Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 23 May 2011

Tracey atimiza miaka 10!!!!!!!!!!!!!

 Tracey-Sarah, Ametizimiza miaka 10,hapo amepozi akitafakali duhh nimekuwa dada sasa.

 Yaani mimi ndiyo nimefika maika hii?



 Kikosi kamili cha Watoto wa Coventry Christian Swahili Fellowship,Kikiongozwa na dada mkuu dada Damari Kihauka chini ya Mwenyekiti da Mija. Nitakueleza Siku nyingine mambo mengi kuhusu kikosi hiki!!!!!!

 Tracey na dada Damari wakitayarisha Keki ili kila mmoja apate.



                                       


                      Tracey akipokea zawadi maalum kutoka kwa kaka Joel.
 Wamama nao hawakuwa nyuma,kwaniaba ya Wazazi wote wa Swahili Felloship.

                                   dada Tracey-Sarah anasema Asanteni sana na Mungu awabariki!!!!!!!

Friday 13 May 2011

Kutokana na Tatizo la kublog, Sabrina atafuta Njia!!!!

Tangu jana kulikuwa na tatizo la kublog,,Mtoto Sabrina akaona ngoja ajaribu kutengeneza!!!!!Alifikiri Tatizo lipo kwa Shangazi yake tuu.Wapenzi wa SwahilinaWaswahili poleni kwa Usumbufu wowote uliojitokeza sasa tunaendelea kama kawaida.

Saturday 7 May 2011

Watoto na Urembo!!!!!!

Mzazi/Mlezi na Mwana familia.Unamawazogani kwa watoto wadogo na  kujiremba?.
Hasa kwa mtoto wakike wa Leo/Sasa, Unafikiri ni umri gani kwake unafaa kwa kuanza kupaka,Shedo,Wanja,Rangi za mdomo,Kunyoa nyusi, kupaka Poda na mapambo mengine yanauotumiwa na Wanawake /kina Mama.Na si kila Mama/Mwanamke anayependa kujiremba pia.
Karibuni sana kwa Kuelimishana na Kusaidiana katika Malezi ya Watoto wetu.

Tuesday 3 May 2011

Waswahili wa Holland na Qeen Day!!!!!!!!


































 Waswahili wa Holland wakisherekea Qeen day.Hii ni Siku muhimu kwa watu wa Holland,Waswahili wa huko nao wakaona vyema kujumuika na wenyeji wao.Tunawatakia Maisha mema na Ushirikiano mzuri.
Je wewe msomaji  huko unapoishi,  Unapenda kuungana na wenyeji wako katika siku zao muhimu?Karibuni sana  Waswahili wote popote mlipo,Mnaweza kutuma picha /matukio yenu.

Friday 29 April 2011

Waswahili na Royal Wedding





















Wazazi/Walezi na Watoto wanaosoma Henley Green Primary School,Coventry,UK.Jana walijumuika pamoja na Walimu wao kwa Kusheherekea Royal Wedding.Wengi wao kama si wote waliokwenye picha hizi wanazungumza Kiswahili,Ni Waswahili wa Tanzani,Kenya,Burundi,Rwanda na Congo. kama uonavyo Kanga ,Vikoi,Mikeka vilitandikwa chini Waswahili wakajiachi.

Swahili na Waswahili inawatakia mapumziko mema na Ndoa njema kwa maharusi.