Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 23 October 2011

Mwanamke na Kujiamini!!!!

Wanawake Tufunguke,Tujitoe,Tuamke,Tushikamane,Tupendane,Tuelimishane,Tujifunze na Tujiamini,
Hakuna kitu rahisi, Lakini ukiamua na kujituma utafanikiwa, Hatua moja huanzisha na nyingine,Tusisite kuulizana na kuomba Ushauri pale unapoona umekwama.Pale ulipo na unaweza kufanya kitu ili kusaidiana na kina baba pamoja na Familia,Jamii. Kila mmoja anamuhitaji mwenzie kwanamna moja au nyingine,Kama wewe unafanya kazi na kuna mwingine anafanya biashara.Unaweza kutamani Vitumbua na pengine unajua kupika lakini umechoka au hujui basi kuna mama yupo nyumbani yeye anapika na akakuuzia nayeakapata pesa kidogo nawe umepata mlo,Binadamu kila mmoja anajua hiki na mwingine anajua kile.WANAWAKE TUSILALE.

Nawatakia Jumapili Njema!!!.


12 comments:

Anonymous said...

Asante, ni ujumbe mzuri sana, ubarikiwe

Yasinta Ngonyani said...

Ni ujumbe mzuri sana na kwa kweli hivyo ndivyo inavyotakiwa ..wanawake tunaweza kama tukiamua. Ahsante da´Rachel!

Mija Shija Sayi said...

Ni kweli kabisa dadake...na kwa kuongezea hapo tusisahau kuomba Mungu atutangulie katika kila hatua ya maamuzi yetu na hapo ndipo mshikamano wetu utakapokufanikiwa zaidi...

Shukrani Mrs Isaac!

Swahili na Waswahili said...

Asanteni wapendwa,Amina da'Mija ni kweli Mungu ndiyo wa kwanza kwa kila jambo @Mwinjiristi wangu!!!!!

Anonymous said...

Mama waswahili na waswahiluna asante kwa ujumbe mzuri kwetu kina mama lakini mimi naona mbona dunia ya leo hii ya utandawazi hasa huku first world wanawake wamefunguka? isipokuwa kama unaongelea wale ambao mila zao na mazingira yao(mfano wenzetu magabachori na baadhi ya majirani zetu wasonjo) yanakuwa kifingo chao.

Ni ujumbe mzuri wa kusisitiza tuzidi kujiamini but we need to hear something more than being confident. Tunaomba zaidi ya hayo please nakuaminia mama yangu. Tufanye nini ile tuwe juu although by nature tuko chini ya wababa. LETE DARASA!!!

Ni mimi mchokozi

guess who???? Ukishindwa nipe mji

God bless you

Swahili na Waswahili said...

kwikwiwkikwi duhhh madau Mchokozi nakupa Miji chukua Mwanza au Tanga!!!

Asante sana kwa ushauri wako,TUKO CHINI YA WABABA, OK mpendwa nitaweka hiyo,Ubarikiwe nawe na karibu tena na ningependa kukujuaaaaaa.

Goodman Manyanya Phiri said...

Uzuri wa kupigania haki yako ni kwamba, hata unaposhindwa, ALAMA LAZIMA UNAACHA!

Mija Shija Sayi said...

Heehee..heeee!! Hilo nalo neno Kaka Manyanya.

Swahili na Waswahili said...

dadake hicho kicheko naona neno limekugusa hilo, duuhhh kaka Manyanya kweli ALAMA LAZIMA UNAACHA, Asante sana kaka yangu, msalimie mwananga Tamara na da'Happy, nieona video mmoja unaongea lugha kama tatu hivi kweli wewe kiboko!!!

Anonymous said...

Kwikwikwi!!!! Mchokozi nimerudi mji hujapatia na offer ya kutoa mji has been withdrawn. Sasa kazi kwako ila uchokozi utaendelea, nitaendelea kukuchemsha mpaka ukipatepate.
But never mind keep smiling coz God loves you and me always.
Kazi kwako!!!

Ni mimi mchokozi

Swahili na Waswahili said...

Kwikwikwikwi Mchokozi utafanya nywele zininyonyoke kwa kuwaza kama Ga....d.f,nipe nafasi ya mwisho nenda Mbeya @Mdau Mchokozi!!!!!!

Absolutely Awesome Things (AAT) said...

Ushauri mzuri,asante sana