Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 26 April 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Kutoka 20...
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu wetu kwa mambo mengi na makuu ..

Asante Baba wa Mbinguni kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Tazama Jana imepita Baba Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine..!!
Tunaomba ukaibariki siku hii na ukatubariki katika maisha yetu..

Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni,Maisha yetu yapo nawe  Yahweh..!! Amani inapatikana kwako, Upendo wa kweli una wewe Jehovah..!Furaha ipo kwako..!
Tumaini letu ni wewe jehovah..!!Mungu wetu,Muumba wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!!
Tunaomba ukabariki kazi zetu,Biashara,Masomo,Vyombo vya usafiri,Tuingiapo,tutokapo,hatua zetu ziwe nawe Jehovah..Vilaji/vinywaji,Ukabariki Ridhiki zetu ziingiazo na zitokazo, vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba ukavitakase kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana wetu na mwakozi wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..Jehovah.. ukatutakase Miili yetu na Akili zetu, tupate kutambua/kujitambua..
Roho Mtakatifu ukatuongoze kwenye kunena/kutenda na tukawe na kiasi..
Tunakwenda kinyume na yule mwovu na kazi zake zote..
Baba wa mbinguni ukatuokoe na kutufunika na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Tunakuja mbele zako Baba tunaomba utusamehe pale tulikwenda kinyume nawe,kwakuwaza,kwakutenda,kwakunena,kwakujua,kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba utupe na sisi Neeema ya kuweza kuwasamehe wote waliotukosea ..
Yahweh..ukawaguse na mkono wako wenye nguvu ,ukawaponye na kuwaokoa wote waliokwenye vifungo mbalimbali,Wagonjwa,wafiwa ukawemfariji wao,wenye shida/tabu,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali..Baba ukawaponye kimwili na kiroho..Baba ukaonekane kwenye shida zao..
Wapendwa tuendelee kuamini na kumtumaini Mungu wetu yeye atosha..

Yesu ni ufufuo na uhai..!!


Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne. Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu, umbali upatao kilomita tatu. Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao. Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa! Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.” Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.” Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi; na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?” Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana! Mimi naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Baba wa Mbinguni tukiamini na kushukuru..
Amina..!
Asante kwa wote mliopita hapa Mungu aendelee kuwabariki na kuwaongoza katika maisha yenu..
Nawapenda.

Amri kumi
(Kumb 5:1-21)

1Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, 2“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa.
3“Usiwe na miungu mingine ila mimi.20:3 Usiwe … mimi: Au usiwe na miungu mingine zaidi yangu.
4 Taz Kut 34:17; Lawi 19:4; 26:1; Kumb 4:15-18; 27:15 “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. 5Taz Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kumb 7:9-10 Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao. 6Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
7 Taz Lawi 19:12; Kumb 18:20; Roma 13:9; Yak 2:11 “Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Maana mimi Mwenyezi-Mungu sitaacha kumwadhibu anayetumia jina langu vibaya.
8“Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato. 9Siku sita fanya kazi na tenda mambo yako yote. 10Lakini siku ya saba ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala watumishi wako wa kike, wala mnyama wako wa kufugwa, wala mgeni aliye nyumbani mwako. 11Maana kwa siku sita mimi Mwenyezi-Mungu niliziumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo, kisha nikapumzika siku ya saba. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu niliibariki siku ya Sabato, nikaitakasa.
12“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
13“Usiue.
14“Usizini.
15 Taz Lawi 19:11; Mat 19:18; Marko 10:19; Luka 18:20; Roma 13:9 “Usiibe.
16 Taz Kut 23:1 Mat 19:18; Marko 10:19; Luka 18:20 “Usimshuhudie jirani yako uongo.
17“Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”
18Watu waliposikia ngurumo na kuona umeme ukiwaka na kuisikia sauti ya parapanda juu ya mlima uliokuwa unafuka moshi, wote waliogopa na kutetemeka. Wote walisimama mbali, 19wakamwambia Mose, “Ongea nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza, lakini Mwenyezi-Mungu asiongee nasi, tusije tukafa.” 20Mose akawaambia, “Msiogope, maana Mungu amekuja kuwajaribu ili mpate kumcha yeye daima na msitende dhambi.”
21Watu wote walisimama mbali wakati Mose alipokaribia lile wingu zito alimokuwamo Mungu.

Sheria kuhusu madhabahu

22Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli: ‘Mmejionea nyinyi wenyewe kwamba nimeongea nanyi kutoka mbinguni. 23Mtaniheshimu mimi peke yangu wala msijifanyie miungu ya fedha wala ya dhahabu. 24Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki. 25Taz Kumb 27:5-7; Yosh 8:31 Kama mkinijengea madhabahu ya mawe, msiitengeneze kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia vyombo vya kuchongea mawe, mtaitia najisi. 26Wala msitengeneze madhabahu yenye ngazi za kupandia, mtu asije akauona uchi wa huyo anayepanda juu yake.’

Kutoka20;1-26

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: