Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Shukrani. Show all posts
Showing posts with label Shukrani. Show all posts

Sunday 9 August 2015

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA NEW YORK NCHINI MAREKANI.


Mchungaji Butiku akiongoza misa ya shukurani na arubaini ya
marehemu Mzee Samuel Luangisa iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 8,
2015 Mount Vernon, New York na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki
kutoka kila pembe ya Marekani.
Mrs Luangisa, mke wa marehemu akifuatilia misa.


Wanafamilia wakifuatilia misa.


Wajukuu wa marehemu wakifanya onesho la kumenzi babu yao.


Mtoto wa marehemu Mao Luangisa akitoa salamu za shukurani.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Hajji Khamis akiongea
machache huku akisisitiza upendo na mshikmano kwenye Jumuiya za
Watanzania hususani zile zilizopo nje ya Tanzania kwani kwa kufanya
hivyo Jumuiya zitakua imara.


Mchungaji Butiku akiongoza misa.


Wakati wa maakuli.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Saturday 19 April 2014

Shukrani/Asanteni Wote na MUNGU awabariki Sana!!!!


Salaam Waungwana;

Tunamshukuru MUNGU mwenyeezi kwa yote.
Tunamshukuru MUNGU kwa maisha ya Mama/Bibi yetu mpendwa Khadija Mgaya Chuma[bibi Mwalimu].
Tunamshukuru MUNGU kwa kufanikisha vyema,Mazishi ya Mpendwa wetu.
Bi Khadija alifariki usiku wa Jumanne na Kuzikwa siku Alhamisi katika Makaburi ya Ilala Mchikichini.Dar.
Mama Kiwinga na Familia yake,Wanawashukuru sana Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani na Wote walioshiriki kwa Michango,Muda,Upendo,Faraja, Sala/Dua na Mengineyo.
MUNGU azidi kuwabariki na kuwaongezea kila lililo jema kwenu.

Wenu Mama Kiwinga
Wa Ilala Sharifu/Shamba.

Asante Sana.


"Swahili Na Waswahili" Tunawashukuru wote katika yote.

Wednesday 1 August 2012

Siku Kama ya Leo da'Rachel-siwa Alizaliwa!!!!!MUNGU yu Mwema Kwanguuuuuuu

Siku kama ya Leo Familia ya M.S.Kiwinga walipata Mtoto wa kike!!!!
Mimi Rachel-siwa NaMshuru sana Mungu kwa Mema Yooote Maishani Mwangu.
Kwangu hakuna baya na nilipo hisi baya Nafuta na Kusema ni MAPITO[MITIHANI]TUU.WEWE UNATOSHA BABA!!!.

 Mtoto  kwa Wazazi atabaki kuwa mtoto hata kama ana Watoto.
Ninawashukuru sana Wazazi wangu kwa yooote mliyojaaliwa kunipatia kulingana na Uwezo wenu,
Nawapenda,Nitaendelea Kuwapenda mpaka mwisho wa Maisha Yangu.
BABA najua hayupo nami kimwili lakini Kiroho nipo nawe na nitaendelea kukumbuka Daima.

Nikushukuru UBAVU wangu ISAAC,Asante sana kwa yooote,MUNGU Azidi kutusimamia katika Maisha yetu.Mimi Penda sana wewe Mubena yangu!!!!!

Niwashuru sana Kaka,Dada,Watoto  Zangu woote Nawapenda.

Pia Niwashukuru Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani na Wooote wanaonifahamu kwa njia moja au nyingine.

Kamwe Sijutii kufahamiana nanyi, Basi Nirudishe Shukrani kwa MUNGU najua ni mpango wake kuniunganisha nawe.

Nanilipo kosea/kukukosea Naomba Nisamehe,Kwani Nami ni Bin'Adam Sijakamilika.

Nawapenda woote wakubwa kwa watoto,Wake kwa Waume.

MUNGU TUBARIKI SOOOOTE.
AMEEN.

Tuesday 5 June 2012

SHUKRANI KUTOKA KWA MCHUNGAJI JOHN KUPAZA WA KANISA LA BAPTIST TANGA.


Marehemu Mama Mchungaji John Kupaza
Familia ya Mchungaji John Kupaza wa Kanisa la Baptist Kisosora Tanga anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliojaribu kuokoa maisha ya Mke wake Mpendwa Marehemu Mama Mchungaji Kupaza na wale walioshiriki kwa dhati katika shughuli za mazishi.
Mchungaji J. Kupaza anapenda shukrani zake za dhati ziwafikie Baptist Convention of Tanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Wanawake wa Baptist Tanzania, Dr. Lugano Mtafya, Umoja wa Makanisa ya Baptist Dar es salaam, Baptist Kanda ya Kaskazini, Umoja wa Makanisa Tanga, Manesi na Wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili, Hospitali ya Cancer ya Ocean Road, Hospitali ya Bombo Tanga, Madaktari na wauguzi wa Magomeni Baptist Center, Majirani wote wa Mchungaji Kupaza na watoto wa Marehemu Sarah, Samwel, Rosemary, Dr. Lawi, Potinna, David na Tumaini wote kwa pamoja wanawashukuru wote mlioshirikiana nao katika kipindi hiki kigumu. Mungu awabariki wote.
Marehemu Mama Mchungaji Kupaza alifariki Tar. 18/05/2012 Jijini Dar es slaam na kuzikwa Tarehe 21/05/2012 Jijini Tanga katika makaburi ya Bombo.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMEN.

Sunday 4 December 2011

PETER KAPINGA SIKU ALIPOTUNUKIWA KAMISHENI NA RAIS DR JAKAYA KIKWETE.


Luteni Peter Kapinga

Tarehe 26/11/2011 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama Amiri Jeshi Mkuu aliwatunuku Kamisheni wanachuo wa Chuo cha kijeshi cha Monduli Mkoani Arusha.

Peter akiwa mmoja wa wahitimu hao anapenda kuwashukuru wote ambao walioshiriki katika kumsaidia kwa namna moja na nyingine mpaka amefikia hapo alipofikia, zaidi anapenda kumshukuru Dada ake Esther Mbapila pamoja na Mr Mbapila kwa kushiriki katika mchakato wote mpaka akafanikisha kupata alichokihitaji.
ASANTENI
Nasi Swahili na Waswahili tunakutakia kila lililojema katika Yote.

Thursday 17 November 2011

SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA JUMA PENZA[JP]!!!


Marehemu JUMA PENZA enzi za uhai wake.
Familia ya Juma Penza ya Gongo la Mboto Dar es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana  nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa, aliyefariki dunia tarehe 12/10/2011 katika hospitali ya Hindu Mandal na kuzikwa tarehe 13/11/2011 katika makaburi ya Kisutu. 



Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. J.M. Kikwete, CCM Makao Makuu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na kwa namna mlivyoshiriki katika shughuli zote za mazishi.  Shukrani za pekee ziwaendee Dr. Macha Ocean Road, wauguzi na madaktari  wa Hindu Mandal.


Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru  kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi  mzipokee  wote kwa mikono miwili  kutokana na jinsi mlivyohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha  shughuli nzima ya msiba wa baba yetu mpendwa Mzee JP.


Tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu  nasi  kwa dua  na maombi wakati wote  hadi tulipompumzisha baba yetu kipenzi .


Vilevile  tunapenda  kuwakaribisha  katika  mkesha  wa dua  itakayofanyika  Ijumaa usiku  Novemba 18 kuamkia siku ya Jumamosi Novemba 19 ambapo khitma  itasomwa  nyumbani kwa marehemu  Gongo la Mboto Dar es es Salaam wote mnakaribishwa .


Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu. Mkesha na kisomo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/11/2011 na kufuatiwa na  Khitma itakayosomwa Jumamosi tarehe 19/11/2011 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.Inna lilah Wainna Ilaih Rajiun

Wednesday 28 September 2011

Mtoto Cecilia Edward Aenda India kwa Matibau!!!!!!!









Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.






CECILIA AWASHUKURU WATANZANIA
   Mtoto Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.
   Cecilia amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.
   Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
   Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
   Mtoto huyu aliondoka hapa nchini jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja  na mlezi mmoja mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa  na madaktari tayari kwa uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
   Kipindi cha Mimi na Tanzania kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na makampuni mbalimbali yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya matibabu. Shukrani za pekee ziifikie hospitali ya regency hasa daktari Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa Sesilia, mzazi na daktari ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi sasa.
   Watanzania, pamoja tumeweza tena. Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na tatizo hili, hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu kwa maombi ili upasuaji anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi yake Mungu mtoto huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto wengine.
Mungu mbariki Sesilia.Amen!
        :Swahili na Waswahili tunakuombea cecilia,Mungu asimamie Matibabu yako na upone haraka.


Habari hii kutoka kwa Zainul.A.Mzinge wa www.mohammedewji.com/blog.





-