Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 31 July 2013

Wazo La Leo;Kutoka Kwa da'Rose-MWANADAMU MWANADAMU MWANADAMU!!!!!!Mwanadamu yeyote anayeweza kuongea na wewe gizani, anayekupa ujumbe fulani kwakutumia jina la kivuli,mwanadamu aliyekosa ujasiri wakujidhihirisha kwenye mwanga, nazungumza na yule mwanadamu anayekufahamu,mwanadam ambaye kama ana neno na wewe anauwezo mkubwa wakukutafuta nakukwambia, mwanadamu ambaye anakuona kwenye mwanga yawezekana kila iitwapo leo lakini hakwambii, hana uhuru na mwanga, mwanadamu ambaye hawezi kutumia silaha zake  wakati akuonapo ila ukimpa nafasi ya giza kidogo anaitumia vizuri,mwanadamu asiyekuwa na ujasiri wakukutishia ila atakutishia gizani na ngurumo nyingi zenye vishindo.......mwanadam ambaye anakuthibitishia gizani kuwa yuko kazini na anaamini utaanguka na amekaa mkao wakusubiri uanguke duuuuu!!!!!(sina jina la kumpa ila mara jingine sidhani km anastahili kuitwa mwanadam) kwa maana nyingine niASKARI WA GIZANI....... 

walio wagizani hawaoni yaliyomwangani,na waliomwangani hawaoni yalio gizani....... wa gizani hata ukimwashia taa kwa jinsi yakibinadamu ataona, lakini kwa sababu yeye ni wagizani atatumia nguvu kujibadilisha ndani yake aendelee kuona giza, japo kuwa neema ya mwanga imemfikia (kwa mana nyingine hana neema yakutambua yaliyo  kwenye nuru)....na alie kwenye mwanga hata giza limpitie bado ataona mwanga tuu japokuwa kuna misukosuko,milima,mabondo, na mikasa ya kila namna bado ataona hicho ni kipindi tu.........JARIBU NI KAWAIDA YA MWANADAMU..............)


ninachoweza kusema ni hivi...... acha vita vya rohoni viwe vya rohoni, kuna wakati huyu mwanadamu (PEPO) anaweza kukupush ubinadamu ukuingie kwa namna fulani  USIJARIBU!!!!! Huo ni mlango mkubwa wa yeye kuingia kwa sababu utafanya uwanadamu usaidie kazi za rohoni  NI MWIKO MKUBWA KUSAIDIA KAZI ZA ROHONI............. ACHA KAZI ZA ROHONI ZIFANYIKE KIROHONI(VITA TULIVYONAVYO SI VYA DAMU NA NYAMA BALI..........................),( VAENI SILAHA ZOTE ZA VITA ILI.............) 

1 comment:

emu-three said...

Tupo pamoja mpendwa