kachumbari!!!!
 Kimepakuliwa kitu Pilau bila ya chochote, wengine hupenda hivyo!
Hapa nimeongezea  Kachumbari na ndizi mimi hupenda hivyo!
Hicho ni Chakula kinachopendwa na Waswahili wengi, Sherehe/mikusanyiko/Misiba, niliyowahi kushiriki
sikosi kukuta chakula hiki!!
Je wewe unakipenda?na unapenda kuongezea na nini pia kushushia na kinywaji gani?
Karibu sana tukijadili hiki Chakula kwanini unafikifili kinachukua nafasi kubwa?
Asanteni na karibu sana!!!!!!

12 comments:

isaackin said...

aisee hapo ni kamili kabisa hamna cha kuongeza,labda tu nyama uliyoweka naona mnofu mimi napendelea yenye mifupa ili nijilambe vizuri,na hapo kinywaji ni maji bariidi tu na kitanda kiwepo jirani ili baada ya kuvimbiwa upige usingizi kwanza.

emu-three said...

Mimi mchana sijauona halafu unaleta ile kitu inayotamanisha, ....mmmmh, ahsate nimeshiba hata kabla sijala.UBARIKIWE SANA NDUGU YANGU

Yasinta Ngonyani said...

Hakika hakuna cha kuongezea ila mwanangu anasena inakosekana ile nyama ya mchuzi au mchuzi tu mama "mdogo"..."mkubwa" Rachel ...lakini kama kawa ni sawa kabisa. yam yam yam...

Swahili na Waswahili said...

hahaha @kaka isaackini ok nitakuwekea mifupa!!!

hahaha @emu-three ndiyo nakupa matumaini hayo!!!!!

@dada Yasinta mwambie mwanangu asijali ninamtengenezea mchuzi wa nguvu!!

Yasinta Ngonyani said...

Rachel mwano amefurahi kweli na yupo mbioni kuja ...!!

Swahili na Waswahili said...

Mwambie Mwanangu nami nimefurahi sana,akaribie sana hapa kwao tuu!!!!Wasalimie sana waambie mimi nawasubiri!!

SIMON KITURURU said...

Jamani mie ni udenda tu hapa!

Swahili na Waswahili said...

hahahah pole @kaka Kitururu karibu pande hii kaka!!

chib said...

Mara nyingi huwa nakwepa kusoma na kuangalia matoleo ya vyakula vya nyumbani, kwani huwa vinanigusa saaana, kiasi kwamba hutamani kukwea pipa nirudi nyumbani nikamate, na kisha nirejee kibaruani na kuendelea kula kwa mama wa kambo(hotelini/ migahawa)

Swahili na Waswahili said...

Pole kaka Chib kwanini hukorofishi hapo ulipo?au unataka vyenye uasili kabisa?kwikwikwikwi nimeipenda hiyo kwa mama wa kambo!!!!!!.

chib said...

Ha si wajua tena, sitaki kutoa sababu nyingi nitajikanyaga bure, lakini sababu kubwa ni muda na mazoea! Ha ha haaa

Swahili na Waswahili said...

hahahha nimekupata kaka Chib!