Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 25 December 2011

Jikoni Leo na Xmas,Wazee wa kazi hawataki ulalamishi!!!!!!!

                                Kaka Asulwisye hapa anageuza!!
                        Hapa zamu ya kaka Hamza kugeuza.


Haya wapendwa mambo ya Xmas hayo,kaka zangu leo wameniambia,unafikiri wewe kutokuwepo watu hatuli?Wameingia wenyewe!!!!hii ndiyo hali halisi ya kwetu kwenye swala la kupika hakuna JINSIA.
Nami nawaunga mkono naona kitu si chakawaida hicho,mimi mwenyewe hapa mate yananitoka!!!


Mpendwa nawe Xmas yako imekwenda/inakwendaje? maana masaa yanatofautiana.
Wengine wameshakula na Wengine wanaandaa.


Tushirikishe basi!!!!Karibuni sana wapendwa.





Nawatakia Kheri, Baraka na Xmas Njema!!!!!!!!

Wednesday 21 December 2011

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akihojiwa na TBC1 juu ya Mafuriko jijini ...

SHINDANO: MCH. MWASAPILE (BABU WA LOLIONDO) NA GODBLES LEMA MBUNGE WA ARUSHA MJINI NANI ZAIDI MWAKA 2011?


 Godbles Lema Mbunge wa Arusha Mjini.
Mch. Mwasapile (Babu wa Loliondo)

Kutokana na maombi ya wengi kutaka kuwashindanisha watu ambao wamefanya mambo ambayo yameigusa jamii ya kitanzania kwa mwaka wa 2011 Blog yenu kwa mtazamo wa haraka kwa mwaka huu imeona iwashindanishe Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbles Lema na Mch. Mwasapile (Babu wa Loliondo).

Blog yenu baada ya kuwaingiza hao kwenye kinyang'anyiro hicho inapenda kuwaelezea kila mmoja kwa kifupi ni kwa nini ameingia. 
Tukianzia na Mh. Lema ni Mbunge kijana ambaye amekutana na mikiki mingi ya kisiasa ukizingatia yeye ni mara yake ya kwanza kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameweza kupambana na majaribu mbali mbali ya kisiasa mpaka kumpelekea kugoma kupata dhamana ya kesi mojawapo katika kesi zinazomkabili na kuamua kwenda rumande ili ujumbe wake ufike, na vile vile kutokana na kura ambazo zilikuwa zinapigwa kutoka Blog ya Mjengwa akishindanishwa na wanasiasa mbali mbali ambao wengi wao ni vijana wenzie nakuweza kushinda katika kinyang'anyiro hicho.

Tukirudi kwa Mch. Mwasapile almaarufu kama Babu wa Loliondo au Babu Ambi, yeye ameingia kwenye kinyang'anyiro hiki kutokana na yeye kuwateka watanzania watoto, vijana na wazee katika nafasi zao mbali mbali kwa staili yake ya kugawa tiba ya asili kwa kutumia kikombe maarufu kama kikombe cha babu.
Mchungaji huyu alianza kutoa huduma hii mwanzoni mwa mwaka huu na kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na watu wengi kuamini dawa anayotoa kwa kutumia kikombe hicho inatibu magonjwa yote sugu yakiwemo Ukimwi, kisukari, TB na mengine mengi, kutokana na tukio hili kuwahusisha watu mbali mbali, ata wale wenye nyadhifa za juu tumeona Babu huyu anafaa kuingia kwenye mtanange huu.

TAFADHALI PIGA KURA YAKO KWA KUTUMIA UJUMBE WA MAANDISHI KWENDA NAMBA +255 714945143

UKIWA KWENYE ENEO LA KUANDIKA UJUMBE KWENYE SIMU YAKO UTAANDIKA:
"2011 WINNER BABU" AU
"2011 WINNER LEMA"
TUMA KWENYE NAMBA HIYO HAPO JUU, MWISHO SAA 5.59 USIKU WA TAR. 31/12/2011.

MAJIBU YATATOLEWA TAR. 1/01/2012

Nimetuwa na KapingaZ Blog
Ahsante sana.