Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 5 October 2011

KITENDO TULICHOKILAANI KUTENDEWA MKUU WA WILAYA IGUNGA CHAJIRUDIA TENA, NANI WA KULAUMIWA.







Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.

Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.

Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?

Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.

KAPINGAZ Blog haifungamani na chama chochote cha kisiasa, Tungependa kuwasikia TAMWA, TGNP na Taasisi nyingine za kijinsia  mkikemea na kuvilaani vitendo hivi.  Tulitegemea kitendo kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya kinaweza kikawa funzo pia kwa askari wetu lakini tunaona bado kinarudiwa tena.

            Imetumwa na KAPINGAZ Blog.

3 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Mjadala huu wa kijinsia unasisimua kweli. Labda akinamama wa vyama vyote wanahitaja kuungana wafanye maandamano ya kijinsia (na hao polisi wakiume wakija kuwakamata akinamama wavue nguo wenyewe.. tena zote... na tuone wataendelea kukamatika au la)

Na kweli, wakati mwingine dawa ya moto ni moto tu!

Rachel Siwa said...

Ni kweli usemayo kaka Manyanya, huu ni unyanyasaji.

Goodman Manyanya Phiri said...

Kwa sasa hivi lakini, mtu yeyote anaetishiwa kubebwa na polisi namna ile anaweza kuzuia balaa hilo ila kwa kuchukua hatua mbili zifuatao.

1. Ziba kinywa na usibishane hata kidogo ukiwaona polisi wamechachamaa.

2. (na hili ni mhimu zaidi) USIWAANGALIE NDANI YA MACHO BALI TAZAMA PEMBENI AU CHINI wanpoanza kukutukana.


Ukifanya hivyo, utaponea kupigwa katika mazingira mengi zaidi ukiwa mwanamke au mwanamume. Mbinu hizo zinatusaidia sana Afrika Kusini kwa madereva wenzetu wenye hasira barabarani na watu wengine wanapigwa mabastola na kufa kwa ujinga wa kuendelea na kubishana na vichaa hao wa barabarani (ROAD RAGE)

Asante kwa posti nzuri, Dada!