Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 6 March 2016

Natumai JumaPili ilikuwa njema;Happy Mother's Day..Burudani-Miriam Paul-Nipe Macho,Mvua ya Baraka......Wapendwa waungwana; Habari za siku nyingi,Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na mwaka huu mpya..
Tunamshukuru Mungu kwa yote,Mungu yu mwema sana..nimeadimika kidogo mambo ni mengi familia imeongezeka
basi na majukumu yameongezeka,Lakini Mungu yu pamoja nasi na tupo pamoja tena..
Natumaini jumapili ilikuwa/inaendelea vyema
turudishe utukufu wa Mungu muumba wa yote...
"Happy Mother's Day" kwa wamama wote, Mungu atupe hekima,Busara katika Malezi ya Watoto wetu..
Mungu pia awaguse wenzetu wanaohitaji watoto ,akawape furaha hii nao wakafurahi pamoja na wengine..
Pia akawape sawasawa na mapenzi yake..
kuna ambao hawana kabisa ,Mungu yu pamoja nanyi,
Kuna walionao wa jinsia moja kike/kiume ,Mungu anamakusudi yake.
Kuna walionao lakini hawawajali/wameterekeza.Mungu awaguse mkumbuke majukumu yenu...

1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:

2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?


 Neno La Leo;Methali 31:1-31

Mawaidha kwa mfalme
1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:
2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?
3Usimalize nguvu zako kwa wanawake,
usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
4Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai,
wala wakuu kutamani vileo.
5Wakinywa watasahau maagizo ya sheria,
na kuwanyima haki wenye taabu.
6Mpe kileo mtu anayekufa,
wape divai wale wenye huzuni tele;
7wanywe na kusahau umaskini wao,
wasikumbuke tena taabu yao.
8Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;
na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,
linda haki za maskini na fukara.
Mke mwema
10Mke mwema kweli, apatikana wapi?
Huyo ana thamani kuliko johari!
11Mumewe humwamini kwa moyo,
kwake atapata faida daima.
12Kamwe hamtendei mumewe mabaya,
bali humtendea mema maisha yake yote.
13Hutafuta sufu na kitani,
na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara:
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka kabla ya mapambazuko,
akaitayarishia jamaa yake chakula,
na kuwagawia kazi watumishi wake.
16Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,
na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
na kuiimarisha mikono yake.
18Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;
hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,
kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20Huufungua mkono wake kuwapa maskini,
hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,
maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22Hujitengenezea matandiko,
mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,
anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,
huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25Nguvu na heshima ndizo sifa zake,
hucheka afikiriapo wakati ujao.
26Hufungua kinywa kunena kwa hekima,
huwashauri wengine kwa wema.
27Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,
kamwe hakai bure hata kidogo.
28Watoto wake huamka na kumshukuru,
mumewe huimba sifa zake.
29Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,
lakini wewe umewashinda wote.”
30Madaha huhadaa na uzuri haufai,
bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.
31Jasho lake lastahili kulipwa,
shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.

                Bible Society of Tanzania
Jifunze zaidi

Mungu awabariki wote mliopita hapa,
muwe na wakati mwema.
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza kabisa napenda kusema HONGERA SANA KWA KUONGEZEKA KWA FAMILIA...Pili napenda kukukaribisha sana tena maana kwa kweli kama ulivyosema uliadimika kweli lakini matunda tumeyaona:-) Jumapili yangu imeishia mzigoni ndo nimerudi tu hapa. Ni furaha ilioje KACHIKI wa mimi ...karibu sana na mwisho ahsante sana kwa neno!

Rachel siwa Isaac said...

asante sana Kadala wa mimi..
Pamoja sana.