Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label jikoni leo. Show all posts
Showing posts with label jikoni leo. Show all posts

Wednesday 12 May 2021

Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali 9;Nyama

 



Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali 9;Nyamna ;yakuokwa/choma/kukaanga/kuchemsha.. ;Nimeunga kutumia; Nyanya,situmii za kopo,na huwa simpenzi sana wa kuzisaga labda niwe na haraka sana,Namenya (kizamani🀣) ;kitunguu maji-cheupe, ;Kitunguu swaum sijui thoum πŸ™ŒπŸ½ Tangawizi,hivi nanunua nakusaga nyumbani πŸ€“ ;karoti ;hoho za rangi zote ;chumvi/maggi Ndimu/Limau ;Roiko/Simba mbili-siyo lazimaa ;pilipili mbuzi natupia karibu na mwisho ;Kupika/ Kuunga; Nyama nyekundu /unaweza tumia yoyote.. ;NyamaNimeosha ;Nikachemsha kwa chumvi/maggi,ndimu/limau ;Kitunguu swaumu/thoum ;Tangawizi ;Pilipili mtama/manga[blacpepper]...kwanza Baada ya Maji ya kuoshea kukauka nikaongeza maji kidogo (inategemea na ugumu wa nyama) Yalivyokauka nikaendelea kukaanga na Mafuta yake mpaka ikawa kavu.. nikakarangiza viungo kwa mafuta kidogo.. ;Nikaweka Nyama nikakaanga na viungo.. ;Nyanya nikaweka mwisho.. ;Kabla sijaokoa nikaweka tomato souse(ketchup)kidogooo ;Unaweza kuweka chill souse(ile ya Tanzania nikiwanayo huwa naweka hiyo) ;Unaweza kuweka tomato pure.. ;Kabla sijaokoa nikatupia pilipili.. ;Unaweza weka kabichi(Cabbege) Mkono mmoja isiive sana πŸ˜‹.. Hayaaaah kazi kwenu mnaweza kuongezea ujuzi nilipokosea ;siyo mpenzi wa viungooo vingii kama unapenda wewe Rukhsa πŸ™πŸ½ Jikoni leo;Mboga 10 za kula na Ugali πŸ˜‹ : :Ugali una mboga zake jee wewe Unapenda mboga zipi kula na Ugali? :Mimi nitaweka hapa ninazo Zipenda na zinazo patikana hapa tulipo 😊 : πŸ™πŸ½πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kitchen today #mboga10 Jikoni Leo πŸ‘©πŸΎ‍🍳

Wednesday 7 April 2021

Jikoni Leo;Mboga 10 Za Kula na Ugali-4;Kuku wa chukuchuku...

 

 





Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali ;4Kuku ;Chukuchuku ;Nimeunga kutumia; Nyanya,situmii za kopo,na huwa simpenzi sana wa kuzisaga labda niwe na haraka sana,Namenya (kizamani🀣) ;kitunguu maji-cheupe, ;Kitunguu swaum sijui thoum πŸ™ŒπŸ½ Tangawizi,hivi nanunua nakusaga nyumbani πŸ€“ ;karoti ;hoho za rangi zote ;chumvi/maggi Ndimu/Limau ;Roiko/Simba mbili-siyo lazimaa ;pilipili mbuzi natupia karibu na mwisho ;Kuku Wagumu Kuunga; Unaweza kuweka Nazi/Mafuta Mimi nimechemsha tuu(chukuchuku) ;Nimeosha ;Nikachemsha kwa chumvi/maggi,ndimu/limau ;Kitunguu swaumu/thoum ;Tangawizi ;Pilipili mtama/manga[blacpepper]...kwanza Baadae nikaweka maji kidogo karibu na kuiva,maji yamebaki kiasi nikaweka viungo vyote,vikaiva pamoja na mchuzi ukabaki kiasi.... Hayaaaah kazi kwenu mnaweza kuongezea ujuzi nilipokosea ;siyo mpenzi wa viungooo vingii kama unapenda wewe Rukhsa πŸ™πŸ½ Jikoni leo;Mboga 10 za kula na Ugali πŸ˜‹ : :Ugali una mboga zake jee wewe Unapenda mboga zipi kula na Ugali? :Mimi nitaweka hapa ninazo Zipenda na zinazo patikana hapa tulipo 😊 : πŸ™πŸ½πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kitchen today #mboga10 Jikoni Leo πŸ‘©πŸΎ‍🍳 :#chakula#kupikaπŸ‘©πŸΎ‍🍳πŸ₯˜ #kitchentoday #inmykitchentoday #jikonileo #mboga #Ugali #mapishi #mpishi #veggies #chicken #kuku #cooking#food#foodie#foodblogger#tanzanianfood#tanzaniaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ #eastafrica#bbcfood#cnnfoodπŸ˜‹ #Coventry#UK#lifestyleblogger#vlogger#mswahiliπŸ‡ΉπŸ‡Ώ#Rachelsiwa

 

Monday 29 March 2021

Jikoni Leo;Mboga 10 Za Kula na Ugali-3;Bamia/Mlenda




 Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali 

3;Bamia/Mlenda 


;chukuchuku

;Bamia,Nyanyachungu...

;Chumvi

;Magadi/unga wa soda kama umekosa magadi..,

;Wakati mwingine huwa naweka majani ya maboga...


;Magadi Nimepewa na @eliadetor πŸ™πŸ½ kutoka ;Tanzania (Nyumbani)

 Akileta ya kuuza nitawaambia 


Kuunga; 

Unaweza kuweka Nazi/Karanga (sijawahi kula hii nasikia)

Mimi nilichemsha tuu (chukuchuku)


:;Nimeziosha na maji 

;Nimezikata ndogondogo 

;Nikamchemsha kwa maji, 

;chumvi,magadi, na Nyanyachungu

Karibu na kuiva maji yamebaki kiasi nikaweka pilipili 


Hayaaaah kazi kwenu mnaweza kuongezea ujuzi nilipokosea 

;siyo mpenzi wa viungooo vingii kama unapenda wewe Rukhsa πŸ™πŸ½


Jikoni leo;Mboga 10 za kula na Ugali πŸ˜‹

:

:Ugali una mboga zake jee wewe 

 Unapenda mboga zipi kula na Ugali?


:Mimi nitaweka hapa ninazo Zipenda na zinazo patikana hapa tulipo 😊


: πŸ™πŸ½πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kitchen today


#mboga10 

Jikoni Leo πŸ‘©πŸΎ‍🍳 


:#chakula#kupikaπŸ‘©πŸΎ‍🍳πŸ₯˜ 

:


:


#kitchentoday

#inmykitchentoday 

#jikonileo 

#mboga

#Ugali

#mapishi 

#mpishi 

#veggies 

#Bamia

#Mlenda

#hombo 

#cooking#food#foodie#foodblogger#tanzanianfood#tanzaniaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ #eastafrica#bbcfood#cnnfoodπŸ˜‹ 


#Coventry#UK#lifestyleblogger#vlogger#mswahiliπŸ‡ΉπŸ‡Ώ#Rachelsiwa 

Wednesday 24 March 2021

Jikoni Le;Mboga 10 Za Kula na Ugali-2;Samaki Mkavu/wakavu..


 Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali 

2;Samaki Mkavu/wakavu 


;chukuchuku/Nazi


;Nimeunga kutumia;

Nyanya,situmii za kopo,na huwa simpenzi sana wa kuzisaga labda niwe na haraka sana,Namenya (kizamani🀣)

;kitunguu maji-cheupe,


;Kitunguu swaum sijui thoum πŸ™ŒπŸ½

Tangawizi,hivi nanunua nakusaga nyumbani πŸ€“(siyo lazima)

 

;karoti

;hoho za rangi zote

;chumvi/maggi

Ndimu/Limau

;Roiko/Simba mbili-siyo lazimaa 

;pilipili mbuzi natupia karibu na mwisho 

;Unaweza kuongezea; bamia,Nyanyachungu...


;Samaki Nililetewa zawadi πŸ™πŸ½ kutoka ;Tanzania (Nyumbani)

 Akileta wa kuuza nitawaambia 


Kuunga; 

Unaweza kuweka Nazi 

Mimi nilichemsha tuu (chukuchuku)


:;Nimemuosha na maji ya moto

;Nikamchemsha kwa maji, chumvi/maggi,Ndimu/Limao..

Karibu na kuiva maji yamebaki kiasi nikaweka viungo vyote pamoja 

Vikaiva pamoja na@mchuzi ukabaki kiasi....


Hayaaaah kazi kwenu mnaweza kuongezea ujuzi nilipokosea 

;siyo mpenzi wa viungooo vingii kama unapenda wewe Rukhsa πŸ™πŸ½


Jikoni leo;Mboga 10 za kula na Ugali πŸ˜‹

:

:Ugali una mboga zake jee wewe 

 Unapenda mboga zipi kula na Ugali?


:Mimi nitaweka hapa ninazo Zipenda na zinazo patikana hapa tulipo 😊


: πŸ™πŸ½πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kitchen today


#mboga10 

Jikoni Leo πŸ‘©πŸΎ‍🍳 


:#chakula#kupikaπŸ‘©πŸΎ‍🍳πŸ₯˜ 

:


:


#kitchentoday

#inmykitchentoday 

#jikonileo 

#mboga

#Ugali

#mapishi 

#mpishi 

#veggies

#fish

#samaki

#samakiwakavu 

#dryfish 

#cooking#food#foodie#foodblogger#tanzanianfood#tanzaniaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ #eastafrica#bbcfood#cnnfoodπŸ˜‹ 


#Coventry#UK#lifestyleblogger#vlogger#mswahiliπŸ‡ΉπŸ‡Ώ#Rachelsiwa

Wednesday 17 March 2021

Jikoni Le;Mboga 10 Za Kula na Ugali-1;Samaki..





 Jikoni Leo;Mboga za Kula na Ugali 

1;Samaki

;Wakuokwa/kukaanga 

;Nimeunga kutumia;

Nyanya,situmii za kopo,na huwa simpenzi sana wa kuzisaga labda niwe na haraka sana,Namenya (kizamani🀣)

;kitunguu maji-cheupe,


;Kitunguu swaum sijui thoum πŸ™ŒπŸ½

Tangawizi,hivi nanunua nakusaga nyumbani πŸ€“

 ;mafuta kidogo nimetumia Olive Oil 

;karoti

;hoho za rangi zote

;chumvi/maggi

Ndimu/Limau

;Roiko/Simba mbili-siyo lazimaa 

;pilipili mbuzi natupia karibu na mwisho 


#Samaki Kama upo πŸ‡¬πŸ‡§ unaweza kuagiza kwa @eliadetor wa kuokoa/kukaanga wangu nimenunua huko 


Kuunga nimeunga mwenyewe


Hayaaaah kazi kwenu mnaweza kuongezea ujuzi nilipokosea 

#siyo mpenzi wa viungooo vingii kama unapenda wewe Rukhsa πŸ™πŸ½


Jikoni leo;Mboga 10 za kula na Ugali πŸ˜‹

:

:Ugali una mboga zake jee wewe 

 Unapenda mboga zipi kula na Ugali?


:Mimi nitaweka hapa ninazo Zipenda na zinazo patikana hapa tulipo 😊


: πŸ™πŸ½πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Kitchen today


#mboga10 

Jikoni Leo πŸ‘©πŸΎ‍🍳 


:#chakula#kupikaπŸ‘©πŸΎ‍🍳πŸ₯˜ 

:


:


#kitchentoday

#inmykitchentoday 

#jikonileo 

#mboga

#Ugali

#mapishi 

#mpishi 

#veggies

#samaki

#fish

#cooking#food#foodie#foodblogger#tanzanianfood#tanzaniaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ #eastafrica#bbcfood#cnnfoodπŸ˜‹ 


#Coventry#UK#lifestyleblogger#vlogger#mswahiliπŸ‡ΉπŸ‡Ώ#Rachelsiwa 

Instagram;Rachelsiwa,Swahli Na Waswahili.

Tuesday 21 April 2020

Jikoni Leo Na Mswahili Da'Sophia Kajembe-Simple meatbballs





zaidi ingia;Sophia Kajembe



 
 
 kwa mapishi na mengineyo kama utapenda ku share nasi..
usisite kututumia kupia Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima..

Friday 17 April 2020

Jikoni Leo Na Mswahili Da'Sophia Kajembe- Simpel Rice...






zaidi ingia;Sophia Kajembe



kwa mapishi na mengineyo kama utapenda ku share nasi..
usisite kututumia kupia Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima..

Saturday 7 April 2018

Jikoni Leo;Uji wa Mchele

Habari za asubuhi wapendwa/waungwana..?
Jumamosi inaendaje hapo ulipo?
Umepanga nini/utafanya nini?Ni cha tofauti au ni utaratibu wako wa kawaida?
Hapa kwetu ni likizo shule zimefungwa,natumaini wazazi/walezi wengi nao wapo likizo
najua wengi wanapenda kuwa likizo nao kipindi hiki ili kwenda sawa na familia..
Basi kama upoupo na una nafasi  usiitumie vibaya hiyo nafasi kwani hairudi tena siku ikienda imekwenda..!

Ok nisiwachoshe kwa maneno ni "Jikoni Leo"Uji wa Mchele...
Unaupenda uji huu?umeshawahi kuuonja?
jee wewe unaupikaje?
Karibu tupeane ujuzi....





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 23 March 2018

Jikoni Leo;Pweza.. eti Pweza ni dawa?

Hamjambo wapendwa/waungwana?
ni "Jiko leo" tunakula Pweza....
Unawajuwa Pweza?
unawapenda jee unawapikaje?unakula na nini?
Mimi nawapenda sana tena kule nyumbani huwa nakula
wale wa mtaani...
sijawahi kula kwa mapishi mengine zaidi ya kukaanga..
Nasiki Pweza ni dawa eti kwa Wanaume jee ni kweli?
Karibu uonje kama hujawahi kula na kama wawajua endelea
kupata utamu...!!



"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday 21 November 2017

Jikoni Leo;Kunde na Rachel-siwa..







Wapendwa/waungwana natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila
siku,Pamoja na hayo siku haipiti na wala mambo hayatoenda sawa kama ukiwa na njaa..
ni "Jikoni Leo"mimi leo nimeandaa/pika KUNDE je wewe leo unapika/umepika nini?
Kunde hizi nimepewa zawadi kutoka Nyumbani Tanzania [Bongo]
Nimezichagua na nikaziacha/loweka kwenye maji usiku mzima,Asubuhi nikaziweka/bandika/tereka..... ok
jikoni kwa kuzichemsha mpaka zilivyoiva,nikakatia/weka Kitunguu maji na chumvu zikachemka kidogo
nikaongezea/unga nazi tuu sikuweka viuongo vingi...

Mimi hupenda kula na maandazi[zege kibongobongo/kiswazi] pia wali/ubwabwa...!
jee wewe unapenda kunde na je unapikaje? na unapenda kula na nini?
Karibuni sana...









"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday 25 October 2017

Jikoni Leo;Boga/Maboga[Pumpkin]



Ni matumaini yangu hamjambo na manaendelea vyema na majukumu yenu..
Wapendwa/Waungwana "Jikono Leo" ni Boga/Maboga,nafikiri wengi mnayajua hata kama hujawahi kula..
Jee wewe ni mpenzi wa Maboga? Unapikaje?hapo ulipo yanapatikana?watoto wako wanayapenda?
Mimi ni mpenzi sana wa  Boga mama yangu alikuwa analima sana,
Nyumbani kwa mama tulikuwa tunapika -kuchemsha wakati mwingine tunachanganya na mihogo na tunaunga/tia
Nazi,lakini wakati wa kula kona zilikuwa nyingi wengi tulikuwa tunaacha mihogo na tunakula maboga hasa ile rojo yake
maana huwa yanarainika sana kwenye mchanganyo[Futari]..
Hapa nilipo yapo lakini ni ghali kidogo..
watu wengi  niliowauliza kama wanayapenda/wanakula?
wengi hawali,wengine wanasema huwa wanatengeneza supu,wengine hawajui kabisa kama haya yanaliwa..
Wao wanajua ni kwasababu ya siku kuu ya Halloween huwa yanafanya mapambo ya hiyo kitu yao
huwa wanachonga/kutengeneza mapambo ya Halloween..
Hayyahh halloween na Maboga...
Kwanza sikuwahi kuisikia hii siku kuu nilipokuwa nyumbani
haya mambo nimekutana nayo huku ya kuvaa vitu vya kutisha
na watoto usiku wanaenda kila nyumba wanapewa pipi,chocolate
[trick or treat]maana zaidi ya halloween unaweza kuipata Google..
Tena hiki ndiyo kipindi chake inakuja hiyo siku..
Eeeh nasikia Bongo-Tanzania nako kuna hiyo siku kwa watoto
wa doti comu,wanaoenda na wakati na mitandao..[sina hakika na hili]

Tuendelee na mapishi katika picha...
lilikuwa hivi..





Nikalikata na kutoa Mbegu hizi mbegu nahifadhi nitakuja kupanda ...

lipo kwa sufuria nikatia maji na chumvi kidogo..

Nimefunika kwa foil,juu na mfuniko nikaweka jikoni..


Lipo tayari unaweza kushushia kwa maji,Chai au chchote..




   Karibuni sana..

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Thursday 12 October 2017

Jikoni Leo;Kahawa(Coffee)...

Habari zenu Waungwana..
Nimatumaini yangu wote hamjambo..
Siku nyingi kidogo nimepotea kwa mambo ya jikoni..
Ni muingiliano wa majukumu tuu..

Haya "Jikoni Leo" ni  Kahawa [Coffee]..
Jee wewe unapenda Kahawa? unaipikaje?unapenda kunywa kahawa wapi?
Kijiweni?kwenye migahawa au Nyumbani?
Hapo ulipo/unapoishi watu wanapenda kunywa Kahawa?
 kahawa inanywewa sana wapi
mkoa/mji gani Tanzania?kwa nini? hali ya hewa inaruhusu?Mazoea?Tamaduni? au....
Nilipokulia mimi Dar es salaam Kahawa ilikuwa kuwa inanywewa sana ..
zamani kidogo kulikuwa na vijiwe vya wazee/wanaume wanacheza karata/bao huku wakijinywea Kahawa
pia kulikuwa  na wauza Kahawa, Kashata wa kupitisha mitaani..
Sina uhakika kama utamaduni huu wa kukaa vijiweni
 kunywa Kahawa na kuongea mawili matatu kama bado upo
hata kama upo lakini umepungua sana..
Unafikiri ni kwa nini?Maendeleo?Sehemu za wazi zimepungua?ubinafsi,Hali ngumu au Vijiwe vipo vya kisasa zaidi(Migahawa]
mikubwa ya ndani imeua Vijiwe/vibaraza vya Kahawa?

Mimi hapa nilipo Kahawa inanyweka sana hasa kipindi hiki kinachokuja cha Baridi ndiyo zaidi...
Hata mimi napenda kunywa Kahawa Nyumbani huwa nakunywa hii kutoka Tanzania ,nikiwa Mtaani ni mpenzi wa Cupccino..

Karibu sana Tunywe Kahawa huku tukipeana story/kubadilishana hadithi za maisha,malezi na mengineyo..







"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.



Tuesday 11 April 2017

Jikoni Leo;MKATE WA AJEMI/BWANA - KISWAHILI,Mpishi da'Fathiya..




Mahitaji:
Mahitaji
Unga wa ngano vicombe 4 - 520 gms
Hamira kijiko 1 kikubwa - 17 gms
Baking soda kijiko cha chai 1 & 1/2 - 10.5 gms
Chumvi kijiko cha chai 1 & 1/2 - 9 gms 
Maziwa ya mtindi kikombe 1 
Maji nusu kikombe ( kwa kuzimua mtindi)
Mafuta vijiko 2 vikubwa 
Yai 1

Shukrani;Aroma of Zanzibar

"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 24 February 2017

Jikoni Leo; Na Da'Farhat- Chicken And Vegetable Spring Rolls In Kiswahili Na Best Homemade Whole Fried Fish In kiswahili


Haya Wapendwa/Waungwana ni siku nyingi kidogo tumekosa "Jikoni Leo"
Tuanze na Dada huyu na mapishi yake haya...

Karibuni...





Kama unayako mapishi unapenda nawengine wajifunze na kukufuatilia..usisite kututumi/kutujuulisha
Email;Rasca@hotmail.co.uk au unaweza kuni Inbox kwa mitandao ya kijamii, Natumia Rachelsiwa..


Zaidi;Farhat Yummy

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Saturday 10 December 2016

Jikoni Leo; Na da'Fathiya (Aroma of Zanzibar)UNGA WA PUFF PASTRY - KISWAHILI





Mahitaji 1

Siagi vikombe 3
Unga wa ngano kikombe 1

Mahitaji 2

Unga wa ngano vikombe 4
Chumvi vijiko 2 vidogo
Maji ya ndimu kijiko 1 kidogo
Maji ya baridi kikombe 1
Siagi 1/2 kikombe


Shukrani;
Aroma of Zanzibar

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Thursday 26 May 2016

Jikoni Leo na Bi Sheikha Agili-Achari ya Mraba





Ingredients:
2 cups sugar
1 and a half cups water
Salt
Chili powder
Red food colour 
Dried uncooked achari (slithered mangoes that have been dried in the sun)
Method:
In a pot, add everything except the achari.
Cook the mixture until it gets sticky enough and the liquid has reduced abit then add the achari and mix well while still on the stove.
You can leave the achari abit saucy(rojo) or let the liquid dry abit so they be somewhat sticky(mraba). If the syrup is done right you can even let liquid completely dry and let the achari get coated with sugar while the syrup is drying (kavu).
Once the desired stage of the achari is reached remove from the stove and let them cool.
Enjoy!!


Zaidi ingia;Sheikha Agil


"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Thursday 12 May 2016

Jikoni Leo na Tupike Pamoja; Recipe of Lemon chicken

Wapendwa waungwa natumai muwazima..
hapa kwetu tupo tupo vyema kabisa na hali ya hewa ni nzuri...kijua kimetoka..
vipi huko uliko wewe?

Ni Jikoni Leo sambamba na Tupike Pamoja wametuletea toleo jipya...

nisikuchoshe na maneno meengi Karibuni..


.....twende pamoja...


zaidiingia;Tupike Pamoja



"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima

Thursday 24 March 2016

Jikoni Leo; Mandazi ya kusokota ,Mapishi ya biscuit za karanga,na Sophie's Kitchen...

Wapendwa/Waungwana natumaini mnaendelea nyema na maandalizi ya Pasaka..
Ni Jikoni Leo na mapishi haya yatawasadia kuongezea kwenye maakuli ya Pasaka..
Mapishi haya kutoka kwa "da'Sophie"...

Basi nisiwachoshe na maneno meengi...

Twende sote sasa....






Shukrani;Sophie Kitchen...Zaidi;jitukumbuka63

"Swahili Na Waswahili"Muwe na wakati mwema.




Friday 2 October 2015