Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 4 May 2013

Poleni Sana Familia Ya Costa Shirima!!!!!


Ulale kwa Amani Mpendwa wetu COSTA SHIRIMA.Pole  Sana Mke,Watoto,Wazazi,Ndugu,Jamaa na Mrafiki kwa Msiba huu wa Mpendwa wetu  COSTA SHIRIMA.Daima Tutakukumbuka na Kuenzi Mema yote uliyoyatenda.Familia ya ISAAC,Swahili NA Waswahili Blog Tupo Pamoja katika wakati huu Mgumu Kwenu.

Habari kamili,shukrani;http://mrokim.blogspot.co.uk/
MFANYA BIASHARA COSTA SHIRIMA ALIYEDONDOKA  GOROFANI KARIAKOO...



TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.


Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Poleni sana kwa msiba. .mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Mungu slitpa mungu amechukua.