Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 21 March 2011

Wanaume na Mitindo!!!!!!!!!!!

Leo sina la kusema wapendwa!!! Naicha hii mada mikononi mwenu!! Inaweza kuwa nzuri kwako/mbaya kwa mwenzio.Je wewe Mwanamke/dada unapenda Mumeo aweke vipi Nywele zake au atoke vipi?Haya na Wanaume jee ukiwananywele zipi au mtindo gani  unajiona ukobomba?  Karibuni waungwana ,Raha jipe mwenyewe au?.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaaaazi kwelikweli!!! Haya wanaume semeni hapa...

SIMON KITURURU said...

Nafikiri MITINDO hutegemea tu na kichwa cha MTU na bila kusahau utamaduni na jamii atokayo mtu.

Kupendeza , UZURI na vitu vingi kama hivyo mimi ukiniuliza -ntakuambia ni vitu BINADAMU anavyojifunza tu kutokana na mazingira aishipo , jamii inayo mzunguka nk.

Ukikulia Umasaini - kwa DUME kutoboa masikio na kusuka nywele haitakushangaza na wala DEMU kukata kipara cha wembe haitakufanya ufikirie KAFIWA.


Na swala sio mitindo ya nywele tu

Kwa mfano .

Ukiwa MUAFRIKA uliyekulia AFRIKA sehemu zenye uhaba wa MISOSI ni rahisi kujifunza kuona VIBONGE wanavutia kuliko vimbaumbau wembamba hasa kutokana na ukweli kunenepa bado ni DILI Afrika hasa maeneo yenye misosi haba .

Na ukikulia ULAYA maeneo ambayo misosi ni kibao unaweza kukuta ujanja ni kujikondesha kwa kuwa kilicho rahisi ni kujinenepesha na watu ladha ya urembo huipata zaidi kwa wawaonao ni wajanja kwa kuweza kuwa wembamba na kujizuia kula vyakula vilivyowazunguka kila mahali ambavyo vingeweza kuwanenepesha.


Na mitindo mara nyingi ni STATEMENT za watu pia hata bila kuongea.


Kwa hiyo katika maeneo ambayo WALOKOLE wa KIUME hukata VIPARA unaweza kukuta atakaye kujitofautisha nao akaamua asuke mabutu nywele . Na kusuka kwake mabutu ni sawa nakuiambia JAMII mimi tofauti na sio MLOKOLE ingawa pia sio NUNDA kwa kuwa manunda wana RASTA.


Pia kumbuka kuna watu huwa hawaridhiki tu na walichonacho. Kwa hiyo wenye nywele za kipilipili utakuta wanataka wazipige pasi ziwe nyororo na wenye nywele ndefu nyororo nao wanataka nyingine. Mablondi wakizungu wanataka nywele nyeusi na Wazungu wenye nywele nyeusi wanaziblichi ziwe nyeupe.

Ndio unaweza kukuta kila mtu anavutiwa na staili za wengine ingawa na wengine labda watamanicho ni kuweza kuwa na staili za wazikimbiazo kama tuonavyo:


Waafrika wenye kipilipili wanajaribu kuzipiga pasi nywele zao zinyooke. Na wenye zilizo nyooka wanajaribu kuzifanya zisinyooke.

Ila pia . Asilimia kubwa ya WATU staili na mitindo yao kama wangekuwa HURU kutoka kwenye PRESSURE za jamii wasingekuwa nazo hizo.

Kuna wapendao RASTA , kukata KIPARA au hata kusuka twende kilioni ambao huwezi kamwe kuwakuta na staili hiyo kwa kuwa kwanza ni jambo litakalo wagombanisha na WAZAZI , jamii au hata kuharibu nafasi zao za kuajiriwa.

Kwa hiyo MITINDO ni kitu kinachoathiriwa na mengi. Na staili na mtindo wowote ule ukiwanao kumbuka

``KUNAWATAKAO UPENDA na kutakaouchukia na wote hao maamuzi ya kuufagilia au kuukandia yametokana tu na katika ukuaji wao walijifunza nini kuhusu MTINDO murua na UZURI wa kitu ni upi!:-(


Pia kumbuka DUME lililokaa kidume kisawasawa kimtazamo waaliyejifunza DUME limekaaje,..
... hata aweke mtindo wa nywele utambulikanao katika jamii kama wa kike bado atatoka kidume. Ingawa kama ni DUME na ukisuka unatoka kidemu usitulalamikie tu MIDUME mingine ikianza kukutamani na kukuomba angalau tako.:-(


Ni mtazamo tu.

Swahili na Waswahili said...

Nafikiri hapa @kaka Kitururu wengi wanatamani mitindo lakini jamii/familiya inawabana,

pia anaweza akawa na kichwa cha mtindo atakao lakini akihofu jamii.

baadhi ya wazazi/walezi mitindo wanayopenda wao ndivyo watakavyo na vijana wao wafuate.

Swali Mzee kitururu alishawahi kukushauri kale kamtindo kake ka weyi?.

@Da Yasinta jamani nawe unahusika dada yangu si tunaye mtoto wa kiume hapo nyumbani je niwewe/baba ndiyo mnamuamulia mtindo wake?.

mimi nakumbuka kuna siku baba yetu alimpeleka kaka kunyoa kwakinyozi wa mwembeni,wakamnyoa mtindo unaitwa Denge weee kurudi nyumbani kuangalia hilo DENGE wacha aliye!!!!!.

EDNA said...

Mmmmh,mitindo ya nywele mie nafikiri huendana na Umri wa mtu...kuna umri fulani ukifika utakuta mtu anajistukia na´kuona hiyo staili ya nywele haiendani na umri wake.

Mija Shija Sayi said...

Mimi napenda Dreadrocks kwa mume wangu., Mwenzetu Rachel unapendaje?

Mcharia said...

Japo kuwa nilizikata DREADROCKS zangu 2004 hata hivyo mazingira ndio yaliyosababisha...ajira bwana.

Sikuwa na njia mbadala maana hali nayo ya kimaisha ilitaka kuleta zengwe kumbe kwenye taasisi ya dini kulikuwa na nafasi ya ajira ambayo ilihitaji mtu kama mimi yaani kumbe ni mimi niliyekuwa nahitajika pale.

KAMA NI WEWE UNGEFANYEJE??
DREADROCKS nazipenda sana, ila ninazo kiroho sio kimwili. I wish hata atakaye kuwa my wife awe na DREADROCKS.

Swahili na Waswahili said...

Da Mija mimi napenda anyoe nywele zote lakini zibaki kama zinaopta hivi si kipara[zungu].

@kaka Mcharia ningefata masharti tuu maana kazi zenyewe bongo nazijua kaka yangu!lakini ipo siku utakuwa nazo tuu!
nadhani bongo labda ukijialiri ndiyo unakuwa huru!.Na utampata mwenza mwenye nazo ili roho yako ipate powa!.

Na wewe umayesoma sasa jee?