Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 9 December 2013

Mheshimiwa January Makamba akihutubia waTanzania DMV‏


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba alipohutubia waTanzania na jamii zao waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Laurel Maryland Desemba 7, 2013 kwa uratibu wa blog ya VIJIMAMBO


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 8 December 2013

Tumalizie J'Pili kwa Upendo na Amani;Burudani-Bonni Mwaitege,Fungua Moyo Wako na Nyingine!!!!

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii kwa Wema,Busara,Hekima,Amani,Unyenyekevu na Upendo..

Malaika wa BWANA hufanya kituo,Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.


Neno La Leo;Zaburi 34:1-12.
Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini
.





"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Friday 6 December 2013

RIP Nelson Mandela Dead at 95 - Hanson Baliruno New Ugandan



Dunia yaomboleza kifo cha Mandela;Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.

Habari Na;http://www.bbc.co.uk/swahili/

Thursday 5 December 2013

Jikoni Leo;How to Make Mabuyu na Vingine vingi Kutoka kwa-Sheikha Agil

Waungwana ni Jikoni Leo; Tuangalie Mapishi mbalimbali kutoka kwa da'Sheikha..
Mmmhh hakika sikuhizi kama wewe ni mpikaji na unataka kujifunza mapishi tofauti hakuna linaloshindikana.
Usitafute visingizio, Oohh mama nanihii nipikie oohhh sijafundishwa na mama/shangazi/dada,Nyumbani...


Pia kama unakinyaa,Hupendi kula chakula cha mtu usiyemjua/sehemu usiyoiamini usafi wake.Ingia Mitandaoni tuu kila kitu utapata  maelekezo yoote na upike mwenyewe...
Haya TEAM[Timu] Mapishi kazi kwenu............


Shukrani;Sheikha Agil

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 4 December 2013

HUYU NA YULE: Mahojiano na waTanzania Evans Mhando na Fatuma Matulanga wakiwa CHINA‏


WaTanzania Evans Mhando (L) na Fatuma Matulanga (M) walipokutana jijini Beijing nchini China. Wiki hii walikuwa wageni katika kipindi cha HUYU NA YULE kinachotayarishwa na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production

Katika huyu na yule wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa
wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga
aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja
tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana

Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo

1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA

2:TOFAUTI
KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi
ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?

3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?

4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?

5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?

6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)

Na mengine mengi

Ni
huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma
Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la
Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China


Kwa maoni ama ushauri, usisite kutuandikia kupitia jamiiproduction@gmail.com
--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Tuesday 3 December 2013

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Majukumu ya Baba katika Familia‏


Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production.

Katika kipindi cha wiki hii, mjadala wa WAJIBU WA BABA KATIKA FAMILIA umefungua mfululizo wetu wa mijadala kuhusu wajibu wa mzazi kwa familia yake

Mbali na washiriki waliokuwemo studio, pia tumeshirikisha maoni toka kwa wasikilizaji wetu wapendwa waliyotoa kwenye ukurasa wa Facebook
Msimamizi wa kipindi Abou Shatry akifuatilia mjadala

Karibu uungane nasi



Mjadala ukiendelea
Mgeni wetu katika mjadala huu Isidory Lyamuya


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Kifuatacho Jamii Production...Fatuma Matulanga na Evans Mhando‏



Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE  wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa
wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga
aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja
tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana

Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo

1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA

2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?

3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?

4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?

5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?

6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)

Na mengine mengi

Usikose kutembelea mtandao huu siku ya Jumatano ili kusikiliza mahojiano kamili

Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma
Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la
Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China

Monday 2 December 2013

[AUDIO]: Maandalizi ya matembezi ya hisani: NCHI YANGU, WAJIBU WANGU, TAIFA KWANZA‏


 Matukio Chuma, muandaaji wa matembezi ya hisani akizungumzia matembezi hayo yatakayofanyika Januari 11, 2014 yenye kauli mbiu Nchi yangu, wajibu wangu, taifa kwanza.

Katika mahojiano haya Chuma anazungumzia mambo mbalimbali kuhusu matembezi hayo, ikiwemo sababu ya kuyaandaa, sababu za kuyafanya katika njia waliyoamua kuyafanya (Dar-Moro), mambo ya kufanya kabla hujashiriki matembezi haya na mengine mengi.

Unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0784 311-056, 0772 545-562 ama barua pepe ambayo ni kwetutanzania@yahoo.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 1 December 2013

Nawatakia J'Pili Njema yenye Baraka;Burudani-Bahati Bukuku,Naomba niulize na Nyingine!!!

Wapendwa muwe na J'Pili Njema yenye,Shukrani,Imani,Upendo na Furaha...
Ninyi ni chumvi ya dunia,lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?
Neno La Leo;Mathayo Mtakatifu:5:11-16.
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye Mbinguni.








"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday 30 November 2013

[AUDIO]: Kuzagaa kwa silaha za moto na kuongezeka kwa mauaji Tanzania‏


Picha kwa hisani ya thehabari.com
Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu.

Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake .

Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.


Ungana
na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia
tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya
waTanzania wengi.



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Wednesday 27 November 2013

Jikoni Leo;[Street food]Chipsi Vumbi Na Hapa kwetu!!!!!!!


Hapa tunapokumbukia Chipsi za Nyumbani, Ma binti zangu hupenda sana Chipsi Mayai[ZEGE]Na sasa wanapika wenyewe kama unavyoona hapo juu,Nyama Choma Baba anawasaidia...

Waungwana;Jikoni Leo Mtaani na Kwa Da'Rachel..
Vipi Chipsi Vumbi/za Mitaani Zina Raha gani? Na Karaha Gani?

Kuna mtu hajawahi kula Chipsi hizi?

Jee wewe uliyekula/Unayekula Wapi KIJIWE bomba Cha Chipsi upendacho?

Pale Dar,Ilala  Kulikuwa kwa Ndago,Barafaa....
Pale Iringa,Kulikuwa kwa Baba Nusa...


Hizi ni Chache tuu nawe Waweza Kuongezea....





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Monday 25 November 2013

Sunday 24 November 2013

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Here I am to Worship[Playlist]!!!!

Wapendwa;Muwe Na J'Pili yenye Baraka,Amani,Upendo na Furaha...
Lakini nafsini mwangu nalikusudia hivi,nisije kwenu tena kwa huzuni...
.Maana mimi nikiwatia huzuni,basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishwaye nami?
Neno La Leo;2Wakorintho:2:1-11.


"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday 23 November 2013

Wa-Africa Na Mitindo Mchanganyiko!!!!!





Mhhhh..Mengi sina..ni Wa-Afrika na Mitindo...mimi naiita Mitindo TATA..
Vipi Inavalika? Si wanasema Wanawake tunavaa mavazi yanayo fanana na Yao..nawao jee?......haya na Nywele za dada kama hivyo.

Kuona Zaidi nifuate;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Miaka 50 tangu kuuawa kwa Rais John F Kennedy‏



 

Ijumaa wiki hii,
Marekani imeadhimisha nusu karne tangu kuuawa kwa Rais wa 35 wa taifa
hilo, John F Kennedy aliyeuawa Novemba 22, 1963 alipokuwa akisafiri kwenye gari la wazi jijini Dallas

Rais John F Kennedy akiwa katika gari la wazi muda mchache kabla hajauawa kwa risasi. Pembeni yake ni mkewe na mbele yake ni aliyekuwa Gavana wa Texas John Bowden Connally, Jr.ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo
Kwa wiki nzima, kumekuwa na shughuli mbalimbali kukumbuka tukio hili lililoshitua wengi nchini humo. Mambo mengi yametendeka. Vitabu vipya vimeandikwa na watu wamezungumzia kuuawa kwa Rais huyo pamoja na ufuasi alioacha kwenye uongozi mpaka sasa. Na kama ilivyotegemewa, Kengele ziligongwa, maua yaliwekwa kwenye kaburi, bendera zilipepea nusu mlingoti na nyimbo mbalimbali ziliimbwa

Rais Barak Obama, aliadhimisha kumbukumbu
hizo Jumatano wiki hii kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais
Kennedy na pia kutoa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali akiwemo Rais
mstaafu Bill Clinton, mwanahabari maarufu Oprah Winfrey na wengine 14.

Rais Barack Obama (wa pili kulia) akiwa na mkewe Michelle, Rais mstaafu Bill Clinton (wa tatu kulia) na mkewe Hillary Clinton wakitoa heshima mbele ya kaburi la JFK jumatano wiki hii.


Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 23, 2013




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Friday 22 November 2013

Jikoni Leo;African Market-Nima Market in Accra, Ghana!!!!




Waungwana;Jikoni Leo, Tupo sokoni  Ghana..haya tuangalie mahitahi...
Kuna vingine wewe huviwezi kula lakini wengine wanaweza.

Nini kimekuvutia?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday 20 November 2013

Ana kwa Ana na Astronaut Dr Donald Thomas‏


Karibu katika mahojiano kamili na Dr Donald Thomas.

Mhandisi na mwanaanga wa Marekani

 Katika mahojiano haya, Dr Thomas anaeleza historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi.

Ilimchukua miaka 9 tangu ajaribu kwa mara ya kwanza mpaka achaguliwe, na katika miaka hiyo, alituma maombi mara nne.

Ili kuongeza nafasi yake kufanikiwa akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo.

Lakini aliamini katika atendalo.

Pia ameeleza maandalizi wanayofanya na mafunzo wanayopitia kuanzia wanapochaguliwa mpaka
wanapoenda kwenye mission hizo, hisia na uoga wake siku ya kwanza alipanda
space shuttle. Amezungumzia safari nzima na shughuli kuanzia
wanavyoondoka mpaka wanavyofika angani pamoja na changamoto za kuishi kwenye
orbit. Kuanzia kupika mpaka kutumia choo. Na pia, namna alivyopokea taarifa za
kulipuka kwa space shuttle Columbia. Shuttle aliyoitumia mara tatu kati ya nne
alizokwenda kwenye orbit.

Baada ya miaka 20 aliyofanya kazi kama mwanasayansi wa NASA, na safari nne kwenye Orbit, akastaafu na sasa ni Mkurugenzi wa Willard Hackerman Academy katika chuo kikuu cha Towson hapa Maryland ambapo anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho

Nilipata fursa ya kuhojiana naye mwaka 2011




Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Monday 18 November 2013

Kipindi Maalum Mazishi ya Bi.Martha Shani Tanzania




Tunawaletea kipindi maalum cha Mazishi ya mpendwa na kipenzi chetu Bi. Martha Shani aliyefariki ghafla nchini Marekani na kuja Kuzikwa nyumbani Tanzania. Katika Kipindi hiki utaona matukio mbalimbali katika safari ya mwisho ya Bi. Martha Shani.

"Swahili Na Waswahili";Mhhh...Pole sana kaka Alex,  Familia,Ndugu,Jamaa na Marafiki.

Ulale kwa Amani da'Martha Shani.


Dr Donald Thomas alipohojiwa na Jamii Production‏


Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE, wiki hii utasikia mahojiano niliyowahi kufanya na Dr Donald Thomas. Mhandisi na mwanaanga wa Marekani.

 Ilimchukua miaka 33 kutimiza ndoto zake za kuelekea kwenye Orbit. Na baada ya kwenda kwenye Orbit mara nne, akastaafu na sasa anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho

Nilipata fursa ya kuhojiana naye ambapo alieleza mengi mema



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 17 November 2013

Tumalizie J'Pili hii Vyema;Burudani-Kutoka,One Nation Gospel Na Gisubizo Choir!!!


Tumalizie J'Pili hii vyema.. Iwe Yenye Neema,Baraka,Upendo na Amani....BWANA asipojenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.........

Neno La Leo;Zaburi:127:1-5





"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana

Saturday 16 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Hatari ya bunduki za kuchapishwa nchini Marekani‏





Bunduki ya plastiki iliyotengenezwa kwa mashine ya 3D ikifyatua risasi wakaati wa majaribio

Photo credits: Screenshot from ATF Video


Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.



Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.

Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha.

Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.


Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)



Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC

Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 16, 2013



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Friday 15 November 2013

Wanawake Na Mitindo Ya Nywele!!!!

Waungwana;Wanawake na Mitindo Ya Nywele...
Hivi ni kweli Nywele ndiyo pambo kubwa kwa Mwanamke?
Kujua/Kuona Zaidi nifuate huku;
http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday 14 November 2013

HUYU NA YULE: Mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.‏


Katika kipengele cha HUYU NA YULE, wiki hii tuliungana na VIJANA WATATU


Liberatus Mwang'ombe, Peter Walden na Ally Badawy kujadili MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.


Ali Badawi (kushoto), Peter Walden (kati(na Liberatus Mwang'ombe (kulia) wakiendelea na mjadala ndani ya studio za Jamii Production

Ulikuwa ni mjadala mrefu na huru ambao ulikuwa na mengi ya kufunzana


Karibu uungane nasi


Wakati tukimalizia mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE, Peter Walden alimuuliza Liberatus Mwang'ombe swali kuhusu kufunguliwa kwa matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi.

Liberatus ni Katibu Mkuu wa Tawi la Chadema hapa Washington DC

Hapo pakawa na ka-mjadala kadoooogo ambako hata Ally Badawy na mwongozaji wa kipindi Mubelwa Bandio wakachangia.

Karibu usikilize



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Tuesday 12 November 2013

Mahojiano na mwanamuziki Dekula Kahanga a.k.a Vumbi‏


Hivi karibuni Jamii Production ilipata nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu katika ucharazaji gitaa nchini Tanzania Dekula Kahanga aliye maarufu kwa jina la Vumbi.
Mahojiano haya "mepesi" yamegusa mambo mbalimbali kuhusu maisha yake kimuziki
Amehojiana na Jamii Production akiwa Sweden yalipo makazi yake ya sasa
KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 10 November 2013

Muendelee na J'Pili hii Vyema;Burudani Mchanganyiko-Hear My Cry Oh Lord,Blessed be the Name of the LORD,Na....!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu  J'Pili inaendeleavyema...
MUNGU ni Pendo.Mimi nakupenda sana wewe uliyepita hapa/Unayepita hapa na Woooote....Muwe na Amani,Furaha na Upendo wa kweli...
Wapenzi na Mpendane;kwakuwa pendo latoka kwa MUNGU, na kila apendaye amezaliwa na MUNGU,naye anamjua MUNGU.

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Yohana:4:7-21











"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Saturday 9 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Athari za vita baada ya kumalizika mapigano‏


Wakati vita ya Congo
ikionekana kuelekea ukingoni, bado tunakumbushwa kuwa athari za vita
katika nchi mbalimbali huendelea kuwaathiri wahusika na hasa wananchi wa
nchi hizo kwa miaka mingi baada ya kumalizika kwa vita hivyo.

Baadhi
ya athari huwa wazi sana. Mfano ni majengo yaliyoharibika wakati wa
mapigano, watu wanaouawa wakati wa mapigano na hata uchumi unaozorota
kutokana na watu kutofanya kazi wakati wa mapigano hayo.

Lakini pia kuna athari ambazo hazionekani ama kutopewa kipaumbele machoni mwa watu wengi baada ya vita hivyo.

Hivi karibuni, waMarekani wamekumbushwa kuhusu hili

Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).



Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 9, 2013



*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

"MISUKOSUKO" KUTOKA KWA NDEGE 3


Jina la Nyimbo ni MISUKOSUKO.
Jina la kundi  ni NDEGE 3
Waimbaji ni Khadija Mnoga (Kimobitel) , Paulyne Zongo na Joan Matovolwa tumefanya featuring na Grayson Semsekwa.

  Audio imeshatoka na sasa VIDEO.




Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joana Matovolwa.Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo linalojulikana kwa jina la NDEGE 3

Friday 8 November 2013

Mapenzi Na Wapenzi; [Love Story]Jee Ulimpata wapi huyo Mwenza wako?


Waungwana;Safari ya maisha huanzia mbali sana mpaka watu Kuchumbiana na  wakaamua Kufunga Ndoa/kuishi Pamoja kama Mke na Mume..Pia kila mtu/watu wanapo walipoanzia.
 Jee wewe ulianzia wapi?
 Hahahah..huyo Mchumba wako,Mkeo/Mumeo ulimtoa/Muona/kutana naye wapi?...
Ulitafutiwa,Mlikutana Njiani,kwenye basi,kazini,Chuoni au....?
Jee Unaushauri gani kwa wanaotafuta Wenza/Wachumba/Mke-Mume?






"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Tuesday 5 November 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Dj Luke Joe‏


Dj Luke akiwa studio na Mubelwa Bandio wa Jamii Production
Karibu katika mahojiano na Dj mkongwe kutoka Tanzania na
mmiliki wa blog ya Vijimambo Lucas Mkami a.k.a Dj Luke Joe


Dj Luke ambaye makazi yake kwa sasa ni Maryland nchini Marekani ameeleza mengi kuhusu kazi zake hizi.

Katika mahojiano haya, ameeleza historia yake katika kuchezesha muziki, aliyemvutia kuingia katika kazi ya uDj, mafanikio ya Dj, changamoto zake, ku-blogu na mengine mengi.


Karibu Uuungane nasi



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Monday 4 November 2013

Kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production......FAMILIA ZA KAMBO (sehemu ya mwisho)‏





Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema
Moja ya sababu zilizotusukuma kujadili masuala kuhusu FAMILIA ZA KAMBO ni takwimu zilizopo hivi sasa kuhusu familia hizi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.blendedandbonded.com, hapa Marekani
• 41% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka
• 60% ya ndoa za pili huishia kwenye talaka
• 73% ya ndoa za tatu huishia kwenye talaka
• 45% ya wanawake na 50% ya wanaume wataoa tena ndani ya miaka mitano ijayo
• 50% ya ndoa za marudio huhusisha watoto wa mahusiano yaliyopita walio chini ya miaka 18
•Ndoa 2100 huanzishwa kila siku nchini Marekani
• 42% ya watu wazima wana uhusiano wa kambo. Hii inajumuisha mzazi wa kambo / mtoto wa kambo ama ndugu wa kambo
Kwa idadi ya Marekani, takwimu hizi zinamaanisha kuwa familia za kufikia zinahusisha watu wazima wapatao milioni 95.5
•Kuna baba wa kambo milioni 16.5
•Kuna Mama wa kambo milioni 14.
•Wataalamu
wa mahusiano wanasema kuwa ndoa za kufikia ndio zitakuwa ndoa zenye
umaarufu na nyingi zaidi nchini Marekani na kuwa, kutokana na kukosekana
kwa taarifa sahihi kuhusu familia za kufikia, familia hizi mara nyingi
zimejikuta kwenye migogoro na mafarakano.
Nasi tuko hapa kujaribu kuepusha hilo kwa kushirikiana nanyi katika kile tunachoweza kuelimisha kudumisha ndoa hizo.
Ungana nasi katika sehemu hii ya mwisho ya MADA hii.




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 3 November 2013

Nawatakia J'Pili Njema yenye Amani;Burudani-bado tupo ,Kijitonyama Choir,Ee Baba,Jehova Baba wa Upendo na...!!!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili hii iwe njema..Na usikate tamaa MUNGU yupo na Anatenda/Ametenda/Atatendaaa.. Jehova Baba wa Upendo..Eeee Baba kama si wewe Ningekuwa/Tungekuwa/Ungekuwa Wapi?...Mhhh Acheni MUNGU aitwe MUNGU Bwaana!!!!!

Watulizeni mioyo,Watulizeni mioyo,Watu wangu asema MUNGU wetu....
Neno La Leo;Isaya:40:1-31;

Bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio,wala hawata choka;watakwenda kwa miguu,wala hawatazimia.






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Saaana.

Saturday 2 November 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Oliver N'goma-Bane na Nyimgine..!!!






Waungwana "Chaguo La Mswahili Leo" Ni Oliver N'goma...
Mhh..wewe unakumbuka wapi na ilikuwaje/ulikuwa wapi wakati huo?
Maneno Meengi sina nasikiliza kutoka kwako..

Twende Sote sasaaa......





Swahili Na Waswahili Pamoja Sana.

Wednesday 30 October 2013

Tanzania: Tunaweza kujitoa A. Mashariki

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Taarifa zinazohusiana
Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.
Habari kutoka;http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Tuesday 29 October 2013

JAMII PRODUCTION YAZINDULIWA RASMI‏ !!




Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano mafupi aliyofanya na Jamii Production kabla ya KUZINDUA RASMI shughuli za kutayarisha na kusambaza matangazo ya Radio na Video.



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa na waanzilishi wa Jamii Production, Mubelwa Bandio (kulia) na Abou Shatry (kushoto)

Naam....
Kwa baraka za Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara, JAMII RASMI IMEZINDULIWA RASMI Oktoba 26, 2013,
alipotutembelea kuangalia utendaji wetu na kuizindua rasmi hapa ofisini
kwetu Washington DC.
Hii ilikuwa ni ZAIDI YA TUKIO.
Ilikuwa ni BARAKA KWETU na tunamshukuru kila aliyewezesha hili.
NA SASA.....
Kazi ya kutekeleza yale yaliyousiwa na Mhe Waziri, yaliyo yaliyo msingi
wa kituo chetu, yale yaliyo MAHITAJI ya walaji (hadhira yetu) NA WAJIBU
WA FANI YETU ndio imeanza.
Na......
Hakuna litajalokuwa na maana kama hatutajua namna ambavyo utendaji wetu unaathiri maisha yako kwa namna CHANYA na HASI
Wewe (msikilizaji, mtazamaji na msomaji wetu) ni mdau mkubwa wa kufanikisha hili.
Tuzidi kushirikiana
TWAWAPENDA



Msimamizi wa vipindi na mpigapicha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry akisisitiza jambo kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi


Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA Georgina Lema akiwa "kitini"


Mmoja wa wawezeshaji wakuu wa Jamii Production Bwn Isidory Lyamuya wa Prestige Health Services akijaribu vitendea kazi vya kituo


Mhe. Waziri Mukangara akipokea maelezo ya utendaji wa kituo. Kushoto ni Afisa Ubalozi Mindi Kasiga

 
Mhe. Waziri akisikiliza RISALA ya Jamii Production 



 Mhe. Waziri Mukangara akijibu risala ya Jamii Production


Bwn Isidory Lyamuya akipata akipata picha ya pamoja na Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production



Bwn Isidory Lyamuya akipata mkono wa pongezi toka kwa Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production

Abou Shatry akipongezwa na Mhe Waziri Mukangara


"Mwanamama" Georgina Lema wa kipindi cha FAMILIA akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri


 Mkurugenzi wa Mambo Jambo Radio Bwn Julius Makiri ambaye aliungana nasi katika uzinduzi huu rasmi akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri



 Mhe. Waziri Dkt Fenella Mukangara na Afisa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mindi Kasiga pamoja na wanaJAMII

 


Hakuna ZAWADI kubwa sawa na kilichofanyika. Na zawadi pekee tuliyonayo ni UPENDO. Ambao hauonyesheki wala haupimiki.

Lakini....tunapenda POPOTE UWAPO, UKUMBUKE SIKU YA LEO.
Na hivyo..twaomba KIKOMBE hiki kiwe kumbukumbu ya tukio hili kubwa kwetu

Abou Shatry akiwa mahala anapopatawala zaidi...


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"