Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 4 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..24


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu na kimbilio letu..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Mfalme wa Amani Baba wa Upendo..Utukuzwe Baba wa Rehema..
Unastahili sifa na kuabudiwa daima..
wewe Ndimi Mwenyezi-Mungu..Muumba wa vyote..!
Wewe ni Alfa na Omega..!
Sifa na Utukufu ni wako Jehovah..!

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..!
Asante kwa ulinzi wako wakati wote...
Asante kwa kutuamsha salama na wenye afya tayari kwakuendelea na majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona leo hii..
Si kwamba sisi ni wema sana ,si kwamba wazuri mno au ni kwanguvu zetu..
Hapana Mungu wetu ni kwa Neema/Rehema zako tuu sisi kuwa hivi tulivyo..
Jehovah tunakuja mble zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..

Ukatubariki na Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu Baba ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani ukawaponye na kuwagusa na mkono wako wenye nguvu wote wanaopitia magumu/majaribu,shida/tabu..Ukawape neema ya kusimamia Amri,sheria zako na Neno lako nalo likawaweke huru..Yesu alipokwisha sema hayo, alitazama juu mbinguni, akasema, “Baba, ile saa imefika! Mtukuze Mwanao ili naye Mwana apate kukutukuza. Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uhai wa milele wote hao uliompa. Na uhai wa milele ndio huu: Kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli, na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu. “Nimekufanya ujulikane kwa watu wale ulionipa kutoka duniani. Walikuwa watu wako, nawe ukanipa wawe wangu; nao wamelishika neno lako. Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako. Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa, nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma. “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale ulionipa, maana ni wako. Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana katika hao ulionipa. Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja. Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule mwana mpotevu, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia. Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu. Mimi nimewapa ujumbe wako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu. Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu. Waweke wakfu katika ukweli; neno lako ni ukweli. Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni; na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli. “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao. Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma. Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja; mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi. “Baba! Nataka hao ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu. Baba Mwema! Ulimwengu haukujui, lakini mimi nakujua. Hawa nao wanajua kwamba wewe ulinituma. Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao.”
Jehovah ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
tuliyoyanena na tusiyoyanena Mfalme wa Amani unayajua na kutujua sisi zaidi ya tunavyojijua..
Utukuzwe milele..Uabudiwe daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa kwakuwa nami..
Mungu aendelee kuwabariki katika yote yampendezayo..
Nawapenda.1Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani. 2Alitazama juu akawaona Waisraeli wamepiga kambi, kila kabila mahali pake. Kisha roho ya Mungu ikamjia, 3naye akatamka kauli hii ya kinabii:
Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori
kauli ya mtu aliyefumbuliwa24:3 aliyefumbuliwa: Au aliyefumbwa, au aonaye vema. macho;
4kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu
mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu,
mtu anayesujudu na kuona wazi.
5Hema zako zapendeza namna gani enyi watu wa Yakobo;
naam, kambi zenu enyi watu wa Israeli!
6Ni kama mabonde yanayotiririka maji,
kama bustani kandokando ya mto,
kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu,
kama mierezi kandokando ya maji.
7Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji,24:7 Yatapata … kutosha: Kiebrania: Maji yatatiririka kutoka ndoo zake.
mbegu yao itapata maji mengi,
mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi,
na ufalme wake utatukuka sana.
8Mungu aliwachukua kutoka Misri,
naye huwapigania kwa nguvu kama nyati.
Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao,
atavunjavunja mifupa yao,
atawachoma kwa mishale yake.
9Ataotea na kulala chini kama simba,
nani atathubutu kumwamsha?
Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli,
alaaniwe yeyote atakayewalaani.
10Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki! 11Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”
12Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu 13kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14“Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.” 15Basi, Balaamu akatamka kauli hii:
“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,
kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu,
na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu,
mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu,
mtu anayesujudu, macho wazi.
17Ninamwona, atakayekuja, lakini baadaye,
namwona, lakini hayuko karibu.
Nyota itatokea kwa wazawa wa Yakobo,
atatokea mfalme miongoni mwa Waisraeli.
Kwa fimbo yake atawachapa viongozi wa Wamoabu
atawaangamiza wazawa wote wa Sethi.
18Edomu itamilikiwa naye,
Seiri itakuwa mali yake,
Israeli itapata ushindi mkubwa.
19Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala
naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.”
20Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii:
“Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote,
lakini mwishoni litaangamia kabisa.”
21Kisha Balaamu akawaangalia Wakeni, akatoa kauli hii:
“Makao yenu ni salama, enyi Wakeni,
kama kiota juu kabisa mwambani.
22Lakini mtateketezwa, enyi Wakeni.
Mtachukuliwa mateka na Ashuru mpaka lini?”24:22 aya ya 22 makala ya Kiebrania si dhahiri.
23Tena Balaamu akatoa kauli hii:
“Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo?
24Meli zitafika kutoka Kitimu,
wataishambulia Ashuru na Eberi,
lakini nao pia wataangamia milele.”
25Basi, Balaamu akaondoka, akarudi nyumbani; Balaki pia akaenda zake.


Hesabu24;1-25


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: