Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 26 July 2011

Kaka Joel Ahitimu!!!!!!!!!

                          Kaka Joel mwenye Furaha.
                                 Duhh sitakuwa nao tena rafiki zangu,hii sasa mbaya kwangu!
                        Dada Jolen akimpongeza kaka.
               Nimeshakuwa mwanakijiji sasa!


Kaka Joel Amehitimu Nursery tayari kwa kuanza/kuingia Reception hapo September.
Joel!! Baba na Mama pamoja na Familia ya Mwasanjala na Shushu,Wanakutakia kila lililo jema katika safari yako ya kutafuta Elimu.


Rafiki[dada] yako kipenzi Tracey anakutakia mema katika masomo yako!


Nasi SwahilinaWaswahili tunakuombea Mungu awe pamoja nawe katika yote.


Mpendwa wewe ulipitia VIDUDU/Nursery?...Je unakumbukumbu gani katika hayo ni Uji,Nyimbo,Kulialia,Ulikutana na watoto Wababe au wewe ndiyo ulikuwa Mbabe!!!!!!


Karibuni sana Waungwana katika Yote!!!!!!!!

6 comments:

SIMON KITURURU said...

Hongera joel!

Goodman Manyanya Phiri said...

Vibaya namna hiyo, Kaka Joel. Ungekaa afadhali mwaka mmoja zaidi shuleni ya vidudu ili mwondoke wote na huyo mdogo wako. Sasa nani atamtetea huko shuleni?

Mimi sikupongezi! (LOL!)

Anonymous said...

hongera kaka J, nakutakia kila la heri

Swahili na Waswahili said...

Asanteni wote kwa niaba ya kaka Joel,
@kaka Manyanya hahhahahahaanamwacha mdogo wake huko wababe watamdunda!.

Mija Shija Sayi said...

Hicho mkononi ndo cheti nini? Naona kimekunjwa kwa nidhamu...

Swahili na Waswahili said...

Kama ndiyo cheti dakika 3 nyingi, wazazi wakijigeuza tuu kimeshachanwa,
maana huyu karithi utundu wa KISUKUMA!!!Hahahahahahaha.