Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 26 September 2012

WASAMARIA WEMA POPOTE DUNIANI TUNAOMBA MSAADA WAKO KUSAIDIA KUOKOA MAISHA YA MTOTO JULIANA MWINUKA !!!!!

Samahani kwa Picha..
Mtoto Juliana Mwinuka mkazi wa kijiji Cha Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe anaendelea na matibabu katika Hospitali ya CCBRT wodi la wagonjwa wa Macho mtandao huu www.francisgodwin.blogspot.com unaendelea kuwashukuru wote wanaoendelea kutoa michango yao kunusuru uhai wa mtoto Juliana ambaye ni yatima


Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin

Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi.

Kwa Maelezo Zaidi waweza kuwasiliana na; http://www.francisgodwin.blogspot.co.uk/
Pamoja Tunaweza..Asante sana.




No comments: