Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 2 August 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Tunamshukuru Mungu tumemaliza Kitabu cha -Methali ,Leo Tunaanza Kitabu Cha Mhubiri 1..

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha

 kupitia kitabu cha "
METHALI"
Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza/kufaidika
 kwenye kitabu hiki...


Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha "MHUBIRI" tunamuomba Mungu wetu akatupe kibali,macho ya rohoni
 na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake...
Ee Mungu  tunaomba ukatuongoze...!!

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele. Watu wa Israeli na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.” Wazawa wa Aroni na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.” Wote wamchao Mwenyezi-Mungu na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Katika taabu yangu nilimwomba Mwenyezi-Mungu, naye akanisikia na kuniweka huru. Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Mwenyezi-Mungu yuko nami, kunisaidia; nami nitawaona maadui zangu wameshindwa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu, kuliko kumtumainia mwanadamu. Afadhali kukimbilia usalama kwa Mwenyezi-Mungu, kuliko kuwatumainia viongozi wa dunia.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Maisha ni bure kabisa
1Yafuatayo ni maneno ya Mhubiri1:1 Mhubiri: Kiebrania: Kohelethi. mwana wa Daudi, aliyekuwa mfalme huko Yerusalemu.
2Bure kabisa, bure kabisa,
nakuambia mimi Mhubiri!
Kila kitu ni bure kabisa!
3Binadamu hufaidi nini
kwa jasho lake lote hapa duniani?
4Kizazi chapita na kingine chaja,
lakini dunia yadumu daima.
5Jua lachomoza na kutua;
laharakisha kwenda machweoni.
6Upepo wavuma kusini,
wazunguka hadi kaskazini.
Wavuma na kuvuma tena,
warudia mzunguko wake daima.
7Mito yote hutiririkia baharini,
lakini bahari kamwe haijai;
huko ambako mito hutiririkia
ndiko huko inakotoka tena.
8Mambo yote husababisha uchovu,
uchovu mkubwa usioelezeka.
Jicho halichoki kuona,
wala sikio kusikia.
9Yaliyokuwako ndio yatakayokuwako,
yaliyotendeka ndio yatakayotendeka;
duniani hakuna jambo jipya.
10Watu husema, “Tazama jambo jipya,”
kumbe lilikwisha kuwako zama za kale.
11Hakuna mtu anayekumbuka ya zamani
wala atakayekumbuka yatakayotukia baadaye.
Aliyoyaona Mhubiri
12Mimi Mhubiri, nilikuwa mfalme wa Israeli, huko Yerusalemu. 13Nilipania kuchunguza na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachotukia duniani. Hiyo ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu.
14Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: Ni sawa na kufukuza upepo!
15Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa,
kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa.
16Basi, nikatafakari nikisema, “Nimejipatia hekima nyingi zaidi kupita wote waliopata kutawala Yerusalemu kabla yangu. Naam, nina uzoefu wa hekima na maarifa.”
17Nilipania kubainisha kati ya hekima, wazimu na upumbavu. Lakini niligundua kwamba kufanya hivyo ni sawa na kufukuza upepo.
18Maana katika kuwa na hekima nyingi mna wasiwasi;
na aongezaye maarifa zaidi huongeza huzuni zaidi.


Mhubiri1;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: