Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 17 March 2016

TANZANIA RED CARPET YAFANA SEATTLE, WASHINGTON STATE


Mama mitindo Asya Idarous Khamsini (kati) akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wake wa mitindo kwenye usiku wa Tanzania Red Carpet uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 mjini Seattle jimbo la Washington na kuhudhuriwa na Watanzania wanaoishi jimbo hilo na marafiki zao.
Mama mitindo Asya Idarous Khamsini akipata ukodak moment.
Wavaaji nguo za mitindo wakipata picha ya pamoja na mama mitindo Asya Idarous Khamsini.

Tuesday 15 March 2016

Ujumbe wa JWTZ watembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC (11 Machi, 2016)

Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kikeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.
 Pichani kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda



HARAMBEE YA KUMCHANGIA MARIAM HUSSEIN YAFANYIKA DMV




Mariamu Hussein akihudhuria harambe ya kumchangia iliyofanyika siku ya Jumamosi Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na WanaDMV na marafiki zao. Mariam Hussein nasumbuliwa na ugonjwa wa saratani.


Vitu mbalimbali vilivyoletwa na WanaDMV kwa ajili ya kuvipiga mnada kwenye harambee iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

WanaDMV na marafiki zao waliohudhuria harambee ya Mariam Hussein (wanne toka kushoto) iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
Baadhi ya WanDMV wakiendelea kupata mapochopocho  kwenye harambee ya kumchangia Mariam Hussein (hayupo pichani) iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
Mariam Hussein (kati) akiwa na familia yake kwenye harambee ya kumchangia fedha za matibabu ya saratani iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016
Mnada ukiendelea 
Vitu mbalimbali vilivyoletwa katika mnada wa harambee ya Mariam Hussein uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, maryland nchini Marekani.
Mariam Hussein (kati) akifuatilia Harambee ya mnada wa kuwezesha kupatikana kwa fedha za matibabu ya Saratani siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, maryland nchini Marekani.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja

Sunday 13 March 2016

Wapendwa Natumaini Jumapili ni Njema;Burudani-Anchor - Hillsong Live,My God is Awesome - Charles Jenkins,Break Every Chain (Live) - Tasha Cobbs,


Wapendwa;Ni Jumapili nyingine tena Mungu ametupa kibali cha kuwa pamoja tena....
Natumai wote wazima na jumapili ilikuwa/inaendelea vyema..
Tumshukuru Mungu kwa kila jambo,Hakuna na hatokuwepo kama yeye..

 "Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake."
Neno La Leo;Wagatia:6:1-18
Tuvumiliane na kusaidiana
1Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, nyinyi mnaoongozwa na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa. 2Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.3
                      3Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe. 4Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5Maana kila mmoja anapaswa kuubeba mzigo wake mwenyewe.
                        Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake.
7Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna. 8Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uhai wa milele. 9Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake. 10Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu.
                           Mawaidha ya mwisho na salamu
11Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe. 12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha nyinyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: Kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.13Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; huwataka nyinyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu. 14Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu

        15Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya.16Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli – watu wa Mungu.
17Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo mwilini mwangu ni zile za Yesu.
18Ndugu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amina.










"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday 6 March 2016

Natumai JumaPili ilikuwa njema;Happy Mother's Day..Burudani-Miriam Paul-Nipe Macho,Mvua ya Baraka......



Wapendwa waungwana; Habari za siku nyingi,Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na mwaka huu mpya..
Tunamshukuru Mungu kwa yote,Mungu yu mwema sana..nimeadimika kidogo mambo ni mengi familia imeongezeka
basi na majukumu yameongezeka,Lakini Mungu yu pamoja nasi na tupo pamoja tena..
Natumaini jumapili ilikuwa/inaendelea vyema
turudishe utukufu wa Mungu muumba wa yote...
"Happy Mother's Day" kwa wamama wote, Mungu atupe hekima,Busara katika Malezi ya Watoto wetu..
Mungu pia awaguse wenzetu wanaohitaji watoto ,akawape furaha hii nao wakafurahi pamoja na wengine..
Pia akawape sawasawa na mapenzi yake..
kuna ambao hawana kabisa ,Mungu yu pamoja nanyi,
Kuna walionao wa jinsia moja kike/kiume ,Mungu anamakusudi yake.
Kuna walionao lakini hawawajali/wameterekeza.Mungu awaguse mkumbuke majukumu yenu...

1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:

2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?


 Neno La Leo;Methali 31:1-31

Mawaidha kwa mfalme
1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:
2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?
3Usimalize nguvu zako kwa wanawake,
usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
4Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai,
wala wakuu kutamani vileo.
5Wakinywa watasahau maagizo ya sheria,
na kuwanyima haki wenye taabu.
6Mpe kileo mtu anayekufa,
wape divai wale wenye huzuni tele;
7wanywe na kusahau umaskini wao,
wasikumbuke tena taabu yao.
8Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;
na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,
linda haki za maskini na fukara.




Mke mwema
10Mke mwema kweli, apatikana wapi?
Huyo ana thamani kuliko johari!
11Mumewe humwamini kwa moyo,
kwake atapata faida daima.
12Kamwe hamtendei mumewe mabaya,
bali humtendea mema maisha yake yote.
13Hutafuta sufu na kitani,
na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara:
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka kabla ya mapambazuko,
akaitayarishia jamaa yake chakula,
na kuwagawia kazi watumishi wake.
16Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,
na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
na kuiimarisha mikono yake.
18Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;
hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,
kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20Huufungua mkono wake kuwapa maskini,
hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,
maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22Hujitengenezea matandiko,
mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,
anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,
huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25Nguvu na heshima ndizo sifa zake,
hucheka afikiriapo wakati ujao.
26Hufungua kinywa kunena kwa hekima,
huwashauri wengine kwa wema.
27Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,
kamwe hakai bure hata kidogo.
28Watoto wake huamka na kumshukuru,
mumewe huimba sifa zake.
29Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,
lakini wewe umewashinda wote.”
30Madaha huhadaa na uzuri haufai,
bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.
31Jasho lake lastahili kulipwa,
shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.

                Bible Society of Tanzania
Jifunze zaidi









Mungu awabariki wote mliopita hapa,
muwe na wakati mwema.








"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.