Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 11 May 2012

Wanawake na Shughuli;Burudani-Bembeleza,Pii pii!!!!


mwanamke akifanya vitu vyake.Picha kwa hisani ya da'Jane Siame wa http://j2wisdom.blogspot.co.uk


Waungwana  natumai wote Hamjambo.

"Wanake na Shughuli " Kumekuwa na Shughuli nyiingi sana zinazohusishwa wanawake tuu.Jee Wanaume Hampendi/Hawapendi Shughuli/kujichanganya peke yenu/Yao?


Au sisi Wanawake ndiyo haswaa tunatakiwa kujichanganya,kufurahi,kukutana wenyewe?


Na jee kwanini tunapoalikana hizo shughuli tunaambiana kuwa ni ya "WANAWAKE TUU" Sasa basi ukienda huko unakuta Dj,Mchukua matukio, Mara kaka,Mjomba kaja na mengine meeengi yanafanywa na "WANAUME".Jee kweli wanawake wa leo hakuna wakutosha kufanya hizo kazi?
Je na hawa MASHOGA  Tumeshawaweka kwenye kundi Letu?

Vipi unapoaga Nyumbani kwa baba Ngina[mume] unaenda kwenye Shughuli za Wanawake tuu, nae anakupeleka na kuishia mlangoni anarudi Nyumbani.
 Akikufuata anakutana na Wanaume kibao wanatoka humo kwa Shughuli jee hii imekaaje?


Mpenzi Msomaji wewe una Mawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?


Karibuni sana Tuelimishane  Kwa Upendo!!!!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli kwa mimi kama mimi shughuli niionayo ya mwanamke ni ile ya kuzaa watoto tu. Nyongine zote hata wanaume wanaweza ila tu ule ubabe umeshamiri mno. Ruksa kuwa kinyuma.

Anonymous said...

Nianze kwa kutanguliza shukrani zangu kwako dada kwa kutuwekea hii mada, jamani jamani mimi binafsi huwa sielewi kabisa maana ya kuita shuhuli ya wanawake na mijibaba ukaikuta,na mara nyingi huwa inatokana na kuwa na upungufu wa kuaminiana kwa watu hasa waandaazi wa shuhuli jamani kitu cha kina mama ni cha kina mama wa mama twaweza kufanya kila kitu wenyewe, ushauri wangu kabla ya kuandaa shuhuli na kuipa jina ni ya kina mama tafuta wamama wenye fani tofauti ukisha wapata basi ita ya wa mama ukikosa basi tafuta jina ila msialike watu kuwa shuhuli ni ya wa mama kumbe na wa baba watakuwepo hayo ndiyo yangu

Mija Shija Sayi said...

Nakubaliana na Anony hapo juu..

Interestedtips said...

anony hapo juu kafafanua vizuri sana