Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 1 July 2012

J'Pili ya leo, Tujifunze kupitia kaka Mubelwa na Mch.F.Shideko !!!!!!!!



Kaka Mubelwa Bandio[Mzee wa Changamoto]

Sijawahi kuhusika na mwisho wa maisha ya mwanadamu kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Kaka Domitian Rutakyamirwa. Na katika kuhusika huku, (tangu kuugua mpaka harakati zilizofuata baada ya kifo chake) nimegundua na kujifunza mengi kuhusu mtu, utu na watu. Ni kwa kupitia maisha ya mwisho ya Kaka Domi, nimeweza kujiakisi na kuakisi mengi yanayoendelea katika maisha yetu wanadamu na kuweka bayana “ndivyo-sivyo” ya maisha yetu.
Binafsi nimeshuhudia maisha yangu yakikaribia kifo tena cha ghafla katika matukio tofauti na bado sikuona ama kujifunza nililojifunza sasa.
Nakumbuka kauli ya mwisho niliyoisikia ikitoka kinywani mwa Kaka Domi ni ile ya kutubu aliyoongozwa na Mchungaji akiwa wodini.
Katika matukio yote niliyokumbana nayo, na ambayo wenzangu baadhi walipoteza maisha, hakuna kati yao aliyepata nafasi ya kutubu na kumuomba Mungu kama alivyofanya Kaka yangu huyu.
Na kama alivyohubiri Mchungaji kwenye ibada ya mazishi, mambo makuu matatu aliyosisitiza ni kuwa
1: Hatujui tutaondoka lini.
2: Hatujui tutaondokea wapi.
3: Hatujui tutaondoka vipi
Domitian, aliyekuwa Kaka, rafiki, Mume, mzazi na mlezi kwa wengi aliishi maisha ambayo yamekuja kudhihirika katika wakati wa uhitaji wake.
ASANTENI NYOTE
Maisha ya Domi yamedhihirisha UMOJA unaotamaniwa na waTanzania hasa wa Washington DC na vitongoji vyake ambao kwa namna moja ama nyingine unakwamishwa na mambo mbalimbali, lakini pale inapotokea tofauti zetu zikawekwa kando kwa ajili ya

 mtu aliyekuwa nasi sote licha ya tofauti zetu, tunaona matunda ya umoja. UMATI unaojitolea kufanikisha jambo kwa namna ya kipekee sana.

Inaendelea.ingia http://changamotoyetu.blogspot.co.uk
                             Marehemu;Domitian Rutakyamirwa; Ulale kwa Amani.[Rafiki wa kaka Mubelwa]

Mahubiri ya Mch. Ferdinand Shideko kwenye ibada ya kumuaga Ndg Domitian Rutakyamirwa iliyofanyika Jumatano June 27, 2012 kwenye kanisa la
The Way Of The Cross Gospel Ministries (at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 2074

U.S.A

Wapendwa; muwe na j'Pili yenye Amani,Baraka,Pendo na Umoja.

Samehe Usamehewe,Mungu atusaidie katika Msamaha!!!!!

            "Swahili NA Waswahili" Nimesamehe na Nawapenda Wooote!!!!!!!

3 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

ni kweli kuna mafunzo makubwa hapa...astarehe kwa amani!

Mija Shija Sayi said...

Si uongo hata kidogo..

Mungu amlaze mahala pema peponi, amen.

Yasinta Ngonyani said...

ASTAREHE KWA AMANI!!