Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 18 June 2017

Natumaini Jumapili ilikuwa njema/inaendelea vyema;Happy Father's Day..Burudani-Phil Wickham - This Is Amazing Grace,At Your Name (Yahweh Yahweh)Shalom wapendwa/waungwana;Nimatumaini yangu mnaendelea vyema na mmekuwa kuwa na wakati mzuri Jumapili hii..
Hapa kwetu leo kijua kimewaka haswaaa kama tupo Dar..
Tunamshukuru Mungu katika yote..

Niwatakie heri na baraka wa Baba wote.."Happy Father's Day" kwa wazazi/Baba wote wanaojua majukumu yao ..
Mungu aendelee kuwaongoza katika malezi ya watoto wenu na kwa watoto wengine wote..

Nimshukuru Baba wa watoto wangu kwa kuwa karibu na watoto wake na kujua/kutumikia majukumu yake..Mungu aendelee kumuongoza..
R.I.P. Baba yangu haupo nasi lakini kila leo tunakukumbuka katika yote..
ulipokuwa unatuasa/kutufundisha ,Kutushauri yooote tunayaona  sasa..
Ulipokuwa unasema wakati ule tulikuwa tunaona kama unaimba au unaongea sana[unatuzingua]
Maneno hayaozi...
Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo yeye nimwema tuu..Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.” Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.


Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu, tegeni sikio mpate kuwa na akili.

Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha nyinyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi. Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema. Kwa hiyo, nawasihi: Fuateni mfano wangu. Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

No comments: