Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 28 February 2012

Jikoni Leo -Bamia,Kwanini Wanaume wengi Hawali?Burudani- Nshomile!!!!!

Bamia za kukaanga na mafuta,Hapo naongeza na nyanya.

Mimi hupenda na Ugali.



Bamia za Kuchemsha[Mrenda]
Waungwana hivi ni kwanini mboga hii ya Bamia Wanaume wengi Hawali/Hawaipendi? Jee wewe Unapenda Bamia na Unapikaje?Wengine wanatia na nyanyachungu,Kwenye Samaki Wakavu na....Jee Unaweza kula Bamia na Ugali wa Muhogo? Karibuni sana!!!!

Monday 27 February 2012

Mtoto Wetu Leo-Sabrina!!!!!!

katika Poziii
Alikuwa MC
Mifugo ni adimu kwao,weee paka njoo hapa!!!
Kwanini jana ulikimbia?utahama humu oohh,haya niamkie..
                                          Kama hutaki ngoja nikuamkie wewe!!!
Waswahili wanasema vyakurithi Vinazidi jee ni kweli?
Jee Watoto wanaweza kurithi Vituko,Ucheshi,Upole na Ugomvi?
Na kwanini baadhi ya misemo ya watoto inafanana kama Maji,kuwa Mma,Nyonyo na.....?
Kunawakati unaweza cheka na Mtoto mdogo au Kulia kwa mambo yake!!!!
Wengine hawapendi kula,kulala Usiku na mambo mengi.Pia kuwa na Mtoto kuna Raha yake!!

Kama wewe huna Mtoto na Unahitaji,Mungu yu Mwema  Uskate Tamaa!!!!

Sunday 26 February 2012

Nawatakia J'pili Njema,Burudani-Unastahili Kuabudiwa !!!!

Naye alipowaona Makutano,alipanda mlimani;na alipokwisha kuketi,Wanafunzi wake walimjia;.Akafumbua kinywa chake,akawafundisha,akisema,Heri walio maskini wa Roho Maana ufalme wa mbinguni ni wao.Heri Wenye huzuni;Maana hao Watafarijika.Neno la  Leo;Mathayo Mtakatifu:5;1-16.Mbarikiwe sana!!!

Saturday 25 February 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Muzina yaTabu ley,Zaiko Langalanga na Bozi boziana!!!

Leo nimekurudisheni nyuma kidoogo,Vipi  kuhusu vibao hivi leo,kuna lolote unalokumbuka?Twende Sote na Burudani !!!!!Nawatakia week end Njema.

Wednesday 22 February 2012

Wanawake na Mitindo,Leo Uvaaji wa Miwani!!!!



Nimatumaini yangu woote wazima,Haya Waungwa vipi kuhusu Wanawake wavaapo Miwani,Nikuongeza Urembo,Kuvutia,Haiba,Kujikinga na jua au Wanaficha kitu,Wanaaibu,Wanajishaua? Na jee Wanaona vizuri kweli ?Wewe /Mkeo unapenda kuvaa/Avae Miwani na kwasababu ipi?


Karibu sana Waungwana.

Tuesday 21 February 2012

Nderemo na Vifijo Leo -Rwanda, Ni da'Rubango apata Mwenza!!!!!!




















Hayawi hayawi sasa Yamekuwa! dada Rubango na Mumeo Hongereni sana kwa kuwa MKE na MUME!!
Mungu asimamie maisha yenu yawe yenye Baraka na Amani.

UJumbe;dada Rubango na  nawatakia maisha mema yenye Furaha na Upendo wewe na Mumeo,Mungu awenanyi kila iitwapo Leo,Nawapenda sana.
   Wako Neema Nyanyile
      COVENTRY.

Sunday 19 February 2012

Nawatakia j'pili Njema,kibao kutoka Kijitonyama-Masiah wanyi!!!!!!!


Ni juma pili nyingine tena Mpendwa,Tunamshuru sana Mungu kwa kututunza siku zote,Mimi na Familia yangu tunawataki kila lililo jema na Baraka,Amani,Upendo,Umoja na Utuwema.Mungu awe nawe kila inapotwa Leo.Tusamahe na kuomba Msamaha pale tunapokosana/kukwazana.Mungu ni Pendo Apenda Watu.Mimi nakupenda wewe!!!.Twende Sote sasa,PAMOJA SANA!!!!!