Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Majonzi. Show all posts
Showing posts with label Majonzi. Show all posts

Saturday 4 May 2013

Poleni Sana Familia Ya Costa Shirima!!!!!


Ulale kwa Amani Mpendwa wetu COSTA SHIRIMA.Pole  Sana Mke,Watoto,Wazazi,Ndugu,Jamaa na Mrafiki kwa Msiba huu wa Mpendwa wetu  COSTA SHIRIMA.Daima Tutakukumbuka na Kuenzi Mema yote uliyoyatenda.Familia ya ISAAC,Swahili NA Waswahili Blog Tupo Pamoja katika wakati huu Mgumu Kwenu.

Habari kamili,shukrani;http://mrokim.blogspot.co.uk/
MFANYA BIASHARA COSTA SHIRIMA ALIYEDONDOKA  GOROFANI KARIAKOO...



TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.


Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.

Wednesday 17 April 2013

Ulale kwa Amani Fatuma Binti Baraka -Bi KIDUDE!!!!!

Fatuma Binti Baraka[Bi KIDUDE] Amefariki.

Pole kwa Familia,Ndugu,Jamaa,Wasanii,Wapenzi na Wa TANZANIA Wote...
Na Apumzike kwa Amani bi Kidude.

"Swahili NA Waswahili" pamoja Daima.

Thursday 17 January 2013

SIMANZI KUBWA; JUDITH CHIKAKA AWALIZA CHUO KIKUU CHA ARDHI, WAFANYAKAZI WENZAKE WIZARA YA ARDHI, WANA CCM TEMEKE, CHAMA CHA WANARIADHA TANZANIA, MUMEWE ERASTO MAPUNDA NA WANAMICHEZO KWA UJUMLA.



Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.


Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
Marehemu Judith Chikaka alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.


Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka

Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi

Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada.
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.

Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.

Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI.
AMIN.


"Swahili NA Waswahili" Inawapa pole wafiwa na wote walioguswa na Msiba huu.

Wednesday 2 January 2013

Poleni Sana; Familia,Wa-Tanzania na Mashabiki wa Sajuki!!!

Marehemu;Juma Kilowoko [Sajuki].

Pole sana Wastara,Familia,Ndugu,Jamaa na Marafiki, Wa-Tanzania na Mashabiki wa Sajuki.Sisi Tulikupenda lakini  Lipangwalo na MUNGU Bina Damu hawezi kulipangua.

  Ulale kwa Amani.

Mboni Yangu-Wimbo uliokuwa ukihamasisha Uchangiaji wa Matibabu ya Sajuki.
Yote hayo yalifanywa kwa Mapenzi mema ili kuokoa Maisha ya Mwenzetu.


Wimbo umeshirikisha mastaa wa kibongo kama Ali Kiba, Wema Sepetu, Mwana FA, Professor Jay, Mzee Yusuph, Chidi Beenz, Fid Q, Afande Sele, Amini, Ditto, Madee, Peter Msechu, Dina Marios na wengine wengi.


"Swahili NA Waswahili" MUNGU awatie Nguvu katika wakati huu Mgumu.
Pamoja Daima.

Wednesday 31 October 2012

Mpendwa Wetu da'Mamie Msuya Amefiwa na Mama Yake!!!!!


Da'Mamie Msuya Pichani.
Amefiwa na MAMA yake Mzazi Afrika.
Dada Mamie anajiandaa na safari, Ataondoka kesho kwenda Afrika.
Tuungane nae katika wakati huu mgumu kwake. Hapa U.K. Msiba upo Nyumbani kwake.
Address;3C THOMAS KING HOUSE,
WELLINGTON ST,
CV1 5SJ.
COVENTRY.
Asanteni.

Monday 3 September 2012

Tamko La Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Iringa Juu Ya Kifo Cha Daudi Mwangosi!!!



KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) na waandishi wa habari wote mkoani Iringa na nchini kwa ujumla wamepokea kwa mshutuko na masikitiko makubwa kifo cha Mwenyekiti wa IPC, Daudi Mwangosi.

Mwangosi ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, alifariki jana majira ya saa 10 jioni baada ya kupigwa bomu katika vurugu za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitawanywa na jeshi la Polisi.


Utata wa nani anahusika na tukio hilo umeendelea kugubika huku jeshi la Polisi likitoa tamko linalodhihirisha dhahiri kwamba wanataka kujiondoa katika kosa hilo kabla uchunguzi haujafanyika.


Katika taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Polisi hii leo imedai kwamba bomu linalodaiwa kumuuawa mwandishi huyo lilitoka katika kundi la wafuasi wa Chadema, wakati Mwangosi akitafuta msaada wa kujinusuru kwa askari waliokuwepo katika eneo hilo.


Lakini wakati jeshi hilo likitoa taarifa hiyo inayokinzana yenyewe, limeshindwa kueleza ni kwasababu gani bomu lililorushwa kutoka katika kundi la wafuasi hao likamdhuru na kumuua mwandishi huyo pekee yake wakati alikuwa ameshikiliwa na mmoja wa askari wa jeshi hilo baada ya kupigwa virungu alipotaka kujua sababu ya kukamtwa kwa mwandishi mwingine Godfrey Mushi aliyekuwa akipiga picha tukio hilo.


Uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwepo katika tukio hilo na zile zilizoandikwa na kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari toka jana.


Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile muhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo.


Ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viiingilie kati katika uchunguzi huo.


Na kwa kuzingatia mazingira hayo, IPC kwa kushirikiana na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani Iringa, kuanzia leo wanatangaza rasmi kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi hilo mpaka pale taarifa au majibu sahihi kutoka kwa vyombo huru vitakavyolifanyia kazi suala hilo yatakapotolewa.


Kazi hizo ni pamoja na kuwataarifu waandishi wa habari kusitisha mara moja kwenda katika Ofisi ya RPC kwa ajili ya kupata taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu yanayotokea kila siku.


Aidha IPC inawataka wanachama au viongozi wake waliokuwa wajumbe wa kamati zozote zile zinazolihusu jeshi hilo ikiwemo ile ya maandalizi ya wiki ya usalama barabarani kujitoa kwenye kamati hizo.


IPC inawaomba waandishi wa habari kushikamana katika kipindi hiki kigumu kwa kuzingatia kwamba yaliyomkuta ndugu yetu Mwangosi yanaelekea kumkuta mwandishi yoyote Yule nchini.


Tukio hilo linadhihirisha jinsi uhuru wa habari na vyombo vya habari unavyozidi kukandamizwa hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania kwa ujumla wao wanatakiwa kushiriki kikamilifu kuandika Katiba Mpya wanaoitaka.


Tukio hilo haliwezi kuvumiliwa na kwa msimamo huu, IPC inaomba waandishi wote wawe na wimbo mmoja utakaowezesha muhusika wa mauaji hayo akamatwe na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.


Pamoja na kukamwata kwa muhusika, IPC inataka kuona jeshi la Polisi ambalo kimsingi halipo juu ya sheria linatimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria kama ilivyo kwa taasisi zingine.


Aidha kwa sasa wanahabari mkoa wa Iringa tunatangaza rasmi kusitisha mahusiano yetu na jeshi la polisi kwa kuandika habari za polisi .


Pia tunatambua kuwa wakati Mwangosi akikamatwa alikuwa katika kutimiza wajibu wake kama mwanahabari hivyo hata kama alikosa kwa kufika hapo hukumu yake haikuwa kuuwawa .


Hivyo kutokana na tukio hilo kubwa ambalo halikuwa na chembe ya siasa kwa mwanahabari huyo kwa kuwa hakuwa ni kiongozi wa chama cha Siasa IPC na Chanel Ten kama mwajiri wake na familia tunachukua dhamana ya kusimamia mazishi hayo bila huku tukiviomba vyama vya siasa kutovuruga taswira ya Tasnia hii ambayo kamwe haifungamani ya chama chochote cha Siasa .


Na tunalitaka jeshi la Polisi litoe ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi na za kweli kwa makundi huru yanayoendelea kulichunguza suala hilo.


Kifo cha Mwangosi kimetufanya wanahabari kote nchini kujipanga upya katika kutathimini upya mahusiano yetu na jeshi la polisi .


Mungu ailaze mahali pema roho ya Marehemu Daud Mwangosi. Amin


Francis Godwin

katibu msaidizi IPC

Shukrani;http://www.mjengwablog.com/

Wednesday 20 June 2012

RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU WILLIAM FOFO MAPUNDA!!!!!





WILLIAM FOFO MAPUNDA (FOFO)

MWILI WA MAREHEMU WILLIAM FOFO MAPUNDA UTAAGWA RASMI LEO TAREHE 20/06/2012 NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU TAYARI KWA KUPELEKWA NYUMBANI KWAO MANDA LUDEWA KWA MAZISHI, AMBAYO YATAFANYIKA KESHO TAREHE 21/06/2012 SIKU YA ALHAMISI.

RATIBA:

SAA 5.00 ASUBUHI: - MWILI KUWASILI NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU

SAA 6.00 - 7.00 MCHANA: - CHAKULA KWA WOTE

SAA 7.00 - 8.30 MCHANA: - SALAMU ZA MWISHO (LAST RESPECT)

SAA 8.30 - 9.00 ALASIRI: - MWILI KUFIKA KANISANI (KANISA LA ANGLIKANA TABATA KISUKULU KARIBU NA BAR YA MAZDA)

SAA 9.00 - 10.30 JIONI: - IBADA NA KUAGA KWA WALE AMBAO WATAKUWA WAMECHELEWA NYUMBANI

SAA 10.30 JIONI: - KUANZA SAFARI YA KWENDA MANDA LUDEWA

WILLIAM FOFO MAPUNDA ALIFARIKI GAFLA USIKU WA KUAMKIA JANA NYUMBANI KWAKE TABATA KISUKULU, KWA TAARIFA TULIZOZIPATA KUTOKA KWA MADAKTARI WA HOSPITALI YA AMANA ILALA, KIFO CHAKE KIMESABABISHWA NA KUPATWA NA BLOOD PRESSURE GAFLA.

KWA TAARIFA YOYOTE PIGA NAMBA: 0713-254553

Monday 9 April 2012

MAMA KANUMBA KAFIKA DAR NA RATIBA YA MAZISHI KAMA IFUATAVYO!!

 


WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE  AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA  KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE
 RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P KANUMBA
Habari hii kutoka http://8020fashions.blogspot.co.uk.

Ahsanteni sana.

Saturday 7 April 2012

MAMA KANUMBA AONGEA;Mmmmmhh Pole sana Mama!!!!!!

Mama Mzazi wa Kanumba.
Mmmmhh,Pole sana Mama,Mungu akutie nguvu.
Picha na Video,kutoka ;http://bukobawadau.blogspot.co.uk   Ingia hapo kujua zaidi.Ahsanteni sana.

Ulale kwa Amani Kaka Steven Kanumba!!!!!

Steven Kanumba Enzi za Uhai Wake.
Poleni sana Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani,WaTanzani na Wapenzi Woote Wa KANUMBA!!
Sisi tulimpenda sana Lakini Mungu amempenda zaidi,Tulie na Kumshukuru Mungu kwa Kila jambo,Sote ni Wapitaji katika hii Dunia,Mwenzetu Ametangulia,Inauma sana lakini hatuna Jinsi,Tukumbuke na Kuenzi Mema yote aliyoyatenda.Tuwe tayari wakati wote kwani hatujui Siku wala Muda,Tupendane na Tusameheane.Mungu awatie Nguvu Wafiwa katika Wakati huu Mgumu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE NA LIHIMIDIWE MILELE;
AMINA.

Friday 3 February 2012

Dada huyu Auwawa Kikatili na Rafiki yake wa Kiume!!!!

Da'Rudo Mawere Enzi ya Uhai wake.


Dada huyu ameuwawa na aliyekuwa Rafiki yake wa Kiume/Mpenzi wake, Jason Dube,Naye mwanaume huyo baada ya kufanya mauaji  hayo  huko Ireland,akarudi U.K. naye amekutwa amejiua.Kaka Jason alikuwa akiishi hapa Coventry,Poleni sana Familia ya Dube na Mawere.Habari kamili unaweza kuipata hapa;http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/01 au htt://www.independent,pia ukiingia face book andika Rudo Mawere pia unaweza kupata maelezo vizuri.Habari hii imetuhuzunisha sana kwani huyu mwanaume tulikuwa tunamfahamu.



   


Wednesday 18 January 2012

Ulale kwa Amani da'Regia!!!!!



 Poleni sana Ndugu,Jamaa,Marafiki na Taifa pia.Bwana alitoa na Bwana Ametwaa.

Monday 19 December 2011

Mtoto huyu Auwawa!!!!!!!

Habari hii inasikitisha sana,Pole sana wazazi/walezi , ndugu,jamaa na marafiki, kwa Msiba huu mzito kweni,Mungu awape Nguvu na Uvumilivu katika wakati huu mgumu kwenu.
               Habari na picha zaidi utazipata kwa MASHUGHULI BLOG.Ahsante.

Thursday 13 October 2011

Mazishi ya Mpendwa Wetu; Baba Mzee Juma Penza, katika Picha

                       Marehemu Mzee Penza wakati wa Uhai wake.
     Kaka Mashaka akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Kaka Mustapha akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Kaka Iddy akiweka Mchanga wa Mwisho.
                   Rais Jakaya Kikwete akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Mzee Janguo akiweka Mchangawa Mwisho.
             Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa, akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Wajukuu nao hawakuwa nyuma kufanikisha Mazishi ya babu yao.


Shukrani kwa Wote Mliofanikisha Mazishi ya Mpendwa baba Yetu Mzee Juma Penza[JP].
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI;AMINA.


Rachel-siwa[Mwanapenza]na Timu Yote ya SwahilinaWaswahili;MAJONZINI.




picha kwa hisani ya Michuzi blog,Asante sana.

Saturday 10 September 2011

Poleni sana Wapendwa wetu Zanzibar,Mungu awatie nguvu kwa wakati huu Mgumu!!!

MELI YA LCT SPICE ISLANDERS YAZAMA KATIKA BAHARI YA HINDI PWANI YA NUNGWI LEO USIKU.



Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.
Naibu Waziri huyo amesema meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima,lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unahitajika.Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helkopta yake kwenye eneo la tukio

Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

Habari kwa msaada wa Kapingaz.

Saturday 23 April 2011

Mshumaa wangu Uliozimika!!!!!!!!!

Saa,Siku,Wiki,Miezi.Leo Tarehe 23/04/2011  Imetimia Miaka 17.Tangu ulipotutoka Tarehe 23/04/1994.Baba yetu Mpendwa Mzee M.S.KIWINGA.Ulituacha katika Majonzi/Huzuni na kukata tamaa ya maisha.Lakini Mungu ni muweza wa yote ametusaidia na kusimama tena.Tulikupenda lakini Mungu  mwenyeezi alikupenda zaidi.Daima hatuwezi kukusahau kwa yote na mengi katika malezi yako.Utakumbukwa daima na Mke wako mpendwa,Watoto,Wajukuu,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Majirani.
Shukurani za Dhati ziwaendee Wote walioshiriki nasi katika wakati ule mgumu.Tunaheshimu sana Michango,faraja zenu kwa wakati ule na hata sasa!Pia niwatakie kila la kheri na lililo jema kila siku.
Kwaniaba ya Familiya ya Mzee KIWINGA wa Ilala Sharifu/Shamba,Nasema asanteni sana wote na Tunawapenda.