Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 14 December 2010

jikoni leo!

Sufuria inavuja,motoumezimika,kibatari hakina mafuta je tutakula leo?

10 comments:

Mija Shija Sayi said...

Patamu hapo, halafu na jirani ametoka huna hata pa kukimbilia..

Swahili na Waswahili said...

hahaha da Mija sasa hiyo mida ya usiku hata pakupotezea hakuna watoto wamejikunyata wanakuangalia wewe!

SIMON KITURURU said...

Kwa kuwa nasikia Adamu na Hawa hawakuwa na sufuria, kibatari wala mafuta,.... basi matumaini yapo ingawa shughuli yake nzito!

Fikiria hapo ndio una watoto na wao wanakuambia njaa inauma huku wakikutegemea wewe ndio una suluhisho!

Kazi kweli kweli!:-(

Ila tukumbuke vyakula vingi hulika vibichi!:-(

Si mchele si sumu hata kama haujapikwa kugeuzwa wali?

Yasinta Ngonyani said...

Yaani hapo umenikumbusha mbali sana. Ahsante kwa kumbukumbu!!

MAMA BRIAN said...

we acha tu halafu utakuta nje mvua inanyesha,watoto wanalia baba kaingia mtini mwee kula hakuna hapo,

Anonymous said...

Muache kusugua masufuria na michanga, majivu yanatosha.

Maza hausi..

Swahili na Waswahili said...

Asanteni wapendwa kwa maoni yenu kaka kitururu shughuli pevu! @da Yasinta nategemea utaimalizia hiyo maana umekosa jibu kwani umewaza mbali sana!hahahhah,
@mamaB hahah baba kaingia mitini!
@maza hausihahahaha tutafanya hivyo!!

emu-three said...

Na mimii sikuwahi kuingia hapa mapema, lakini kuna usemi wasema `mtu hataishi kwa mkate pekee...' nahisi una maana pevu, siku hiyo ni kuwapa mchele watafune, wanywe maji mumuombe Mungu...~
Lakini kinachonikuna ni `kuwa baba kaingia mitini?' kwanini kaingia mitini? Maisha magumu sio...
Tatizo hilo kiundani linaelezea halii halisi ya nchi zetu masikini. Sasa hivi umeme hakuna na bado wajamaa wanataka kupandisha bei, ...bei vitu juu, mshahara au kipato kiduchu, ukizunguka kidogo jamaa wa city hawa, watu wa kodi hawo...mtoto anaumwa, hospitali hakuna dawa...unachangia nini? sijui, mashulenii masomo mmmh, kila siku michango, walimu hawaonekani!
Mungu wangu na jana mvua imenyesha kwa hapa Dar, manake usafiri shida, barabara zetu za uchaguzi sasa ndio mabwawa ya samaki, magari hayapiti...kiatu kimeharibika kwa kukanyaga matope...mungu ...baba kaingia mitini! Hajaingia mitini, wapo sasa hivi wanakula honey moon, wapi ZENJ, wengine Mikumi, wengine Ulaya...KUFA HATUFI CHAMOTO TUTAKIONA!

Swahili na Waswahili said...

hahahahha@emu-three ujachelewa wangu!baba ajaingia mitini hahahh!yupo chobingo! sasakiatu chenyewe kikikatika mjini na washonaji wanakimbizwa na city!kazi ipo,na hilo ndilo jiji la darisalama waliyokuwa mikoani na vijijini bado wanandoto ya kufika hapo je tutafika?
Aksante sana mpendwa kwa ufafanuzi wako!.na karibu sana.

Mija Shija Sayi said...

Limenikuna hilo la bei ya vitu Bongo ambalo emu-three aligusia. Jamani bongo bei ni kukomoana.