Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 27 January 2012

Watoto wa Kiume na Wakike Wanamajukumu Sawa?


Nimatumaini yangu woote Muwazima!!!na Kama kunamgonjwa Pole sana na Mungu akuponye.
Waungwana Eti watoto wa kijijini wa Kiume na Wakike wanamajukumu sawa?Yaani si lazima wote waende kuchota maji pamoja,basi kama huyu anafagia mwingine aoshe vyombo,na ikifika saa ya kujisomea wote wanasoma,ikifika saa ya kucheza wote wanacheza.Najua kila familia inamalezi yake,Jee vipi kwa malezi ya kileo huko kijijini yameweza kubadili muonekano/Majukumu ya watoto? kama si kijiji kizima basi kuna nafuu?na kama hakuna jee tunaweza kuwasaidiaje?Sawa Mwanamke ni mwanamke, Mwanaume ni Mwanaume hilo naliheshimu pia.Jee Vipi na Watoto hawa wa Mjini?

Karibuni sana Wapendwa, kwa Mawazo,Ushauri,Kuelimishana  kwa Upendo.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mtazamo au kwa uzoefu wangu mimi naona hakuna kazi ya msichana wala mvulana...Ni vizuri kuwalea watoto sawa kwani ipo siku wote itawabidi waishi maisha peke yao je? itakuwaje kama mvelana hawezi kufagia au kuosha vyombo?

Swahili na Waswahili said...

Dada Yasinta vipi wewe ulipoenda nyumbani hivi karibuni ulikuta kunamabadiliko kidogo ya malezi, ukilinganisha na ulivyokuwa wewe?