Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 2 April 2013

COVENTRY WOMEN GALA-[sehemu ya 2]!!!!!!!!!!!



Mgeni wetu Da'Mariam Kilumanga..Ni Mwenyekiti wa Wanawake waTanzania UK....Akihamasisha Wanawake..
Zaidi Kujiendeleza  Zaidi Kimasomo na si kubeba BOX tuu.,Kujifunza,Kuiga yaliyo mema  ,Kushikamana ,Kujitolea,Kupendana.
 Kutumia Mitandao Vizuri na si Kutukanana kwenye Ma-Blogu[Mitandao ya Kijamii].
 Na Mengine Meengiii...

Asante sana Da'Mariam kwa Yote na Tumejifunza Mengi Sana.
         


     Da'Fay Pia alisisitiza Wanawake Tuungane,Tuinuane,Tusaidianae Pia Tupende vya Kwetu..Tujitoe ilitujifunze zaidi,,Tuache Ubinafsi ,Elimu ndiyo Mkombozi wetu..Tusonge mbele na Tuamke.....na Mengine Meeengi Sana.........


Mwanamke wa Shoka hapa katulia anasikiliza kwanza.....

Akapewa Nafasi....




Msanii kaachiwa Jukwaaa...........

Da'Mija alionngelea kwa nini Wanawake wanakuwa na Migogoro,Malezi,Familia,Kazi za Mikono,Kutokata Tamaa na Mengine Mengiiiiiiii.....

Da'Stellah katika Poziii.....


Aliongelea Kwa nini  waliamua kufanya hii Shughuli ya Coventry Women Gala, Matarajio,Mafanikio,Mapito/Changamoto na Mengine meeeengiii....

Kwa niaba ya wenzie..da'Halima na da'Agness..waliwashukuru sana Wageni wao wengine walitoka Mbali ili kufanikisha Jambo Hili..

Akiendelea..hii ni mwanzo tuu na tutasonga mbele..hatutaishia hapa..Kuna mengi yanakuja  yenye kupendeza na Kunufaisha........

Yaani watu waliongea Mambo Mengi yenye Maana na Kujifunza..Kubadilishana ujuzi,Kuelimishana,Kutambulisha Kazi zao,Kujuana,Kula,Kunywa na Kucheza.........nikisema nielezee hapa hapatoshi!!!!!!!!!!!

Da'Iren Mswahili ya KENYA........

Yeye alisisitiza si BOX tuu hapa...Wanawake Amkeni na mji -Ajiri  inawezekana..
yeye ameji Ajiri sasa na mambo yake iko Pouwa....








Wanawake wametulia wakisikiliza kwa makini........

Mwanamke Urembo...


Da'Zanel na  Da'Asina.. Waliongelea mambo ya Urembo...Wanasema hata ukitingwa vipi lakini Kujipenda ni Muhimu.Vipodozi kwa Mwanamke visikosekane...

mambo ya
Mary Kay..Pia kama unataka kufanya Biashara hiyo Inawezekana.....na Mengine mengi yanayohusu Usafi na Kutunza Ngozi yako!!!!!!!!

Wasichana walioonyesha Mitindo ya Mwanamke wa Shoka....
Kanga hiyo... imevaliwa na mtoto wa Kiswahili...

Mishono ndiyo hiyo....... na watoto wa kwetu...

Summer..ipo njiani.............

Wacha weeee.....Motooo...DJ Nae alituwekea Moshii..hahahhaha!!!!!!!

Ahhhh dadake..Mwanamke wa Shoka,Da'MIJA Na Watoto wa Kiswahili...Mmewezaaaaaa...

Mbunifu Da'Mija na Watoto/wadada wa Kiswahili..Pamoja Wakipoziii .......Baada ya kumaliza Maonyesho Yao.....

Hakika mmeweza..MUNGU azidi kubariki kazi za Mikono Yako.......
Picha Zaidi ingia;
http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/
Pia kwa Mawasiliano zaidi na Da'Mija au kujua Zaidi Mtembelee;http://damija.blogspot.co.uk/
Da'Stellah,Da'Halima,Da'Agness..Wakimpongeza Mwanamke wa Shoka na Walioonyesha mitindo!!!!!!



Da'Mariam Kilumanga alifurahishwa sana sana na Kazi za Da'Mija pamoja na wasichana....kama unavyoona hapo Wakiongea zaidiiiiiii....








Kwa Furaha kabisa na bila ya kujizuia,baadhi ya watu walitoka mbele kupiga picha na kuongea nao ........
MC Wa siku hiyo alikuwa da'Rachel-siwa na ndiyo Aliyepamba  Ukumbi.... Kwa mahitaji ya vifaa vya Mapambo,vya kuhifadhia Vyakula,Burudani na Mengine yoote yanayo husu Shughuli..vyote Vinapatikana..Kutoka;Swahili NA Swahili na Mitimndo Africa...

Kaka Paul  ndiyo Alikuwa DJ wa Siku Yetu  Amefanya kazi nzuri sana Tumuunge mkono...Kijana/Mtoto wa Nyumbani..namba yake..07521 32 15 43 ...

Kaka Paul na Da'Rachel..Picha ya pamoja kwakumaliza vyema kazi ya BURUDANI!!!!!!!!!!!






Kwenye Shughuli kula lazima na Tulishiba.........
Waanzilishi wa COVENTRY WOMEN GALA.. HALIMA,STELLAH,AGNESS!!!!!!


  Wakakutana na Vichwa hivi...da'Mija,da'Rachel.[MI-RA]..hahaahaa..Moootoooo......

 Kama ulikosa hii usikonde zitakuja nyingine zaidi..wewe tuu....

Kaa Tayari kwa Mambo ya Watoto;
 MTOTO WA AFRIKA INAPIKWA!!!!!!

Kama utapenda kutudhamini,Ushauri/Maoni na Mengine ya Kuelimisha kwa Upendo..KARIBUNI SANA.

         Nikiripoti Kutoka COVENTRY WOMEN GALA....
         Ni mimi;RACHEL wa "SWAHILI NA WASWAHILI" 
                                                  PAMOJA SANA.

Mbegu Za Furaha Na Kaka Said Kamotta!!!!!!!



Kila mtu anapenda kuwa na furaha muda wote, Ila kwa bahati mbaya sio wote tunafuraha kwasababu mbalimbali za kimaisha. Wengine wana matatizo ya kiafya, wengine wana matatizo ya kiuchumi na wengine wana matatizo ya kimahusiano na watu muhimu kwao, yote haya ni matatizo tunayokabiliana nayo katika maisha. Licha ya kuwa kila mtu na matatizo yake bado kuna maana na umuhimu wa wewe kuwa na faraja ya kuwa hali za maisha yetu hubadilika kila siku. Hakuna hali isiyobadilika iwe nzuri au mbaya ila tuna matumaini ya kuwa siku zote tuwe wenye furaha na mafanikio katika pilikapilika za maisha yetu. Kwa mantiki hiyo kuna mambo ambayo ukizingatia yatakuza na kuimarisha furaha yako.

Je ni mambo gani hayo?
 

Inaendele..Zaidi ingia;http://kamotta.blogspot.co.uk/


       "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.