Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mswahili Mitaani. Show all posts
Showing posts with label Mswahili Mitaani. Show all posts

Friday 16 May 2014

Matembezi ya Mswahili Vijijini;Burudani-Nuta Jazz Band (Tanzania) - Pongezi Wakulima (60's Tanzanian Rumba!)

Waungwana;Nipatapo muda huwa napenda kuzunguka/Kutembea na kujifunza/kujione mambo yakoje...
Basi Leo niwapeleke Shamba /Vijijini kidogo.

Swali.....
Wakulima wa Ng'ambo wapi wanapatia na Wakulima wa Afrika wapi wanakosea?
Jee Mkulima ni Mtu Masikini/Fukara,Mnyonge,Kaishiwa na........?

Jee unapenda kuwa Mkulima?








Nuta....Pongezi kwa Wakulima...


"Swahili Na Waswahili" Muwe na Wakati Mwema.

Tuesday 28 August 2012

Pitapita ya Mswahili Mitaani-Coventry!!!!

                                   Alikutana na Wapiga Ngoma
                                   Ikapigwa na Akacheza
Mswahili mtoto akapiga ngoma nae


Banda la Wazungu, wanauza vitu kutoka kwa Waswahili wa KENYA



                            Banda la M'SENEGAL,Ameshona hizo Nguo na hivyo vidude wanatengeneza.

Waungwana ni "Pitapita ya Mswahili Mitaani" Ilikuwa Coventry.  kulikuwa na Mabanda mbalimbali ya Bidhaa , Vyakula na Michezo.

Kwabahati mbaya WaTanzania hatukuwa na Banda.
Nimatumaini yangu siku/wakati mwingine tutakuwa na Banda hata la Mchezo wa Bao,Kijiwe cha Kahawa ile Chunguu yanywewa kwa Vikombe Vidoogo na Kashata.

 Ndugu wa mimi/Blogger Mwenza EMU wa Three.Mmmhhh Ushauri wako Naufanyia Kazi.Hahahaha Eti Ndugu wa mimi ananishauri  nijiunge na Michezo kama Miereka,Judo,Sarakasi ,Kuogelea na.........Uwiiii Kweli umenichoka, Sikuweza Mikundeni itakuwa Michorokoni? hhahaha na Uzee huu mwili umekomaaa.Hahah Usichekeshe walionuna.

Sina Meengi,Unalolote la kuongezea,Maoni,Ushauri?
Pamoja sana "Swahili NA Waswahili"