Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 8 October 2012

PERFECT LADY SALON YADHAMINI SHINDANO LA BONGO STAR SEARCH 2012!!!!!!



 Mkurugenzi wa Perfect Classic Salon (kati mwenye nguo nyeusi) Bi. Ester Kiama akitoa maelekezo kwa mmoja ya wafanyakazi wa Salon yake jinsi ya kumtengeneza mshiriki wa Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012). Perfect Classic Salon imedhamini shindano hilo kwa kuwapendezesha washiriki na kuwapa muonekano mpya wanapokuwa wakiimba stejini.
 Wafanyakazi wa Perfect Classic Salon wakiwasuka na kuwapamba washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 katika jumba lao lililopo jijini Dar.
 Mwanadada Kulwa ambaye ni mtaalamu wa kusuka kutoka Perfect Classic Salon akiwajibika.
 Gabriel ambaye ni mtalaamu wa make up, kucha, kusuka na kuwasokota wale wenye rasta original.
Nae mwanadada Sabrina ambaye ni mtaalamu wa kushona nywele za akina mama (Weaving) akiwajibika.
---
Na Mwandishi Wetu.
 Perfect Lady Salon yadhamini shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 kwa kuwapamba na kuwapa muonekano mpya washiriki wote walio katika kinyanga'anyiro hicho.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kuwatambulisha wadhamini uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Perfect Lady Salon Bi. Ester Kiama alisema kuwa ikiwa yeye ni mtanzania anayependa maendeleo ya vijana ameona ni vyema kujitoa kudhamini shindano hilo kwa kuwapa washiriki muonekano mpya.

"Nafurahi sana kuungana na Bi. Ritta Poulsen kudhamini shindano hili linalovumbua vipaji vya vijana ambapo mimi, nimechukua upande wa kuwapamba washiriki na kuwapa muonekano mpya wawapo stejini," alisema Ester Kiama.

Hata hivyo aliongeza kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuungana mkono pale unapoona mtu anafanya jambo linaloleta maendeleo katika nchi yetu.


Pia Bi. Ester Kiama alisema, Perfect Lady Salon imefungua milango kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya kazi na nao, asisite kuwasiliana nao wanapatikana Kinondoni mkabala na Chuo Kikuu Huria.

Shindano la EBBS linaendelea ndani ya Stesheni ya ITV na sasa wapo katika hatua ya mtoano

2 comments:

emuthree said...

Mambo mazuri hayo ndugu wa mm tupo pamoja

Rachel Siwa said...

Umeona eehh ...Pamoja sana ndugu wa mimi!!!