Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 15 August 2012

Jikoni Leo; Mswahili alilifuata Mtaani;Burudani-MIRIAM MAKEBA - Pata, Pata!!!

  Huu ulikuwa Mchanganyiko[Msetoo], Mchele,spaghetti,Karoti naaaNjegere yaani kama Biliyani,Pilau. haa hhaaaaaa [Mchanyatooo]

 Huyu alipika Nyama iliyochanganywa na Majani siyajui, Ndizi na vingine vingi kama Tulavyo Waswahili lakini Michanganyo yake tofauti kidogo.[Jamaica]


 Hawa waliandaa OLIVE Kwa radha Tofauti, hii mimi nilitaka kurudisha Chenji[sikuweza kumeza]

 Hii ni Nazi, hiyo Nyeupe kabla haija Okwa, hii ya chini imeOkwa nilipenda sana.

 Hawa walitengeneza/kupika kutumia Tambi[Noodles]Ngano na Viungo vya kwao....


 Hawa walitumia Ngano zaidi.Mmmhhh Ngano ina mambo meeengi sana!!

 Waungwana;"JIKONI  LEO"Lilikuwa Mitaani kuona,kujifunza,kuonja tusivyovijua/Mapishi ya watu wa Nchi Mbalimbali.
Kulikuwa na mambo meengi, Leo tuanze na Jikoni.Kuonja ilikuwa Bureeeee ,Duhh nilionja mpaka nilichoka Mmmmhh vingine havionjeki. Nafikiri ni Mazoea ya Vyakula.
Nazi ilitengenezwa kivingine,Ngano ambayo mimi nimezoea kwa Maandazi,Chapati na vitu vichache vya Kiswahili, nayo ilipikwa kivingine.
Duuhh sijui nianzie wapi niishie wapi,wewe kula kwa picha tuu.MCHELE MMOJA Mapishi Mbali mbali..........

Yote tisa Chakula cha Waswahili Hakikuwepo,Sikujua kwa nini labda hawakuwa na Taarifa au Mwezi Mtukufu waliona walaji Wachacheeeee!!
Katika Kutembea watoto wakaniita Mama tumeona Banda la ZANZIBAR!!!!!!Lakini Tumemsalimia kwa KISWAHILI Amecheka tuu,Tukamsalimia kwa Kiinglishi[ENGLISH] Ametujibu.Nilipofika hapo nikakutana na Muhindi Amezaliwa KENYA naye anamuuliza kama ametokea TANZANIA?Kwa KISWAHILI,Duhhh kaka Muuzaji alichekaaaaa.Akasema hajui hiyo Lugha yeye anajua hiyo kitu ZANZIBAR na MASAI Tuu.Baada ya kuongea Nae Akasema yeye ni MJAMAIKA[JAMAICAN] Hupenda kujifunza Mapishi na Mambo ya Nchi Tofauti.

Mimi nikamsalimia MUHINDI Tuka chapa SWAHILI YETU  na TUKAFURAHI.

Jee Unalolote la Kuongezea kuhusu kwanini WASWAHILI Kutokuwepo/Kutokuwa na Banda hapo?
Uoga,Kutojiamini,Hatupendi kujitangaza,Hatuna Muda/Nafasi ,Mwezi Mtukufu,Hatufuatilii nini kinaendelea Sehemu Tunayo Ishi ...AU?
Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

 Hii ilikuwa; COVENTRY.U.K.
 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.


4 comments:

isaackin said...

duh huyo kumbe sio yakheeee toka pale makunduchi!anyway hilo biryani ndio mwake kabisa,na huo msosi alikuchanganyia na majani usioyajua ujue mwenzio kaweka majani bunduki(msuba)ungeonja tu lazima ucheze yeke yeke

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli ukitaka kujua lazima ufuatilie/uulize na utapata mengi. Nimefurahi kuona JIKONI LEO imetoka na kutuletea mambo mazuri mapya...Nadhani waTZ ni waoga hatupendi kuitangaza TZ yetu au ni ile nikipika labda hakuna atakayeonja...

Rachel siwa Isaac said...

Hahhahahah kaka isaackin ningecheza Yeke yeke yeketeeeee.si Yakhee wa makunduchi ndugu yangu.

@da'Yasinta[Kadala]nakubaliana nawe lazima ufuatilie/uulize.

Asante kwa kujibu/kutoa maoni yako mama Erik.

EDNA said...

Yamyam... udenda unanitoka na huo mseto hapo juu.