Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 20 September 2015

Muendelee Vyema na Jumapili hii;Burudani-Martha Mwaipaja,Tulikotoka ni Mbali, Kwa Msaada Wa Mungu,Bwana ni Nuru.......(Have a nice Sunday)


Wapendwa/Waungwana;Nimatumaini yangu jumapili ilikuwa njema/Inaendelea vyema.
Pole kwa wote walio wagonjwa,waliopatwa na misiba,wenyeshida/tabu,Waliokwenyemapito/mitimahani MUNGU akaonekane juu yao.

1Wakati huo Saulo alikuwa akizidisha vitisho vikali vya kuwaua wafuasi wa Bwana. Alikwenda kwa kuhani mkuu,2akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
3Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote.4Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: “Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?” 5Naye Saulo akauliza, “Ni nani wewe Bwana?” Na ile sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa. 6Lakini simama sasa, uingie mjini na huko utaambiwa unachopaswa kufanya.” 7Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja na Saulo walisimama pale, wakiwa hawana la kusema; walisikia ile sauti lakini hawakumwona mtu. 8Saulo aliinuka, na alipofumbua macho yake hakuweza kuona chochote; hivyo wale watu wakamwongoza kwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko. 9Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakati huo hakula au kunywa chochote.

Neno La Leo;Matendo Ya Mitume 9;1-43
Kuongoka kwa Sauli
(Mate 22:6-16; 26:12-18)





10Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.” 11Naye Bwana akamwambia, “Jitayarishe uende kwenye barabara inayoitwa Barabara ya Moja kwa Moja, na katika nyumba ya Yuda umtake mtu mmoja kutoka Tarso aitwaye Saulo. Sasa anasali; 12na katika maono ameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani na kumwekea mikono ili apate kuona tena.”13Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kutoka kwa watu wengi; nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watu wako huko Yerusalemu. 14Na amekuja hapa akiwa na mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwa jina lako.” 15Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli. 16Mimi mwenyewe nitamwonesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu.”
17Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka mikono yake juu ya Saulo, akasema, “Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu.” 18Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka machoni mwa Saulo, akaweza kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia.

Saulo anahubiri huko Damasko
Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko. 20Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. 21Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, mtu huyu si yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu hao na kuwapeleka kwa makuhani!”
22Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa. 23Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi walikusanyika na kufanya mpango wa kumuua Saulo. 24Lakini Saulo alipata habari ya mpango huo. Usiku na mchana walilinda milango ya kuingia mjini ili wapate kumuua. 25Lakini wakati wa usiku wanafunzi wake walimchukua, wakamteremsha chini ndani ya kapu kubwa kwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani.



Saulo anarudi Yerusalemu
26Saulo alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na wale wanafunzi. Lakini wote walimwogopa hawakuweza kuamini kwamba yeye amekuwa mfuasi. 27Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko. 28Basi, Saulo alikaa pamoja nao, akatembelea Yerusalemu yote akihubiri neno la Bwana bila hofu. 29Pia aliongea na kubishana na Wayahudi wanaoongea Kigiriki, lakini wao walijaribu kumwua. 30Wale ndugu walipogundua jambo hilo, walimchukua Saulo, wakampeleka Kaisarea, wakamwacha aende zake Tarso.
31Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.


Ainea anaponywa
32Petro alipokuwa anasafirisafiri kila mahali alifika pia kwa watu wa Mungu waliokuwa wanaishi Luda. 33Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Ainea ambaye kwa muda wa miaka minane alikuwa amelala kitandani kwa sababu alikuwa amepooza. 34Basi, Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya. Amka utandike kitanda chako.” Ainea akaamka mara. 35Wakazi wote wa Luda na Saroni walimwona Ainea, na wote wakamgeukia Bwana.




Dorka anaponywa
36Kulikuwa na mfuasi mmoja mwanamke mjini Yopa aitwaye Tabitha (kwa Kigiriki ni Dorka, maana yake, Paa). Huyo mwanamke alikuwa akitenda mema na kuwasaidia maskini daima. 37Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakaulaza katika chumba ghorofani. 38Yopa si mbali sana na Luda; kwa hiyo wafuasi waliposikia kwamba Petro alikuwa Luda, wakawatuma watu wawili kwake na ujumbe: “Njoo kwetu haraka iwezekanavyo.” 39Basi, Petro akaenda pamoja nao. Alipofika alipelekwa ghorofani katika kile chumba. Huko wajane wengi walimzunguka Petro wakilia na kumwonesha makoti na nguo ambazo Dorka alikuwa akitengeneza wakati alipokuwa hai. 40Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi. 41Petro akamsaidia kusimama, halafu akawaita wale watu wa Mungu na wale wajane, akamkabidhi kwao akiwa mzima. 42Habari za tukio hili zilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi wakamwamini Bwana. 43Petro alikaa siku kadhaa huko Yopa, akiishi kwa mtu mmoja mtengenezaji wa ngozi aitwaye Simoni.
Bible Society of Tanzania

"Swahili na Waswahili Mbarikiwe Wote"

Maonyesho ya ndege za kivita Washington DMV Sept 19, 2015‏


Picha kwa hisani ya Vijimambo na Kwanza Production



Maonyesho hayo yasiyo na kiingilio, yaliambatana na maadhimisho ya miaka 100 ya jeshi la maji nchini hapa.
Maonyesho ya ndege za kivita na vifaa vingine kutoka majeshi ya Marekani, yamefanyika leo na kuhudhuriwa na maelfu ya watazamaji.

 Askari miavuli wakishuka kwa aina yake

 Mmoja wa askari wa mwavuli akishuka katika ufunguzi wa maonyesho hayo

 F-22 Raptor

Watoto wenye asili ya Tanzania wanyakua vikombe katika SETLC FALL JR. OPEN 2015 Washington, DC‏


Vijana wenye asili ya Kitanzania Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wameonyesha umahiri wa mchezo wa Tennis uliofanyika leo Jumamosi, September 19,2015 katika viwanja vya nyumbani kwao South East Tennis and Learning Center, South East Washington, DC.

Briana Kagemuro alikuwa katika kinyanganyiro cha Wasichana wenye umri wa miaka 12 Singles (Girls 12 singles) ambapo alimshida Isabella De Leo 6-4,6-4; Cassi Chen 7-6,6-3,10-6 na Asha verma 6-4,6-4.



Naye Bryan Mwombeki alipata kombe lake la ushindi la wavulana wenye umri wa miaka 10 (USTA) (Boy's 10 Singles) dhidi ya Jason De Silva 4-0,4-0, Arbert Vardimisky 4-3,4-1; Aarush Rajanala 4-1,4-2.


Bryan Mwombeki




Briana Kagemuro



Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao wa mchezo huo mapema leo siku ya Jumamosi Septemba 19, 2015 baada ya kushinda makombe yao.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.‏


 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
 Mhe. Wilson Masilingi   Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho  Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.  Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi. Mke wa Balozi.
 Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.

Wednesday 16 September 2015

Jikoni Leo;Vilosa ( sweet rice dumplings)


Mahitaji, vipimo kwa vilosa 20

Unga wa ngano mweupe 1/2 Kikombe
Unga wa mchele 1/2 kikombe
Mayai 2
Tui la nza kikombe kasoro ( 3/4)
Hamira kijiko cha chai 1 na 1/2
Hiliki ya unga kijiko 1/4
Zafarani kidogo

Mafuta au samli ya kukaangia


shukrani;Aroma of Zanzibar


"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima

[AUDIO]: Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 14 2015


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dr Magufuli
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla
Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dr Patrick Nhigula na Arthur