Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 2 November 2015

[PICHA]: MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC


Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC

Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi

 Wanafamilia Richard Mollel akisoma somo la kwanza

Janice Manse akisoma somo la pili
 Joseph Maro akisoma historia ya marehemu Gren Judica Moshi

 Julius Manase, akiongoza utaratibu wa ibada

Mchungaji Ferdnand Shideko akihubiri
 Wachungaji wakiombea familia

 Watoto wa Marehemu, Donald na James Moshi wakifuatilia Ibada

Wachungaji wakiongoza maombi kwa wanafamilia

 Andrew Mushi akitoa shukrani kwa niaba ya familia


No comments: