Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 14 May 2012

Wanawake na Urembo;Ya kale ni Dhahabu!!!Burudani-Rangi ya Chungwa,Pamelah!!

Mrembo wa enzi hizooooo
Nipe siri ya urembo huu


Waungwa Leo nimewaletea Mrembo wa zamani kidogo,lakini mimi kwangu bado wananibamba sana.
Angalia hajajichubua,Hana makoroooombwezo meengi,Shedo za kuwaaakaa,Jee Hajapendeza?

Na sasa naona kama vimitindo tindo vya zamani  vinarudi, Sijui kukosa ubunifu, Ya metushinda au kukumbukia Enzi?

Huyu yeye hakuweka dawa Nywele wala kusuka,Lakini wapo pia wazamani waliokuwa wakisuka,Nywele za Uzi,Rafya,Jicho la mke wenza,Kilimanjaro, walibana Mchicha, waliweka Zazuuu, wali roli , Waliweka Kan'ta, Walifunga Vilemba  na..... duuuh nimengi nao Walikuwemo sana tuu.

Jee kunachochote cha Mitindo ya Zamani wewe bado Unapenda au Kukumbuka? na nini Kimekugusa/Kuvuti,  kwa huyu Mrembo?
Unapicha za BABA/MAMA za Wakati huo wakiwa Vijana na Unapenda Tujifunze Mitindi yao?

Usiwe na Tabu Unaweza kututumia Kupitia email.rasca@hotmail.co.uk

Karibuni sana Waungwa!!!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Safi sana mimi napenda sana kuwa hivyo labda niseme mimi wa zamai nini? LOL Ila uwongo mbaya haya makolombwezo tuyatumiayo tunajiwekea sumu tu mwilini ...nimependa huuu wimbo wa Pamela Ahsante kwa zilipendwa

Mija Shija Sayi said...

Natamani ungeweka na picha yake ya sasa... Pleeeeeeeease kama unayo..

Anonymous said...

Nimeupenda uzuri wa asili jamani mweee, yaani uzuri katurisisha wanae ngoja tujifagilie da Rachel hahaha alafu Mwenyezi Mungu kamjalia udongo mzuri mpaka leo ukiambiwa umri wake unajiuliza mara mbili mbili kweli?
Napicha zimenoga na zilipendwa kikwetu tunasema wakondiya (asandi)

emuthree said...

Uzuri wa asili dhahabu.
Kuutunza kwake ni adhabu,
Umenenwa hata kwenye vitabu,
Kudumu kwake ni aghalabu.

Ni hayo ndugu wa mimi. Tupo pamoja

Mtani said...

Halafu wewe Kachiki Muke ya Mubena una kesi kubwa sana, ili kumaliza hii kesi inabidi utafute jogoo mwenye manyoa ya rangi ya kijani na pishi moja la mchele!

Rachel Siwa said...

Asante sana Waungwana@da'Yasinta hhaha tnajiwekea sumu.......burudika na Pamelah.

@da'Mija nitatafuta na kuweka, hapa sina mpk nyumbani.

@Anony: hahah tuwekee picha hapa jamani tufananishe,hahahah sande mwana Wesu!!.

@Ndugu wa mimi wewe kiboko naona hata Mashairi yanapanda!!Pamoja sana sana!!.

@Mtani hahahhaha uwiiiii, umesikia Ngorooo hiyoo,Jamani Jogoo utapata lakini Mchele mpk niagize Pawaga au Mbeya, kama Mahindi na Ulanzi nitatoa sasa hivi,

Karibu sana Mtani.