Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Waswahili na maisha Yao. Show all posts
Showing posts with label Waswahili na maisha Yao. Show all posts

Monday 29 July 2013

Waswahili Na Maisha Yao;Futari Ya Pamoja Marekani[DMV]!!!




Waungwana;"Waswahili na Maisha Yao",Waswahili wa Marekani DMV, wana utaratibu huu wa kukutana pamoja kila J'mosi na J'pili na Kuwa na Futari/Kufuturu pamoja.. Hii inaonyesha kuwa Waswahili hawa hawasahau baadhi ya mambo Mema/Mazuri ya kwao,Ukarimu,Umoja na Mengine meengi.

Hongereni Sana na Muwe na Funga Njema.

Shukrani;Vijimambo Blog.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday 18 December 2012

Waswahili Na Maisha Yao;AFRICAN VILLAGE LIFE!!!



Waungwana; Leo tuangalie Maisha ya Kijijini..........

Jee wewe umewahi ishi kijijini?
 Nini kizuri unakumbuka  na Nini kibaya unakumbuka?.....

Jee Unafikiri kwanini Wazungu hupenda kuchukua Matukio ya Vijijini? kwa sababu ni mageni kwao,Wanataka kutusaidi au?.

 MUNGU Ibariki Afrika,MUNGU Ibariki TANZANI!!!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Tuesday 4 September 2012

Waswahili na Maisha Yao;Leo Tupo IRINGA-Village Schools International-Shamba Darasa!!!!!!!!!



"Waungwana, Waswahili na Maaisha Yao". Leo tupo IRINGA.

Watu wa vijijini wengi wao bado ni wanyeyekevu  kwa Wageni,Shukrani na Kujitoa.
Hapo wakiimba kwa Sauti Taaamu. Pamoja na Mgeni wao,Wakimshuruku MTALAAMU.

Wewe unafikiri kwanini watu wa Vijijini  wengi wao bado wanaukarimu,Shukrani na Unyeyekevu?
 Hawajafunguka,Hawaendi na Wakati,Hawajaumizwa au Mazingira yanachangia?
Jee Vipi watu wa Mjini?Yaani ukiachana na mtu mwaka mmoja  tuu baadhi yao  inabidi Utulize Akili na kuchunguzana upya, kwani Wengi Tabia imebadilika.
Jee  Washalizwa sana/kutapeliwa,Ugumu wa Maisha, Waelevu au Wajanja  Au.......?

 Karibuni sana kwa Maoni/Mawazo,Ushauri na Tuelimishane kwa Amani na Upendo.
[KILIMO KWANZA AU...?]

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Friday 24 August 2012

Waswahili na Maisha Yao-TX Seleleka in Mgama Tanzania 1981,Makassy CCM,Mwendo Mdundo-CHADEMA!!!!!

Waungwana sina la kusema nimekumbuka Nyimbo hizi  za Zamani za Chama Tawala na nikaona niweke na Nyimbo ya sasa ya CHADEMA. Nimeshindwa kupata ule chama chetu cha mapinduzi lakini utausikia kidooo hapo kwenye Video hiyo ya Mgama IRINGA.Hii nimeipata:http://watafiti.com.

Waswahili wakitimbwilika/kucheza, wengine huku wananyonyesha baasii ahhh.

Unalo la kuongezea hapo Muuungwa? Karibu sana kwa 
Upendo na Amani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA. "Swahili NA Waswahili" 
Pamoja sana.

Tuesday 10 July 2012

Mswahili Wetu Leo; Da'EMMY KOSGEI,Ameanzia Wapi na Anaendeleaje,Msikileze!!!

Emmy Kosgei;Amepata Tunzo ya Nyimbo Bora ya Injili Barani Afrika 2012.Nyimbo;OLOLO.
Waungwana Mswahili Wetu Leo ni Emmy.
Yeye anatumia Lugha ya  kikuyu kwenye kuimba nyimbo zake,
Pia Mavazi yake Zaidi ni ya Ki Afrika.
 Mimi ananivutia sanaaa na da'Emmy 
 Nimetokea sana kupenda midundo,Mirindimo, Sauti na..... Lakini KIKUYU IMEPIGA CHENGA!!!

Vipi wewe Muungwana Emmy anakuvutia? Zaidi nini?

Ebu Tumsikilize kidogo yeye ni Nani na Ameanzia wapi na Anafanyaje!!!!!

Swahili NA Waswahili Pamoja Sana!!!!
Shukrani; Africanacts na k24Tv
Wimbo Alio upatia Tunzo Ololo!!!!
Emmy akiwa Uk.

Friday 25 May 2012

Waswahili wetu Leo;WaTanzania na Madawa ya Kulevya!!!!!!!

Haya Waungwana;Hawa ni Ndugu zetu,Jamaa zetu,Rafiki zetu,
Jee nani Alaumiwe? Muuzaji au Mtumiaji?
"Swahili na Waswahili" Pamoja sana.

Wednesday 21 March 2012

Waswahili na Maisha Yao - Zanzibar na Mwaka Kogwa Festiva-Burudani Marashi ya Pemba!!


Waungwana Waswahili wa Zenji wanamambo yao,Unajua kuhusu Mwaka Kogwa?Sijui ni Matambiko,Michezo,Sherehe au?Jee mpenzi msomaji Umeshawahi kukutana,Kuona,Kushiriki Mwaka Kogwa?Hivi wanavyotandikana, Kama kunamtu unasababu nae si ndiyo Utamtandika Kwa hasira?Jee Mwaka Kogwa wanaruhusu kushiriki mtu yeyote au mpaka uwe Mzaliwa wa huko?
Karibuni sana Waungwa!!

Friday 17 February 2012

Waswahili na Maisha yao - Washington DC,Marekani na Mzee Yusuf,Nyumbani kwa Missy Temeke!!!

Haya wapendwa waswahili na  Maisha yao,Makhanjumati/Vyakula kwa wingi,Burudani, watu na furaha.ilikuwa siku ya Wapendanao,Wao waliamua kupendana kihivyo,Hayo yote ni Mapenzi,Umoja,Kufurahi ,Kushirikiana na Wengine!.Ukitakata kujua zaidi ingi. http://swahilivilla.blogspot.com

Wednesday 8 February 2012

Waswahili na Maisha yao -Nyimbo za Mipasho[Rusha Roho]!!!!!!!

Waungwana vipi kuhusu nyimbo hizi za MIPASHO,[RUSHA ROHO]Zinajenga au Zinabomoa?jee nahii michezaji vipi?kwani mpaka tukukatike na kugusana?jee hizi  ni Taarabu,Chakacha au ni Mitindo gani?Wenyewe wanaema meseji Send wewe unasemaje?Duuhh SWAHILI NA WASWAHILI AU VIPI? KARIBUNI SAAANA.

Thursday 5 January 2012

Waswahili na Maisha yao-Coventry Swahili Party/Mwaka Mpya[shukrani]!!!



                             Asanteni sana  Swahili dadazzzz.
                                   dada Esther Asante.
                                      Wapendwa Mungu awabariki sana.
                                       Mbarikiwe Malongazzzzz.
                                    Ahsante sana mamaKisa.
                                       Ahsante sana Dj Rik/blogger wa the network.





                   Chakula; Nyama choma na vyote,Vimepikwa kwa  da'Batuli.
Ahsanteni sana wote kwa Upendo na kutoa Muda wenu kwa kujumuika nasi ,  Mungu awabariki sana,Tunawatakia kila lililo jema.Kwaniaba ya da'Maggie ,da'Vick na Familia yangu,TUNAWAPENDA SANA.


Wednesday 19 October 2011

Nimekumbuka Kwetu,Nyumbani ni Nyumbani!!!!!!!!!!!!

                Nimewakumbuka Rafiki Zangu.
               Nimewakumbuka wa kaka wa Mitaa ya Kwetu.
                           Nimewakumbuka Ndugu zangu.
          Nimewakumbuka Vijana wa Mitaa ya Kwetu.
      Nimekumbuka hata Usafiri Wetu.
Nimekumbuka  Maembe,Mabungo na Matunda yote na Wauzaji wake.Hasa Magenge ya Karibu!!!!!

Wapendwa mimi Leo nimekumbuka Kwetu/Nyumbani, yaani ukiniuliza sana machozi yanaweza kunitoka.
Nanimekumbuka meeeeengiiiiii yakwetu.

Zamani ikiwa Likizo tunapelekwa kwa bibi mzaa mama[bi' Mwalimu], sasa ukiona naanza kuandika majina ya ndugu zangu,marafiki na wazazi wangu ujue kumekucha, nikimaliza kuandika bibi ajiandae kunirudisha.Na kila j'Mosi tunapelekwa kwa bibi mzaa baba[bi'MwanaPenza],yeye alikuwa mzee kidogo hawezi kutuhudumia, Hatukai sana huko, nae akiona narudi rudi ndani kunywa maji ajiandae na maswali baba alisema atakuja saangapi?akizugazuga tuu nitamuangushia kilioooo mpaka atuja kwanini tulienda.

Duuhhhh sasa huku nilipo sasa na Ukubwa huu sijui nifanye nini??
Nimeimba leo kuanzia Nyimbo za mchakamchaka,za mwalimu Kachale,Kibuzi,Ukuti na zote za utoto,
Nikahamia Youtube na Cd zote za Nyumbani, lakini nikaona Haitoshi ngoja nishiriki nanyi.

Jee Mpendwa nawe kunasiku yanakukuta haya na je unafanya nini ili kusahau?au unajifariji vipi?

Karibuni sana kwa mchango wa mawazo na Ushauri!!!!!!!!!