Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Monday, 12 December 2011

Watoto wa Kiume na Mitindo!!!!!!

                                        Kaka Mohamed kapozi
                                  hapa na Tabasam
                                              hapa katulia.
Wapendwa Watoto wa kiume na Mitindo yao!!Nakumbuka zamani kulikuwa na Kaunda Suti,Ngwabi,Mchelemchele,Jinzi za Chatu/kujikunjakunja hivi,Mashati ya drafti na nyingine nyingiii,pia watoto wengi walikuwa wanashonewa hizo Suti kwa Fundi tena SareSare,Viatu Moro shoes,Vimokasini,Raba Mtoni, Ndopa/Lakupanda.Pia kulikuwa na viatu vya Bora sijui kama bado lipo hili duka.Pia naona kama mitindo inajirudia .

Wewe unakumbuka nini/kuvutiwa na nini vya wakati ule na Wakati wa sasa jee?

Karibuni sana Waungwana!!!!!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kweli watoto wa kiume na mitindo..umesema mitindo yote wewe mdada...ila labda ...ngoja kwanza nifikirie..