Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 28 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo49...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Asante Mungu wetu Baba Yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi,Mfalme wa Amani,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...

Tunashukuru na kukusifu daima,Hakuna wa kufanana nawe,Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho...Tazama jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya na Kesho ni sikunyingine Jehovah..!!!Asante kwa ktuchagua kuiona tena Leo hii Baba Mungu, Umetupa Neema/Rehema hii Mfalme wa Amani, si kwamba sisi ni watenda mema sana, kwamba ni wazuri sana,si kwamba wajuaji na wenye nguvu hapana si kwa nguvu/utashi wetu Baba..Bali ni kwa mapenzi yako..
Tunaomba ukaibariki siku hii Baba ..ikawe yenye kukupendeza wewe, Amani na Upendo..Baba Tubariki Tuingiapo/Tutokapo,vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!! 
Vilaji/vinywaji na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase na Damu ya Mwanao, Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo..Ukatutakase Miili na Akili zetu, Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda..
Utusamehe pale tulikwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni..Nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe wengine..
Baba ukwaguse/kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu, Wagonjwa, Wenye Shida/Tabu,Waliovifungoni Baba ukawafungue na ukaweke huru kimwili na kiroho.. 

1Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni,
ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.
2Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima,
ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake,
tangu sasa na hata milele.[Zaburi 125:1-2]

Baba ukawabariki na kuwapa Neema ya kukujua zaidi na Kutembea nawe watoto wetu, familia na wote wakutafutao

10Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea,
wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.
11Mwimbieni sifa Mwenyezi-Mungu akaaye Siyoni.

Yatangazieni mataifa mambo aliyotenda![Zaburi 9:1o-11]

Sifa na Utukufu ni kwako Daima..
Tunajinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu.. Tukiamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina..!!
Mungu awabariki.

Yakobo anawabariki wanawe

1Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo.
2“Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo,
nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu.
3“Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza,
nguvu yangu na tunda la ujana wangu.
Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu.
4“Wewe ni kama maji ya mafuriko.
Lakini hutakuwa wa kwanza tena,
maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako,
wewe ulikitia najisi;
naam wewe ulikipanda!
5“Simeoni na Lawi ni ndugu:
Silaha zao wanatumia kufanya ukatili,
6lakini mimi sitashiriki njama zao;
ee roho yangu, usishiriki mikutano yao,
maana, katika hasira yao, walimuua mtu,
kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
7“Nalaani hasira yao maana ni kali mno,
na ghadhabu yao isiyo na huruma.
Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo,
nitawasambaza katika nchi ya Israeli.
8“Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu.
Adui zako utawakaba shingo;
na ndugu zako watainama mbele yako.
9“Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba
ambaye amepata mawindo yake akapanda juu.
Kama simba hujinyosha na kulala chini;
simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha?
10“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda,
wala bakora ya utawala miguuni pake,
mpaka atakapofika yule ambaye ni yake;49:10 yule ambaye ni yake: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
ambaye mataifa yatamtii.
11“Atafunga punda wake katika mzabibu
na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora.
Hufua nguo zake katika divai,
na mavazi yake katika divai nyekundu.
12“Macho yake ni mekundu kwa divai,
meno yake ni meupe kwa maziwa.
13“Zebuluni ataishi sehemu za pwani,
pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli.
Nchi yake itapakana na Sidoni.
14“Isakari ni kama punda mwenye nguvu,
ajilazaye kati ya mizigo yake.
15“Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,
na kwamba nchi ni ya kupendeza,
akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo,
akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.
16“Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,
kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
17“Atakuwa kama nyoka njiani,
nyoka mwenye sumu kando ya njia,
aumaye visigino vya farasi,
naye mpandafarasi huanguka chali.
18“Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe!
19“Gadi atashambuliwa na wanyanganyi,
lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia.
20“Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi,
naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.
21“Naftali ni kama paa aliye huru,
azaaye watoto walio wazuri.49:21 azaaye … wazuri: Au naye huimba nyimbo nzuri.
22“Yosefu ni kama mti uzaao,
mti uzaao kando ya chemchemi,
matawi yake hutanda ukutani.
23“Wapiga mishale walimshambulia vikali,
wakamtupia mishale na kumsumbua sana.
24“Lakini upinde wake bado imara,
na mikono yake imepewa nguvu,
kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,
kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli;
25“kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia,
kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki;
upate baraka za mvua toka juu mbinguni,
baraka za maji ya vilindi vilivyo chini,
baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
26Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele,
ziwe bora kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.
27“Benyamini ni mbwamwitu mkali;
asubuhi hula mawindo yake,
na jioni hugawa nyara.”
28Hayo ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hayo ndiyo maneno aliyowaambia baba yao alipowabariki, kila mmoja wao kama alivyostahili.

Kifo cha Yakobo

29Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti, 30kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. 31Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. 32Shamba hilo na pango lake lilinunuliwa kwa Wahiti.”
33Yakobo alipomaliza kuwausia wanawe, aliirudisha miguu yake kitandani, akatoa roho akajiunga na wazee wake.
Mwanzo49;1-33

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: