Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 26 July 2013

Wimbo Toka Kwa Neema Decoras Milele Nitalisifu Jina Lako!!!!



 Ndugu,

 Salamu katika Jina la Yesu Kristo,

 Ninaitwa Neema
 Decoras. Ni muimbaji wa Nyimbo za Injili toka Dar es Salaam, Tanzania.
 Nimeambatanisha wimbo wa kwanza kutoka katika albam yangu, uitwao Milele Nitalisifu Jina Lako na kuutuma kwako ili uusikilize.


 Mashairi ya wimbo huu ni haya yafuatayo:

Kibwagizo (Chorus)
 Milele, Milele, Milele eeee,
 Milele, Milele, Milele
 eeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Aaah,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,

 Beti 1
 Hakika Upendo wako, ooooh
 Nashindwa
 kuupima mimi,
 Ulinipenda mimi, iiiih,
 Ukatoa uhai wako,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na mateso,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na kuzimu,
Ukaja duniani, iiiih,
Ukapata mateso mengi,
Ulijishusha sana, aaaah,
 Ili utukomboe sisi,
 Mimi sijaona, aaaah
 Upendo kama wako tena
 Mimi sijaona, aaaah
Upendo kama wako tena
 Nasema, Milele, Milele Nitalisifu Jina Lako

 Kibwagizo
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
  Aaah,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,

 Beti 2
 Niwapo mashakani, iiiih
 Rafiki hunikimbia,
 Niwapo ni mgonjwa, aaaah
 Watu husema pole sana,
 Lakini hawawezi, iiiih
 Kutatua shida zangu,
 Lakini hawawezi, iiiih
 Kutatua shida zangu,
 Peke yako nakuona,
 aaaah
 Waja kunifariji moyo,
 Peke yako nakuona, aaaah
 Waja kutibu afya yangu,
 Peke yako nakuona, aaaah
 Wanitendea miujiza,
 Ndio maana nasema, aaaah
 Una upendo mwingi sana,
 Ndio maana nasema, aaaah
 Una upendo mwingi sana,

 Kibwagizo
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele, Milele, Milele eeeee,

Swahili Na Waswahili;Inakutakia kila lililojema,Baraka katika Yote.Hongera Sana da'Neema Decoras.

No comments: