Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 14 September 2011

Wanaume na Mitindo,Leo tupo Igunga!!!

                       Huyu baba kavaa shanga na katupia kikoi.
                Kijana Kasuka,shanga hakukosa na katupia kikoi,anasalimia kwa mapozi kabisa.
              Hawa wamejifunika vikoi, sijui hii ya mwisho nyeusi ni kaniki au....
Haya wapendwa Leo tupo Igunga,Tanzania.Kama uonavyo wanaume wa huko na Mitindo.
Sijajua kama hii ndiyo Mitindo ya Asili au yakisasa,Maana nasikia kunamitindo ya Asili,kama ndivyo,
Hongereni kwa kuendeleza Mila ambayo wengine wanameacha.

Wapendwa sina la zaidi nawasikiliza ninyi, Vipi kuhusu mitindo hii wewe unaionaje?
Na je kama Mitindo hii niya kiasili vipi kwenye Harusi au Sherehe za Kitaifa mtu akitinga si itakuwa mwake?

Karibuni sana Waungwana.2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi kama mimi nimependa sana hiyo maana wanaendeleza uasili...na kwangu mie akitokea mtu kwenye harusi kavaa hivyo nitaona raha sana kuliko hizo suti hii ni mimi:-)ruksa kuwa tofauti

Anonymous said...

yaani kwa sisi wasukuma hiyo nipoa sana, maana tunakandamizaga kwa kwenda mbele bila woga. kwa maana mavazi kama hayo kule kwetu ni babeja sana yaani kabisakabisa.