Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 21 June 2011

Wanaume na Mitindo,Leo wenye Rasta Eti!!!!!!!

                                           Simon wa Kitutruru [kitururu Mawazoni ,Blog]
                                         Bob Sankofa [Fotobaraza blog]
                                     Arba wa Manillah [Kukaye moto Blog/Mziki]
                                   Mrisho Mpoto [Muziki,blog]


Wapendwa Kufuga nywele ni kupenda si kama vinyozi hakuna!!!Kumekuwa na mtazamo wa baadhi ya watu kuhusu Rasta.Watu waonaopenda kuwa na Mtindo huo kuonenakana kama Wahuni,Wavuta bangi,hawatakiwi kula Nyama na Si heshima kwa jamii. Labda nisimalize yote nawe kama unayo  unayoyajua mengi.


Je Unasemaje kuhusu haya?
Karibuni sana kwa kuelimishana na Kutoa mawazo, maoni,Ushauri wako!!!!.

Sunday 19 June 2011

Leo ni Siku ya wa BABA!!!!!!!!

                                  Sandra & Tracey na Baba yao.[Faraja Yangu ].
                                        Joel & Jolen na Baba yao.
                                         Arianna na BABA!!.
.
                                     Baba Paulina.
                                        Sabrina na BABA.
                                      Jawahiri na BABA.
                                       Anna-Harrieth na BABA.
Nawatakia Kheri wa BABAWote popote mlipo, Mungu awabariki sana.
Tuwe bega kwa bega katika malezi ya watoto,Kama si Baba tusingeitwa mama.
Pia Shukrani kwa baba yangu Mpendwa [R.I.P]


Kama una Picha au salamu kwa BABA  yeyote Rukhsaaaaaa!!!! Tuma kupitia Rasca@hotmail.co.uk


Wapendwa kina BABA wa leo/kisasa  na Wazamani,  Kundi lipi linaongoza Kutelekeza Watoto/Familia?
Na Sababu ni nini, Nyumba ndogo, Ulevi,Ujana,Umimi au...........

Tuesday 14 June 2011

Penye Wengi Pana Mengi!!!!!!

 Hapa kina Mama/Wanawake wapo Jikoni na Mazungumzo yao.
Hapa kina Baba/Wanaume wapo Nje na Mazungumzo yao.

Wapendwa, Wanapokutana watu wawili au watatu hapakosi neno/maneno ya kuongea.
Na katika pitapita zangu  Mswahili mimi, Kwenye  Mikusanyiko ya Wa Afrika/Waswahili wengi kama si wote,Utakuta Wanawake/Kinamama wanakaa pekeyao na Kina baba Wanakaa pekeyao,Hata kama hawakuambiwa Kina MAMA sehemu yenu hii na Kina BABA manaombwa kukaa hapa.

Wenyewe  tu mmoja baada ya mwingine utaona wanajitenga.
Jee wewe mpenzi msomaji Unamawazo gani katika hili? Ni Utii,Heshima,Kujinafasi,Malezi tuliyo lelewa Au....
Na unafikiri wakina Mama wakiwa huko zaidi wanaongelea nini?
Na kina Baba jee?.

Karibuni sana Wapendwa Tuzungumze Pamoja!!!!

Saturday 11 June 2011

Siku kama ya Leo Mash-P Alizaliwa!!!!!!!

Hongera  kaka Mash-p kwa kuongeza mwaka mwingine! Tunakutakia kila la kheri na baraka katika Yote.
Mungu akuongezee Miaka mingine Mingi.

Wednesday 8 June 2011

Wanawake na Urembo!!!!!!!!







Haya wapendwa Urembo wakati mwingine unataka Moyo! Kama unavyoona kwenye picha.
Wewe mwanamke/dada unapenda kujiremba na unapendelea nini kuongezea Urembo wako?

Wewe baba/kaka unapenda wanawake/kina dada wanaojiremba na unapenda nini waongezee katika Urembo wao?.

Na jee kwenye Picha hizo nini kimekuvutia na nini Kimekuchukiza?.
Kwa wanaopenda kujiremba, Wanajiremba ili iweje? Ni kujiweka nadhifu,kumfurahisha mpenzi,kujipenda au.......
Na wasiopenda kujiremba, Nini sababu, Nikujiamni, kutojipenda,wapenzi wao hawapendi,kuona Aibu au.....

Karibuni sana Waungwana kwa kuelimishana.

Sunday 5 June 2011

Mtoto Wetu Leo ni Frank- Jayden!!!!!!!!!!!!!!!!

 Hapa anawaza leo nianze na  Mchezo upi au nikacheze wapi Sijui?
 Nimekuja kunywa maji tuu,Wao wameshanibana nisiende tena kucheza je hii ni haki jamani?
 Nimeshindwa kutoka tena,ahhh ngoja nioge zangu tuu!!!!!
 Sasa watajuta kunifungia ndani ,mimi naungana na huyu ni kelele tuu mpaka kieleweke!!!!!!
 Wakaona wanitoe kidogo hata kwa Mangi nipate walau Soda!!!!!!!
 Hapa sasa mambo poa watu wangu, Asanteni kwa Ofa baba na mama!!!!!!!!
Ngoja nikatafute Elimu , Eti yule babu wanaemuita sijui NYERERE [R.I.P] Nimeambiwa alisema Elimu ni Uti wa Mgongo,Sasa sijui kama nikweli au maneno tuu.

Waungwana kila Mtoto anavituko vyake,Hata wewe kwenye Utoto wako ulipitia mambo mengi  sana mpaka kufikia hapo ulipo.Katika hayo ya Mtoto wetu Frank-Jayden, Umeguswa/kumbushwa na  nini katika Maisha ya Utoto?. Karibuni sana kwa Ushauri na kuelimishana katika malezi ya Watoto wetu!!!!!!!

Wednesday 1 June 2011

Mapenzi/Mahusiano ya Jinsia Moja!!!!!!

Kumekuwa na Ongezeko  la Mahusiano ya kimapenzi  ya Jinsia Moja, Mpaka kutaka /kufunga Ndoa za jinsia Moja.Kuna baadhi ya Nchi wanapinga mpaka kutaka kuwadhuru au kuwaua kabisa.Na kunawanaoandamana kwa kupinga Mauaji hayo, Nakutaka wapewe haki zao za Kuoana au Kuendeleza Mapenzi/Mahusiano yao ya Jinsia Moja.

 Je wewe Mpenzi msomaji unamawazo/mchango gani katika hili? Karibuni sana Waungwana!!!!!!!