Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 22 February 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?‏


Photo: Mobile88.com

Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya
WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu
bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi
kifupi tu.

Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano
ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni
19 kununua WhatsApp.

Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Ila mimi najiuliza: Je inamaana sisi tusiotumia Whatsapp lakini tukiwa Facebook, tutaweza sasa kuwasiliana na wenye Whatsapp pitia kampyuta zetu kama hatuna sim za mkononi?

Rachel Siwa said...

Asante kaka Manyanya jee unajiuliza au...Unahitaji na Jibu kutoka kwa watumiaji?

Wapo watumiaji Wazuriiiiii sana humu..watakujibu/kusaidia tuu.