Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 25 January 2011

Wanaume na mitindo!!!!!!!!!


Kumekuwa na mitindo mingi ya wanaume kama,kusuka,kunyoa kipara,kuweka rasta,kuvaa hereni na mingine mingi!jee mitindo hii inaendana na umri wa mtu?
15 comments:

Koero Mkundi said...

Nomba nijitambulishe.....Naitwa Koero Mkundi

Yasinta Ngonyani said...

Haha ha haaaaa! yaani nimebaki nashikilia mbavu kasuka kilimanjaro kama sikosie...tuendako sasa...hapana haiendani na umri wala mtu..labda tuseme mila na desturi.

Mija Shija Sayi said...

Haaa! Da Rachel, nami umenichana mbavu na huu mtindo, halafu post hii nimeifananinsha na ile ya Yasinta ya Mavazi ya Wanawake.

Kwa kweli mimi naona wanaume wanapotoka sasa...au?

Mcharia said...

Ni uvamizi tu wa mambo. Wanawake kuvaa suruali-eti leo kuna suruali za kike.

Jiulize TENA. Inashangaza kumuona mwanamke ana ndevu (usicheke!!)

Sasa, wanaume nao Duh kusuka bwana na hereni. Hivi niiteje kati ya maadili kumomonyoka, mwisho wa dunia, mitindo huru, ulimbukeni na na naaaaa..

Umeme nao umekatika, sorry!

Swahili na Waswahili said...

Aksante @da Koero karibu sana nimefurahi kukuona!.

@da Yasinta na da Mija jamani mbona hivyo mnamcheka?

@kaka Mcharia lakini ndevu si zinaota zenyewe tuu au zipo za kubandika? Umeme nao umeharibu mambo!!natumaini ukirudi utamalizia ulipokomea ili tujifunze zaidi!!.

EDNA said...

Hahaaa hiyo style mie hoi, kweli bwana mitindo mingine inaendana na umri,embu imagine unakatiza kariakoo unapishana na kibabu cha miaka 70 kimesuka nywele..mweee

Anonymous said...

Hehee! Mambo ya mitindo hayo, nywele ni nyeusi, sijui zake au msuko umebandikwa! Mimi naona watu wanabadilika kulingana na wakati, sasa hivi utaona ni vijana wengi ndio wana mambo ya hereni na kusuka, ukikutana na mzee utashangaa kuliko, tunakoelekea itakuja kuwa kitu cha kawaida pia hatutawashangaa hata wazee wakisuka. Huu ni uhuru uliopitiliza, watu wa zamani wakisema wataambiwa wamepitwa na wakati. Inabidi wazee wetu wafanye kama vile hawaoni, ila na uhakika wanaumia sana moyoni.

SIMON KITURURU said...

Mara nyingi kiasili mitindo ya nywele KIAFRIKA iliendana na umri na nyazifa pia na zilitofautiana kutoka jamii na jamii.

Na usishangae kuwa hiyo staili pichani ndio staili ya chifu wa kabila fulani tokea mamia ya miaka iliyopita.


Makabila yanatofautiana,...
.... kwa mfano kwa WAMASAI ni vijana wa kiume ndio husuka kimila ila staili ambazo zinafanana na twende kilioni au mabutu kwa wanaume zipo tu tokea zamani katika jamii za KIAFRIKA.

Pia tukumbuke staili nyingi za nywele sasa hivi zimeathiriwa na mitazamo yakutoka nje ya Afrika kutoka kwa waliotutawala.Kitu kifanyacho STAILI za KIAFRIKA kushangaza WAAFRIKA kwa kuwa WAAFRIKA wenyewe wanaangalia staili za KIAFRIKA kutokana na jicho la KIZUNGU au KIARABU na tafsiri zao.:-(


Hii hufanya kuna watakao ona kuvaa wigi ni poa kwa kuwa humfanya msichana kuwa na nywele kama za watawala waliozoeleka kuliko kwenda ofisini na mabutu ambayo ndio ya Kiafrika.


Hili pia huathiri kwa wanaume pia kwa mfano ukiwa na Rasta kama mimi kuna kazi ndio itakuwa chanzo cha kukataliwa na mwafrika mwenzako kuliko ungekuwa hata na kalikiti nyweleni au tu unabonge la wei,...
... na yote inachangiwa kinamna na mitazamo kutoka kwa waliowahi kututawala WAAFRIKA ambao ni WAAARABU na WAZUNGU.

Kwa mfano BABA yangu hata nifanyeje tumekubaliana kupingana ila yeye na nywele zangu ni mbalimbali ingawa enzi zake na akina Kambona ilikuwa heshima kabisa kupiga ma wei kwa kwenda mbele kwa kuwa kinamna waliamini kunafanafana na staili za akina Bwana mkubwa.

Mwisho:
Tafsiri ndio tatizo katika staili za nywele . Na tafsiri ni kitu cha kujifunza kwa hiyo kila mtu na kichwa chake.

Kwa maana kuna njemba zenye bonge la chogo na kunyoa kipara kabisa kuna watakao tafsiri ni noma.

Kunyoa kabisa pia kunawatafsirio mtu ni mvuta bangi au UMEFIWA kama tu waaminivyo wengine kila mwenye rasta lazima tu anaungua au kichaa.

Na kwa vyovyote jamii inamchezo wa kuhukumu na kama mwoga nashauri fuata jamii ifuatayo na staili bora kwa wanaume ni zile zikubaliwazo tu kwa wafanyao kazi BENKI Afrika. Kwa hiyo kama unataka staili ikubaliwayo kijamii ,iga wafanyakazi wa benki.

Lakini,...
.... naamini hakuna CHA ZAIDI kiumuhimu kiunganishacho UMRI na STAILI za nywele zaidi ya TAFSIRI TU za watu katika JAMII uliyopo.Na jamii tofauti zitakutafsiri tofauti kwa ulivyonyoa nywele hasa kama mchango wako kwenye jamii ujulikanao hauna sauti kubwa kuliko staili yako ya nywele.:-(

Ndio,...
.... Mandela alivyokuwa hachomekei shati uheshimiwa wake ulikaa palepale na naamini angekuwa anasuka mabutu watu wangetafuta vielelezo mpaka vya uchifu wa kabila lake na heshima yake ingekuwa palepale. Ila mwenzangu na mimi ukiingia kichwa kichwa watu wanaweza wasikuelewe na kama maisha yako yanategemea watu wa aina hiyo unaweza ukaumia.


Mfano:

Naamini ningekuwa naishi BONGO na nategemea maishani kuajiriwa na BENKI fulani au angalau kuingia kwenye fasheni ya kugombea UBUNGE ,...
... labda ningekuwa nachana nywele nifanane fanane na waheshimiwa!:-(NI mtazamo tu!:-(

Swahili na Waswahili said...

Aksanteni wapendwa kwa maoni yenu!
@haah da Edina ukipishana nae k`koo unamwambia mabo au shikomoo!!!!nyee.

@Anonymous vipi mzee anarudi na unakuta anakamtindo kama hako hhaaaa!

@kaka Kitururu nimekupata haswa mzee yeye na wei lake mbona mama Kiruru alimkubalia tuu?hahhaha ya bwana mkububwa!!!!

Mija Shija Sayi said...

Unajua huyu mzee ana akili sana, yeye kaamua yote mawili KUSUKA NA KUNYOA kweli watu kiboko.

Swahili na Waswahili said...

hahahaaa da Mija leo umempatia jibu!
vipi baba watoto naye akijaribu hako kamtindo?

Mija Shija Sayi said...

@Rachel, unamaanisha kaka Isaack???????

Swahili na Waswahili said...

hahahha@Mija noo baba Manjulaaaaaaaaaa!!!!!!

Anonymous said...

Mie huyu bwana sijui ni kutoka Ghana? Simshangai sana yawezekana ikawa ni utamaduni wake na pia yaonyesha status aliyonayo kwenye jamii/kabila lake. That's the beauty of AFRICA. AFRICA ya sasa wanaume wanavaa na kuwa na hair style tofauti kabisa na ile ya zamani. Nakumbuka miaka ya 1980s kipindi tuko Windhoek (Namibia), kuna kabila wanaume walikuwa wananyoa upara wa wembe halafu kijisehemu kilichobakia kinasukwa. Hivi sasa ukienda yabidi uende vijijini ndio utakuta wanaume bado wanakasuka, elimu na dini ya wageni imechangia sana wanaume wa kabila lile kubadili muelekeo wao wa maisha kuanzia mavazi, hair style hadi vyakula. Na hiyo si Namibia peke yake hata Tanzania itafikia kipindi hutomuona mwanaume wa maeneo ya unyanyembe hadi kote Shinyanga anasuka nywele. Zamani wanaume wa kigogo walikuwa wanatoga sikio na kuvaa heleni, miaka michache ijayo hata huo utamaduni nao utapotea. Nafikiri sasa wamebaki wachache sana.

Mdau toka UK

Swahili na Waswahili said...

Mdau wa uk nimekupata vyema!karibu sana kwa michango yako na kuelimishana!.