Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 22 February 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 2 Samueli 18...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Asante Mungu wetu Baba yetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Si kwamba sisi ni wema sana wala si kwa nguvu zetu utashi wetu wala si kwamba sisi ni wazuri mno si kwa akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa neema/rehema zako ni kwa Mapenzi yako Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo....
Neema yako yatutosha ee Mungu wetu,Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako niya ajabu,Matendo yako yanatisha Yahweh
Hakuna lisilowezewekana mbele zako Mungu wetu,Utukuzwe ee Mungu wetu,wewe ni mwanzo na wewe ni mwishi,Alfa na Omega..
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..!!

Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia. Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali. Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Mchana jua halitakuumiza, wala mwezi wakati wa usiku. Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.
Tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Yahweh
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah
Mungu wetu tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea...
Baba wa Mbinguni tunaomba utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba, waijengao wanajisumbua bure. Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure. Mnajisumbua bure kuamka mapema asubuhi na kuchelewa kwenda kupumzika jioni, mjipatie chakula kwa jasho lenu. Mungu huwaruzuku walio wake hata walalapo. Watoto ni riziki kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; watoto ni tuzo lake kwetu sisi. Watoto waliozaliwa wazazi wakiwa bado vijana, ni kama mishale mikononi mwa askari. Heri mtu aliye na mishale hiyo kwa wingi. Hatashindwa atakapokabiliana na adui mahakamani.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba  ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe....

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Yahweh tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Jehovah tunaomba ukatamalaki na kutuatamia Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu,Neema yako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu,Baba wa Mbinguni tukawe salama moyoni Jehovah ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii,Mungu wetu ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Jehovah ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu ukaonekane  popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni...
Yahweh tukanene yaliyo yako,ukatuepushe na kiburi,majivuno,ubinafsi,choyo,fitina,unafiki,ugombanishi,makwazo na yote yanayokwenda kinyume nawe...
Mungu wetu ukatupe neema ya Hekima,busara,utuwema,fadhili,huruma,Imani,upendo ukadumu kati yetu na yote yanayokupendeza wewe..
Jehovah ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....


Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake. Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka. Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako. Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Uishi na hata uwaone wajukuu zako! Amani iwe na Israeli!

Mungu wetu tunarudisha shukrani na utukufu una wewe
Asante kwa majibu yako,Asante kwa uponyaji wako,Asante kwa wokovu wako,Asante kwa yote uliyotutendea/unayoendelea kututendea Mungu Baba,Hakuna kama wewe Mungu wetu,Mungu mwenye kujibu,Mungu mwenye kusikia,Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye kubariki
Yahweh mkono wako wenye nguvu na uponyaji umeponya,umebariki umetenda meengi ya ajabu,Tulikuita ukaitaka,tulikuomba ukajibu,tulikulilia ukatufuta machozi,Umekuwa mwema sana kwetu umekuwa faraja kwetu
imani na amani imetanda kwa watoto wako waliokuja kwako na kukuomba  ukuwajibu na kuwapa furaha,Mungu wetu si kiziwi anasikia,Mungu wetu si bubu anajibu,Mungu wetu si kipofu anaona,Mungu wetu si binadamu hata aseme uongo...!!
Mungu wetu ni Mungu wa walio hai akisema atabariki na huwa anabariki
mpe Yesu maisha yako,Mkabidhi dhiki zako shida na magonjwa kwakwe yeye hakuna linaloshindikana,maarifa na akili,ubunifu na mbinu vyote vina yeye tembea naye wakati wote,imba sifu abudu shangilia Mungu anatoshaaa...!!!

Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako na wengine
wanao kungoja,wanaokuita kwa bidii na imani,Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kufuata njia zako na kujiombea,Mungu wetu ukaonekane katika mapito yao,Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe,Yahweh ukawasimamishe na kuwabariki
Nuru yako ikaangaze Yahweh ukawape macho ya rohoni,imani,wakawe salama moyoni,wakasikie sauti yako na kuitii,Ee Baba wa Mbinguni ukawatendee sawasawa na mapenzi yako...
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Bwana Yesu kwakuwa nami/kunisoma
Pendo lenu likadumu amani ikawe nanyi daima,furaha na upole kiasi
Mungu wetu akawaguse kwa mkono wake wenye nguvu nanyi mkawe salama moyoni...
Nawapenda. 




Absalomu anashindwa na kuuawa

1Daudi aliwahesabu watu waliokuwa pamoja naye, akawagawanya katika vikosi vya maelfu chini ya makamanda wao; na vikosi vya mamia, navyo chini ya makamanda wao. 2Daudi akalituma jeshi lake vitani katika vikosi vitatu: Theluthi moja chini ya Yoabu, theluthi ya pili chini ya Abishai mwana wa Seruya, nduguye Yoabu; na theluthi ya tatu chini ya Itai, Mgiti. Kisha mfalme Daudi akawaambia wote, “Mimi mwenyewe binafsi nitakwenda pamoja nanyi.” 3Lakini watu wakamwambia, “Hutatoka. Maana, ikiwa tutakimbia, hawatajali juu yetu. Ikiwa nusu yetu watakufa, pia hawatajishughulisha juu yetu. Lakini wewe una thamani kuliko watu 10,000 miongoni mwetu. Hivyo inafaa wewe ubaki mjini na kutupelekea msaada ukiwa mjini.” 4Mfalme akawaambia, “Lolote mnaloona ni bora kwenu, nitalitenda.” Hivyo, mfalme akasimama kando ya lango, huku jeshi lake likipita: Mamia na maelfu. 5Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kwa ajili yangu, mtendeeni yule kijana Absalomu kwa upole.” Watu wote walimsikia mfalme alipoamuru makamanda wake kuhusu Absalomu.
6Hivyo, jeshi la Daudi likaenda nyikani kupigana na watu wa Israeli. Mapigano hayo yalifanyika katika msitu wa Efraimu. 7Watumishi wa Daudi waliwashinda watu wa Israeli. Mauaji ya siku hiyo yalikuwa makubwa kwani watu 20,000 waliuawa. 8Mapigano hayo yalienea nchini kote na watu wengi walikufa msituni kuliko wale waliouawa kwa upanga vitani.
9Kisha Absalomu, akiwa amepanda nyumbu, alikutana na watumishi wa Daudi. Nyumbu huyo alipokuwa anapita chini ya tawi kubwa la mwaloni, hapo kichwa cha Absalomu kikakwama kwenye mwaloni. Absalomu akaachwa ananinginia juu. Lakini nyumbu wake akaendelea mbele. 10Mtu fulani aliyeona tukio hilo, akamwambia Yoabu, “Nimemwona Absalomu akininginia kwenye mwaloni.” 11Yoabu akamwambia mtu huyo, “Nini? Ulimwona Absalomu? Kwa nini, basi, hukumpiga papo hapo hadi ardhini? Ningefurahi kukulipa vipande kumi vya fedha na mkanda.” 12Lakini yule mtu akamwambia Yoabu, “Hata kama ningeuona uzito wa vipande 1,000 vya fedha mkononi mwangu, nisingeunyosha mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Maana, tulimsikia mfalme alipokuamuru wewe Abishai na Itai kwamba, kwa ajili yake, mumlinde kijana Absalomu. 13Kwa upande mwingine, kama ningemtendea kwa hila18:13 kama … hila: Au hata kama ningeyahatarisha maisha yangu. (na hakuna lolote linalofichika kwa mfalme) wewe mwenyewe ungeniruka.” 14Yoabu akamwambia, “Mimi sina wakati wa kupoteza pamoja nawe.” Hapo Yoabu akachukua mikuki midogo mitatu mkononi mwake, akaenda na kumchoma Absalomu moyoni, Absalomu akiwa bado hai kwenye tawi la mwaloni. 15Kisha, vijana kumi waliombebea silaha Yoabu, wakaja kumzunguka Absalomu, wakampiga na kumwua.
16Ndipo Yoabu akapiga tarumbeta na wanajeshi wote wakarudi kuwafuatia watu wa Israeli, kwani Yoabu aliwakataza. 17Wakamchukua Absalomu wakamtupa kwenye shimo kubwa msituni na kurundika rundo kubwa sana la mawe. Watu wote wa Israeli wakakimbia, kila mmoja nyumbani kwake. 18Absalomu, wakati wa uhai wake, alikuwa amejijengea na kujisimikia nguzo iliyoko kwenye Bonde la Mfalme, kwani alisema, “Mimi sina mtoto wa kiume wa kudumisha jina langu ili nikumbukwe.” Nguzo hiyo aliipa jina lake, na inaitwa “Nguzo ya Absalomu” mpaka leo.

Daudi anaarifiwa juu ya kifo cha Absalomu

19Kisha, Ahimaasi mwana wa Sadoki, akasema, “Niruhusu nikimbie kumpelekea mfalme habari hizi kuwa Mwenyezi-Mungu amemkomboa katika nguvu za adui zake.” 20Yoabu akamwambia, “Leo, hutapeleka habari hizo. Unaweza kupeleka habari hizo siku nyingine. Lakini leo hutapeleka habari zozote kwa kuwa mwana wa mfalme amekufa.” 21Ndipo Yoabu akamwambia mtu mmoja, Mkushi, “Wewe, nenda ukamweleze mfalme yale uliyoona.” Mkushi akainama kwa heshima mbele ya Yoabu, akaondoka mbio. 22Kisha Ahimaasi mwana wa Sadoki akamwambia Yoabu tena, “Haidhuru; niruhusu na mimi nimkimbilie yule Mkushi!” Yoabu akamwambia, “Mbona unataka kukimbia mwanangu? Wewe hutatuzwa lolote kwa habari hizi!” 23Ahimaasi akamwambia, “Haidhuru; nitakimbia.” Basi, Yoabu akamwambia, “Haya, kimbia.” Kisha Ahimaasi akakimbia akifuata njia ya nyikani akawahi kumpita yule Mkushi.
24Daudi alikuwa ameketi kati ya malango mawili ya mji. Naye mlinzi wa lango akapanda ukutani hadi juu ya lango na alipoinua macho yake aliona mtu anakimbia peke yake. 25Huyo mlinzi akapaza sauti akamwambia mfalme. Mfalme akasema, “Kama yuko peke yake, lazima ana habari.” Yule mtu akazidi kukaribia. 26Mlinzi akamwona mtu mwingine anakimbia, akaita tena langoni akisema, “Tazama, mtu mwingine anakimbia peke yake!” Mfalme akasema, “Naye analeta habari.” 27Yule mlinzi akasema, “Naona kuwa yule anayekimbia zaidi ni Ahimaasi mwana wa Sadoki.” Mfalme akasema, “Huyo ni mtu mwema, anatuletea habari njema.”
28Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.” 29Mfalme akamwambia, “Je, kijana Absalomu hajambo?” Ahimaasi akasema, “Wakati Yoabu aliponituma mimi mtumishi wako,18:29 mimi mtumishi wako: Kiebrania: Mtumishi wa mfalme pia mtumishi wako. niliona kulikuwa na kelele nyingi, lakini sikufahamu maana yake.” 30Mfalme akasema, “Kaa kando, na usimame hapo.” Basi, Ahimaasi akaenda kando na kusimama kimya.
31Ndipo na yule Mkushi akafika; naye akasema, “Kuna habari njema kwako bwana wangu mfalme! Maana Mwenyezi-Mungu leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote walioinuka dhidi yako.” 32Mfalme akamwuliza, “Je kijana Absalomu hajambo?” Mkushi akasema, “Maadui wako, bwana wangu mfalme, pamoja na wote wanaoinuka dhidi yako wakikutakia mabaya, wawe kama huyo kijana Absalomu.” 33Hapo mfalme alishikwa na huzuni kuu, akapanda kwenye chumba kilichokuwa juu ya lango na kulia. Alipokuwa anapanda, akawa analia akisema, “Mwanangu Absalomu, mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako! Ole, Absalomu mwanangu! Mwanangu!”

2Samweli18;1-33

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: