Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 21 August 2019

Kikombe Cha Asubuhi; Wimbo Ulio Bora2...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Sisi tunajivunia kitu kimoja: Dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali na neema ya Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Tunawaandikia nyinyi mambo mnayoweza kuyasoma na kuyaelewa. Ninatumaini kwamba mtaelewa vizuri kabisa,
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea nyinyi fahari.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

1Mimi ni ua la Sharoni,
ni yungiyungi ya bondeni.
Bwana arusi
2Kama yungiyungi kati ya michongoma,
ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wasichana.
Bibi arusi
3Kama mtofaa kati ya miti ya msituni,
ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wavulana.
Nafurahia kuketi chini ya kivuli chake,
na tunda lake tamu sana kwangu.
4Alinichukua hadi ukumbi wa karamu,
akatweka bendera ya mapenzi juu yangu.
5Nishibishe na zabibu kavu,
niburudishe kwa matofaa,
maana naugua kwa mapenzi!
6Mkono wake wa kushoto chini ya kichwa changu,
mkono wake wa kulia wanikumbatia.
7Nawasihi enyi wanawake wa Yerusalemu,
kama walivyo paa au swala wa porini,
msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,
hadi hapo wakati wake utakapofika.
Shairi la pili
Bibi arusi
8Hiyo ni sauti ya mpenzi wangu,
yuaja mbio,
anaruka milima,
vilima anavipita kasi!
9Mpenzi wangu ni kama paa,
ni kama swala mchanga.
Amesimama karibu na ukuta wetu,
achungulia dirishani,
atazama kimiani.
10Mpenzi wangu aniambia:
Bwana arusi
“Inuka basi, ewe mpenzi wangu, unipendezaye,
njoo twende zetu.
11Tazama, majira ya baridi yamepita,
nazo mvua zimekwisha koma;
12maua yamechanua kila mahali.
Wakati wa kuimba umefika;
sauti ya hua yasikika mashambani mwetu.
13Mitini imeanza kuzaa;
na mizabibu imechanua;
inatoa harufu nzuri.
Njoo, basi, ewe mpenzi wangu unipendezaye,
njoo twende.
14Ee hua wangu, uliyejificha miambani.
Hebu niuone uso wako,
hebu niisikie sauti yako,
maana sauti yako yapendeza na uso wako wavutia.
15“Tukamatieni mbweha,
wale mbweha wadogowadogo,
wanaoiharibu mizabibu yetu inayochanua.”
Bibi arusi
16Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake.
Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,
17hadi hapo jua linapochomoza
na vivuli kutoweka.
Rudi kama paa mpenzi wangu,
kama swala mdogo juu ya milima ya Betheri.

Wimbo Ulio Bora2;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: