Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 10 February 2013

Natumaini mlikuwa na J'Pili Tulivu..Pole kwa Wote waliopatwa na Msiba;Burudani - Ambassadors of Christ Choir Rwanda, Ni Kwanini? na Nyingine Nyingii!!!!

Wapendwa J'Pili ya Leo tuwaombee wenzetu waliopatwa na Misiba shida na Tabu..MUNGU awape Nguvu kwa wakati huu Mgumu kwenu..

Kuna mwenzetu Amefiwa na MUME na Mwingine Amefiwa na BABA yake Mdogo Na Wengine wote waliopoteza Wapendwa wao.....

Tumshukuru MUNGU  siku zote kwa ajili yenu  nyote,tukiwataja katika maombi yetu.

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Paulo Mtume kwa WATHESALONIKE:1:1-7
.Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika BWANA wetu YESU Kristo, mbele za MUNGU Baba yetu.....Endelea....

"Swahili NA Waswahili"
Mbarikiwe Sana.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ni matumaini yangu hata wewe na familia mmekuwa na jumapili murwaaa..mimi yangu naimalizia kubeba mabox:-)

emu-three said...

Tunapa pole sana waliofiwa na kuwaombea kwa mola awape subira, kwani hayo yote ni mapito, na sote tupo njia moja. Tupo pamoja mpendwa , NDUGU WA MIMI

EDNA said...

Mimi yangu imeisha kwa kufua ngua za wiki mbili na kufanya usafi lol...Hope ya kwako ilikuwa poa mdada wangu.

Rachel siwa Isaac said...

Asanteni sana wapendwa wangu.....nashukuru MUNGU ilikuwa salama na niliweza kwenda kuwafariji wengine!!