Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili,Pamoja Daima!![Tuache kuua Ndugu zetu kwa Imani mbaya;Hawa ni Wapendwa Wetu/Ndudu Zetu,Kuwalinda na Kuwatunza ni Jukumu Letu..!]#Tuache Kuua#Walemavu wa Ngozi#Tanzania.!!

Wednesday, 16 March 2011

Kuna Wanaojikondesha na Wanaokonda si kwa Kupenda!!!!!!!!!!!!!

Wapo  wanaotamani  hata Uji wa chumvi na hawapati,Wapo wanaoweza kupata chakula chochote watakacho,lakini hawali kwa sababu wanafanya Diet. Wapo wafujaji, waharibifu na wachoyo.Wapo wanaopenda kusaidia waliokosa lakini wana vichache.Binadamu tujenge tabia ya kusaidiana / Kutoa ni Moyo si Utajili!!!!! Wewe unamawazo/mchango  gani katika hili? Karibu tuelimishane Wapendwa!!!!

8 comments:

Mcharia said...

Ili uweze kufanikiwa maishani unatakiwa uwe na mipango ya maisha yako.
Mara nyingi watu wengi wamekuwa ni hodari wa kupanga mipango ya harusi na mambo mengine madogo madogo lakini wanasahu kupanga mipango ya maisha yao.
Kama huna mipango juu ya maisha yako si rahisi kupata mafanikio, hivyo basi matokeo ya kila jambo hutokana na mipango uliyonayo ilivyo.
Japokuwa kweli kihali kuna wasio na kitu hata hivyo ni ujinga wetu kudhani kuwa kila mmoja anacho kitu. Fikra na mitizamo tuliyonazo hazikubali kuwa tu wabinafsi.
Ni mtizamo wangu kuwa tuna ujinga busara ambayo tuna kazi kubwa ya utambuzi na kujitambua.

Fita Lutonja said...

Katika kupenda binadamu tumeubwa tofauti kwani wapo wenye mali nyingi lakini hawezi hata kumsaida ombamba wa jiani lakini wapo wenye shida lakini akiona mtu mwenye shida zaidi yake anamsaidia.

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana kwani kuna wakati unaona mtu hadi anaamua kujitapisha ili akondo kwa ajili ya muonekano. Wakati wengine wanakufa njaa. Mara nyingi nimekuwa najiuliza hivi hii dunia ni mwisho wake au vipi?

Mija Shija Sayi said...

Ndio dunia ilivyo, ukiwa navyo huoni hadi pale unapovikosa ndo unafunguka macho. Kwa kweli suala la kusaidiana ni la msingi sana ila watu siku hizi tumejaa ubinafsi mtupu.

EDNA said...

Binadamu tumetofautiana,mwingine anaweza kuwa na kila kitu navingine hata akawa hana uhitaji navyo,yupo radhi atupe kuliko kumsaidia yule mwenye uhitaji.

SIMON KITURURU said...

Lakini labda BINADAMU alivyo na TABIA ZAKE ni mipango ya MUNGU- kama unaamini MUNGU.

Na uchoyo, UFUJAJI , kupenda kusaidia, KUPENDA kusaidiwa tu - na mambo mengine yote mpaka ya ufikiriaji wa kujikondesha ili kupendeza au kujinenepesha angalau tako liwe kubwa kwa MCHINA ili KUPENDEZA yote ni tabia ambazo zina umuhimu wake kuwepo ili BINADAMU abakie BINADAMU na DUNIA ibakie kuwa DUNIA na si MBINGUNI.


Kama kila mtu angekuwa ni mtoaji labda kunaathari zake ambazo zingejitokeza kama tu kila mtu angekuwa kashiba tu wakati wote ijulikanavyo kuwa na athari zake katika Psyche ya BINADAMU .

Na inasemekana swala zima la UKOMUNISTI wa SOVIET UNION na hata ujamaa na kujitegemea /vijiji vya ujamaa wa NYERERE vilikuwa ni kujaribu kufanya watu wawe na tabia , fikira na hali zinazofananafanana kitu ambacho kilionyesha kushindwa.


Na inasemekana hata KUFA kwa binadamu ni muhimu kwa dunia lasivyo tungebanana hapa duniani na labda hata kwa BINADAMU kujiongezea miaka ya kuishi tayari athari zake kwa DUNIA zinaonekana tayari moja wapo likiwa ndio hilo la baadhi kukosa msosi,...


... MIBWABWAJO yote hiyo hapo juu ni katika kuwaza kwangu kuwa labda kila kitu kina sababu zake na wakati kutoa ni MOYO na si UTAJIRI,...
... labda kutotoa nako kunahitaji MOYO na kunamakusudio yake ambayo hayapo katika tabia za BINADAMU kibahati mbaya.

Na ni kwanini kuna WENYENAVYO waonao wafao na njaa lakini kwa moyo wanawanyima mmsosi labda ni kitu kihitajicho MOYO kwa kuwa kama una roho ndogo huwezi kuacha mtu afe wakati unajua unaweza kusaidia asife.


Swali la kizushi:
Hivi ni kweli kuna mtu anayeweza kusaidia kuokoa mtu asife?

Ya MUNGU ni mengi na labda kama yaliumbwa na MUNGU kuna uwezekano hayapo ndani ya BINADAMU kwa bahati mbaya -kama tu isemekanavyo ni MUNGU aliyemuumba SHETANI na labda makusudio ya kuwa na SHETANI hapa ulimwenguni sio kitu cha bahati mbaya kwa kuwa kina makusudio yake labda na ni MUNGU MWENYEWE ndiye ajuaye.

Swali:
Si uwepo wa wasiosaidia watu labda ndio moja ya kilichoibua hari ya kusaidia watu wengine hata itolewayo kwenye kipengele hiki?

Na si kwa kuwa kuna mabahiri wachoyo labda moja ya dhumuni lake ndio hili tunafunzwa na Dada Rachel ``KUTOA ni moyo na si UTAJIRI?´´


Ndio,..
... nawaza tu kwa sauti!

Swahili na Waswahili said...

Kwa Wachina yapo @kaka Kitururu!
Asante sana kaka nimekupata vyema!
Tuendeleee!!.

chib said...

Hizo taswira mbili zinatia imani sana!