Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 13 July 2017

Msiba Wa Mtanzania Prof Henslay Kabisama Nchini Marekani



WaTanzania nchini Marekani wanaomboleza msiba wa Profesa Henslay Kabisama aliyefariki huko California mwishoni mwa mwezi June
Mjane wa Marehemu pamoja na wadau kadhaa waliungana na Mubelwa Bandio katika kipindi cha NJE-NDANI kuongelea mipango ya mazishi ilipofikia sasa.

Unaweza kushiriki kusaidia gharama za kuusafirisha mwili kupitia akaunti HII ya GoFundME

Karibu uwasikilize


Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..8

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..! Baba wa Mbinguni..
Mungu wetu, Baba yetu, Muumba wetu na Muumba wa Mbingu na Nchi vyote vilivyomo Baba ni mali yako..Hata sisi Baba ni mali yako..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..Baba wa Yajatima,Mume wa wajane..Muweza wa yote Alpha na Omega..!!
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Mfalme wa Amani..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona Leo hii..Si kwa uwezo wetu wala nguvu zetu Mungu Baba ni kwa rehema/neema zako Muumba wetu..
Si kwamba wale waliotangulia/kufariki na wanaougua na wengine wamekata hata kauli hawawezi hata kutamka jina lako Mungu Baba..
kwamba ni wabaya sana au hawafai..hapana ni kwamapenzi yako..

Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile. Baba ampenda Mwana, na humwonesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu. Kama vile Baba huwafufua wafu na kuwapa uhai, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uhai wale anaopenda. Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuli yote ya hukumu amemkabidhi Mwana, ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba ambaye amemtuma. “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai. Kweli nawaambieni, wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia, wataishi. Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo pia alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai. Tena amempa mamlaka ya kuhukumu kwa sababu yeye ni Mwana wa Mtu. Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, nao watafufuka: Wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.

Baba wa Mbinguni tunashuka mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..Mungu Baba tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe..Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu Baba tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..Utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..Mungu Baba ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..Yeye aliteseka kwanza ilisisitupate kupona...

Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa, tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema. Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote,Tupate kutambua na kujitambua na tukasimamie Neno lako  sheria na Amri zako Mungu wetu na tukawe na kiasi..
Ukatufanye chombo chema na tukatumike kama inavyokupendeza wewe...

Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure. Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa; sasa ndiyo siku ya wokovu! Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuizi chochote. Badala yake, tunajionesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: Kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu. Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula. Tunajionesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki, kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu kila upande. Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli; kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote; kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni hai kabisa. Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu. Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko wazi kabisa. Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu nyinyi wenyewe, na si kwa upande wetu. Sasa nasema nanyi kama watoto wangu: Wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.

Baba wa Mbingu tunaomba ukatubariki na kubariki Nyumba zetu/familia na ukabariki  Kazi zetu,Biashara,Msomo na vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende kama inavyokupendeza wewe..

Mungu wetu ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu na ukawaponye wote wanaotaabika,wenyeshida/tabu,waliokatika vifungo mbalimbali na wanaopitia magumu/majaribu yoyote..Mungu wetu ukawepe neema ya kujua na kusimamia Neno lako na wakaijue kweli nayo iwaweke huru.
Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu..
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu Baba..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Mbarikiwe sana wote mnaotembeale/kusoma..
Mungu awenanyi daima..
Nawapenda.




Kuwekwa kwa taa

1 # Taz Kut 25:31-40; 37:17-24 Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Mwambie Aroni kwamba wakati atakapoziweka zile taa saba kwenye kinara, azipange ili ziangaze upande wa mbele wa kinara hicho.” 3Aroni akatii maagizo hayo, akaziweka taa hizo ili ziangaze upande wa mbele wa kinara, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. 4Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kwa dhahabu iliyofuliwa kufuatana na mfano ambao Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwonesha Mose.

Kutakaswa na kuwekwa wakfu kwa Walawi

5Tena Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 6“Watenge Walawi kutoka Waisraeli, uwatakase. 7Hivi ndivyo utakavyowatakasa: Wanyunyizie maji ya kutakasia kisha uwaambie wajinyoe mwili mzima, wafue nguo zao na kujitakasa. 8Kisha watatwaa fahali mmoja mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka, yaani unga laini uliochanganywa na mafuta; nawe utatwaa fahali mwingine mchanga kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi. 9Kisha utawakusanya watu wote wa Israeli na kuwaleta Walawi mbele ya hema la mkutano. 10Utakapowaleta Walawi mbele yangu, Waisraeli watawawekea Walawi mikono, 11halafu Aroni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanihudumie. 12Kisha Walawi wataweka mikono yao juu ya vichwa vya fahali hao; mmoja wao utamtoa kuwa sadaka ya kuondoa dhambi, na huyo mwingine utamtoa kuwa sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwangu, ili kuwafanyia upatanisho Walawi.
13“Kisha utawasimamisha Walawi mbele ya Aroni na wanawe na kuwaweka mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa. 14Hivi ndivyo utakavyowatenga Walawi miongoni mwa Waisraeli wengine ili wawe wangu. 15Baada ya kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kutikiswa wataingia ili kuhudumu katika hema la mkutano. 16Hao wametolewa wawe wangu kabisa, badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli. 17#Taz Kut 13:2 Maana wazaliwa wote wa kwanza miongoni mwa Waisraeli ni wangu, wanadamu na wanyama; kwa sababu katika siku nilipowaua wazaliwa wote wa kwanza nchini Misri, niliwaweka wakfu kwangu. 18Sasa ninawachukua Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, 19na nimempa hao Aroni na wanawe, kama zawadi kutoka kwa Waisraeli, ili wafanye kazi katika hema la mkutano kwa ajili ya Waisraeli na kuwafanyia upatanisho ili pasitokee pigo miongoni mwa Waisraeli wakikaribia mahali patakatifu.”
20Kwa hiyo Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli wakawaweka wakfu Walawi, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. 21Walawi wakajitakasa dhambi na kuzifua nguo zao, naye Aroni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Pia, Aroni alifanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa. 22Baada ya hayo Walawi waliingia na kufanya huduma yao katika hema la mkutano chini ya usimamizi wa Aroni na wanawe, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
23Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 24“Kila Mlawi mwenye umri wa miaka ishirini na mitano na zaidi, atahudumu katika hema langu la mkutano; 25na kustaafu afikishapo umri wa miaka hamsini. 26Baada ya hapo, anaweza kuwasaidia Walawi wenzake wanapohudumu katika hema, lakini haruhusiwi kutoa huduma yoyote peke yake. Ndivyo utakavyowapangia kazi Walawi.”

Hesabu8;1-26


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 12 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..7


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Mungu wetu yu mwema sana tumshukuru na kumsifu daima..
Asante Mungu Baba kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutupa pumzi na kutuamsha salama tukiwa wenye afya na
kuendelea na majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda kwakujua/kutojua..
Baba wambinguni nasi tunaomba utupe neema yakuweza kuwasamehe wale waliotukosea...

“Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa! Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu. Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii na kutubu. Usipokesha nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutaijua saa nitakapokujia. Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wamevaa mavazi meupe. “Mshindi atavikwa hivyo kwa mavazi meupe. Nami sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uhai; tena nitamkiri kwamba ni wangu mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika wake. “Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!

Utuepushe na majaribu Mungu Baba na utuokoe na  yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli. Basi, wako mashahidi watatu: Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana. Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae. Anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae. Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai.
Mungu wetu tunaomba utubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na tukatende sawasawa na mapenzi yako...
Na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Tuweka mikononi mwako nyumbazetu/ndoa,familia,ndugu na wote wanaotuzunguka..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana. Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
Tusipungukiwe kwenye mahitaji yetu na ukatupe kama itakavyo kupendeza wewe..
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami
Mungu Baba wa Mbinguni aendelee kuwatunza na kuwabariki katika yote
akawape sawasawa na mapezni yake.
Nawapenda.


Matoleo ya viongozi

1Siku Mose alipomaliza kulisimamisha hema takatifu, kulimiminia mafuta na kuliweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote, kuimiminia mafuta na kuiweka wakfu madhabahu na vyombo vyake vyote, 2viongozi wa Israeli na wakuu wa koo na viongozi wa makabila ambao walisimamia watu wale waliohesabiwa, 3walimletea Mwenyezi-Mungu matoleo yao: Magari yaliyofunikwa sita na mafahali kumi na wawili, gari moja kwa kila viongozi wawili na fahali mmoja kwa kila kiongozi. Baada ya kuvitoa mbele ya hema takatifu, 4Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 5“Pokea matoleo haya ili yatumiwe katika huduma itakayofanywa kwa ajili ya hema la mkutano, uwape Walawi, kila mmoja kwa kadiri ya kazi yake.” 6Basi, Mose akachukua magari na mafahali akawapa Walawi. 7Wagershoni wakapewa magari mawili na mafahali wanne, kwa kadiri ya huduma yao, 8na Wamerari wakapewa magari manne na mafahali wanane, kuwasaidia katika kazi zao zote chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni. 9Lakini Mose hakuwapa chochote Wakohathi kwa kuwa wao walikuwa na jukumu la kutunza vitu vitakatifu ambavyo vilipaswa kubebwa mabegani.
10Viongozi hao wakatoa sadaka kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu siku ile ilipopakwa mafuta; walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu. 11Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja atatoa sadaka yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.”
12Basi, yule aliyetoa sadaka siku ya kwanza, alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda. 13Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha yenye uzito wa kilo moja u nusu na birika moja la fedha lenye uzito wa gramu 800 kulingana na vipimo vya hema takatifu; sahani na birika hilo vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 14kisahani kimoja cha dhahabu chenye uzito wa gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 15fahali mmoja mchanga; kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 16beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 17na fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
18Siku ya pili, Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari alitoa sadaka. 19Nethaneli alitoa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800 kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli hilo vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya tambiko ya nafaka; 20kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 21fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 22beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 23fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.
24Siku ya tatu ikawa zamu ya Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zebuluni. 25Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli hilo vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 26kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 27fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 28beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 29fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.
30Siku ya nne ikawa zamu ya Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni. 31Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli hili vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 32kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 33fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 34beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 35fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.
36Siku ya tano ikawa zamu ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai, kiongozi wa kabila la Simeoni. 37Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 38kisahani kimoja cha fedha cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 39fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 40beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 41na fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai.
42Siku ya sita ikawa zamu ya Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa kabila la Gadi. 43Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 44kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 45fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 46beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 47na mafahali wawili, beberu watano, na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
48Siku ya saba ikawa zamu ya Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa kabila la Efraimu. 49Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 50kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kikiwa kimejazwa ubani; 51fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 52beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 53mafahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.
54Siku ya nane ikawa zamu ya Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa kabila la Manase. 55Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu, na bakuli la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 56kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani; 57fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 58beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 59mafahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka za amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamalieli mwana wa Padasuri.
60Siku ya tisa ikawa zamu ya Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa kabila la Benyamini. 61Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kulingana na vipimo vya hema takatifu, sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 62kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani; 63fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 64beberu mmoja kwa ajili ya sadaka kuondoa dhambi; 65fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya tambiko ya sadaka ya amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.
66Siku ya kumi ikawa zamu ya Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa kabila la Dani. 67Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 68kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani; 69fahali mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 70beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 71fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.
72Siku ya kumi na moja ikawa zamu ya Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa kabila la Asheri. 73Sadaka yake ilikuwa: Sahani ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800 kadiri ya vipimo vya hema takatifu vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 74kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani; 75fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 76beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 77fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo wa mwaka mmoja watano kwa ajili ya kutoa tambiko ya sadaka ya amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
78Na siku ya kumi na mbili ilikuwa zamu ya Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa kabila la Naftali. 79Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli la fedha la gramu 800 kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka; 80kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 ambacho kilikuwa kimejazwa ubani; 81fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 82beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; 83fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume wa mwaka mmoja watano kwa ajili ya tambiko ya sadaka ya amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.
84Jumla ya matoleo ya sadaka za viongozi wa Israeli kwa ajili ya madhabahu siku ilipowekwa wakfu ilikuwa: Sahani za fedha kumi na mbili, birika za fedha kumi na mbili, na visahani vya dhahabu kumi na viwili. 85Kila sahani ya fedha, ilikuwa yenye uzito wa kilo moja u nusu na kila kisahani kilikuwa chenye uzito wa gramu 800. Hivyo vyombo vyote vilikuwa na uzito wa kilo ishirini na saba na gramu 600 kadiri ya vipimo vya hema takatifu.
86Vile visahani vya dhahabu kumi na viwili vyenye kujaa ubani, kila kimoja kikiwa na uzito wa gramu 110 kadiri ya vipimo vya hema takatifu vilikuwa na jumla ya uzito wa kilo moja na gramu 320. 87Jumla ya wanyama wote wa sadaka ya kuteketezwa ilikuwa mafahali kumi na wawili, kondoo madume kumi na wawili, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja kumi na wawili, pamoja na sadaka ya nafaka na beberu kumi na wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, 88na kwa ajili ya tambiko ya sadaka ya amani, jumla ya wanyama waliotolewa ilikuwa mafahali ishirini na wanne, kondoo madume sitini, beberu sitini, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja sitini. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka iliyotolewa kwa ajili ya madhabahu, baada ya madhabahu hiyo kupakwa mafuta.
89Wakati Mose alipoingia ndani ya hema la mkutano ili kuongea na Mwenyezi-Mungu, alisikia sauti kutoka upande wa juu wa kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la agano, kutoka kati ya wale viumbe wawili wenye mabawa.#

Hesabu7;1-89


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 11 July 2017

Mahojiano ya Mubelwa Bandio, Viola na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A




Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.

Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.

Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2

Karibu utazame ukisikiliza

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..6

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru kwa wema na fadhili zake kwetu..
Yeye aliyetuwezesha kuiona leo hii..
Yeye aliyetulinda wakati wote na anaendelea kutulinda..
Yeye aliyetuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona siku hii..
Yeye ni muweza wa yote..
Yeye asiye sinzia wala kulala..Yeye aliye Ndimi Mwenyezi Mungu wetu..
Yeye Ndimi njia na uzima,Yeye Ndimi njia na ufufuo na uzima..
Yeye Ndimi mzabibu wa kweli..Yeye Ndimi chakula cha uzima..
Yeye Ndimi Mchungaji mwema...

Mungu asema hivi: “Enyi wakazi wa mbali nyamazeni mnisikilize! Enyi mataifa jipeni nguvu; jitokezeni mkatoe hoja zenu, na tuje pamoja kwa hukumu. “Nani, ila mimi, aliyemwita shujaa toka mashariki, mtu ambaye hupata ushindi popote aendako? Mimi huyatia mataifa makuchani mwake, naye huwaponda wafalme chini ya miguu yake! Upanga wake huwafanya kuwa kama vumbi, kwa upinde wake huwapeperusha kama makapi. Yeye huwafuatia na kupita salama; huenda kasi kana kwamba hagusi chini. Nani aliyefanya yote haya yatendeke? Ni nani aliyepanga wakati wa kila tukio? Mimi Mwenyezi-Mungu nipo tangu mwanzo, mimi nitakuwapo hata milele. “Wakazi wa mbali wameona niliyotenda, wakaogopa; dunia yote inatetemeka kwa hofu. Watu wote wamekusanyika, wakaja. Kila mmoja anamhimiza mwenzake akisema, ‘Haya! Jipe moyo!’ Fundi anamhimiza mfua dhahabu, naye alainishaye sanamu kwa nyundo, anamhimiza anayeiunga kwa misumari. Wote wanasema, ‘Imeungika vizuri sana!’ Kisha wanaifunga kwa misumari isitikisike. “Sikiliza ewe Israeli, mtumishi wangu, wewe, Yakobo ambaye nimekuchagua, wewe mzawa wa Abrahamu, rafiki yangu; wewe niliyekuleta toka miisho ya dunia, wewe niliyekuambia: ‘Wewe u mtumishi wangu; mimi sikukutupa, bali nilikuchagua.’ Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi. “Naam! Wote waliokuwakia hasira, wataaibishwa na kupata fedheha. Wote wanaopingana nawe, watakuwa si kitu na kuangamia. Utawatafuta hao wanaopingana nawe, lakini watakuwa wameangamia. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: ‘Usiogope, nitakusaidia.’” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Enyi watu wa Yakobo dhaifu kama mdudu, enyi Waisraeli, msiogope! Mimi Mwenyezi-Mungu nasema nitawasaidia. Mimi ni Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli. Nitawafanya muwe kama chombo cha kupuria, chenye meno mapya na makali. Mtaipura milima na kuipondaponda; vilima mtavisagasaga kama makapi. Mtaipepeta milima hiyo, nao upepo utaipeperushia mbali, naam, dhoruba itaitawanya huko na huko. Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu; mtaona fahari kwa sababu yangu Mungu Mtakatifu wa Israeli. “Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate, wakiwa wamekauka koo kwa kiu, mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu; mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha. Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu, na chemchemi katika mabonde. Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji, na nchi kame kuwa chemchemi za maji. Nitapanda miti huko nyikani: Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni; nitaweka huko jangwani: Miberoshi, mivinje na misonobari. Watu wataona jambo hilo, nao watatambua na kuelewa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo, mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”

Mungu wetu yu mwema sana..Asante Mungu Baba..
Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu..
Maisha yetu yapo mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda kwakujua/kuotojua..
Mfalme wa Amani nasi tunaomba utupe neema yakuweza kuwasamehe waliotukosea..
Utuepushe na majaribu Mungu wetu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Mwano Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kusimamia Neno lako na sheria zako..
Tukafuate Amri zako na tukawe barua njema na tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Mungu wetu ukatubariki na ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda
tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Ukabariki ridhiki zetu nasi utupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Tusipunguki kwenye mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako

Mwenyezi-Mungu atawafungulieni hazina yake nzuri kutoka mbinguni na kunyesha mvua katika nchi kwa wakati wake, na kubariki kazi zenu. Mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza, bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

Asante Baba wa Mbinguni..
Sifa na utukufu tunakurushia Mungu wetu..

Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Mungu aendelee kuwabariki katika yote..
Asanteni sana kwakunitembelea/kunisoma..
Nawapenda.




Maagizo kuhusu kuweka nadhiri

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Wape Waisraeli maagizo yafuatayo: Iwapo mwanamume au mwanamke ataweka nadhiri maalumu, nadhiri ya kujiweka wakfu,#6:2 nadhiri au kujitenga au mnadhiri; Kiebrania: Nazir. akajitenga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu, 3#Taz Luka 1:15 basi, asinywe divai au kileo, asinywe siki ya divai au ya namna nyingine, asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu zilizoiva au kavu. 4Muda wote atakaokuwa mnadhiri asile kitu chochote kinachotokana na mzabibu, tangu kokwa hata maganda yake.
5“Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu. 6Siku zote atakazokuwa amejiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo asikaribie maiti, 7hata kama ni ya baba, mama, ndugu au dada yake, asije akajitia unajisi kwa maana amejiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa kiapo. 8Muda wote atakaokuwa mnadhiri atakuwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.
9“Endapo nywele za mnadhiri zitatiwa unajisi mtu afapo ghafla karibu naye, atakinyoa kichwa chake wakati wa siku ya kutakaswa kwake; atakinyoa katika siku ya saba. 10Katika siku ya nane atapeleka hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa kuhani penye lango la hema la mkutano. 11Kuhani atamtoa mmoja kuwa sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atamfanyia upatanisho, kwa sababu alitenda dhambi kwa ajili ya maiti. Siku hiyohiyo, atakiweka wakfu kichwa chake 12na kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimewekwa wakfu zimetiwa unajisi. Atatoa mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya hatia.
13 # Taz Mate 21:23-24 “Hii ndiyo sheria ya mnadhiri wakati akisha kamilisha muda wake wa kujiweka wakfu: Ataletwa penye lango la hema la mkutano, 14na kumtolea Mwenyezi-Mungu zawadi zake: Mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; mwanakondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi; na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya amani. 15Pia atatoa kikapu cha mikate isiyotiwa chachu: Maandazi ya unga laini na mafuta, na mikate myembamba iliyopakwa mafuta pamoja na sadaka za nafaka na za kinywaji.
16“Kuhani atamtolea Mwenyezi-Mungu vitu vyote hivi pamoja na sadaka yake ya dhambi na sadaka yake ya kuteketezwa. 17Atamtolea Mwenyezi-Mungu huyo kondoo kama tambiko ya amani, atamtoa pamoja na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, sadaka ya nafaka na ya kinywaji. 18Hapo penye mlango wa hema la mkutano, mnadhiri huyo atanyoa nywele zake na kuzitia katika moto ulio chini ya tambiko ya sadaka ya amani.
19“Kisha kuhani atachukua bega la yule kondoo dume likiwa limechemshwa pamoja na andazi moja lililotiwa chachu kutoka kikapuni na mikate myembamba pia isiyotiwa chachu na kumpa mnadhiri mikononi akisha maliza kunyoa nywele zake alizokuwa nazo wakati wa kuwekwa wakfu. 20Halafu kuhani atavitikisa vitu hivyo kama sadaka ya kutikisa mbele ya Mwenyezi-Mungu; vyote hivi ni sehemu takatifu kwa kuhani, pamoja na kidari kilichotikiswa na paja lililotolewa kama sadaka. Baada ya hayo yote, mnadhiri anaweza kunywa divai.
21“Hiyo ndizo sheria inayomhusu mnadhiri anayeahidi kwa kiapo. Sadaka yake kwa Mwenyezi-Mungu ilingane na nadhiri yake, licha ya chochote kingine anachoweza kutoa; atafanya kulingana na nadhiri aliyoweka, kadiri ya sheria ya kujiweka wakfu kwake.”

Baraka ya makuhani

22Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 23“Mwambie Aroni na wanawe kwamba hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli: Mtawaambia,
24‘Mwenyezi-Mungu awabariki na kuwalinda;
25Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili;
26Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’
27“Ndivyo watakavyotamka jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”

Hesabu6;1-27


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 10 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..5



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Asante Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Baba wa Rehema,Baba wa Upendo, Alpha na Omega..!
Asante kwa ulinzi wako wakati wote..
Asante kwakutuamsha salama na wenye afya..
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Si kwamba sisi ni wema sana au niwajuaji sana..
Si kwanguvu au uwezo wetu hapana Mungu wetu ni kwa Neema/Rehema zako tuu..kuwa hivi tulivyo...

Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia. Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali. Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Mchana jua halitakuumiza, wala mwezi wakati wa usiku. Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.

Tunakuja mbele zako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu
Tulizoziwaza,tulizozinena,tulizozitenda kwakujua/kutojua..
Baba wa Rehema tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea...

Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake. Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo. Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi, tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu. Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote. Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.
Roho Mtakati akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako tunaomba utubariki na ukabariki nyumba zetu/Ndoa zetu,Familia,Ndugu na jamaa zetu..
Baba wa Upendo ukaonekane katika maisha yetu na tusipungukiwe katika mahitaji yetu..Basi ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani ukabariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda na tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Tazama wenyeshida/tabu,wanaopitia magumu/majaribu,waliokatika vifungo mbalimbali na wote wataabikao..Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu..ukawape uponyaji wa mwili na roho pia..
Ukawape Neema ya kukujua wewe na kufuata sheria zako..
wakasimamie neno lako nalo liwaweke huru...

Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia. Ishini kwa kupatana vema nyinyi kwa nyinyi. Msijitakie makuu, bali jishughulisheni na madogo. Msijione kuwa wenye hekima sana. Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote. Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wote mnaopitia hapa..
Mungu akawe nanyi daima na msipungukiwe katika mahitaji yenu..
Akawape kama inavyompendeza yeye..
Nawapenda.




Watu najisi

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waamuru Waisraeli wamtoe nje ya kambi kila mtu mwenye ukoma, kila mtu anayetokwa usaha, na kila aliye najisi kwa kugusa maiti. 3Mtawatoa nje ya kambi watu wote hawa, wanaume kwa wanawake, ili wasije wakaitia najisi kambi yangu ninamokaa.” 4Waisraeli walifanya hivyo, wakawafukuza nje ya kambi. Kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, ndivyo Waisraeli walivyofanya.

Toba baada ya kufanya makosa

5Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 6“Waambie Waisraeli kuwa: Mtu yeyote, mwanamume au mwanamke akitenda dhambi dhidi ya mtu, akakosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo ana hatia; 7itambidi aungame dhambi yake aliyotenda. Lazima atoe fidia kamilifu kwa kosa lake, akiongeza asilimia ishirini ya fidia hiyo; atampa fidia hiyo yule aliyemkosea. 8Lakini ikiwa mtu huyo amefariki na hana jamaa wa karibu ambaye anaweza kupokea fidia hiyo, basi, fidia ya kosa itatolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kumfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake. 9Michango yote na matoleo yote ambayo Waisraeli wataweka wakfu kwa Mungu na kumletea kuhani itakuwa yake huyo kuhani. 10Kila kitu kilichowekwa wakfu kwa Mungu na kupelekwa kwa kuhani kitakuwa chake.”#5:10 tafsiri si dhahiri na makala ya Kiebrania si dhahiri pia.

Kesi za wake wasio waaminifu kwa waume zao

11Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 12“Waambie Waisraeli: Kama mke wa mtu yeyote amepotoka akakosa uaminifu kwa mumewe, 13akalala na mtu mwingine bila ya mumewe au mtu mwingine yeyote kujua; amejitia najisi lakini hakuna mtu aliyeshuhudia kitendo chake kwa kuwa hakufumaniwa. 14Basi, mumewe akiingiwa na shaka na kuwa na wivu juu ya mkewe aliyejitia najisi; au kama amekuwa na wivu juu ya mke wake ingawa mkewe hakujitia najisi, 15basi wote wawili watakwenda kwa kuhani na kupeleka sadaka inayotakiwa, yaani sehemu ya kumi ya unga wa shayiri; lakini bila kuitia mafuta au ubani, kwa kuwa ni sadaka ya nafaka ya mume anayemshuku mkewe, sadaka inayotolewa kuhusu kosa ambalo linabainishwa.
16“Kuhani atampeleka huyo mwanamke karibu, na kumsimamisha mbele ya Mwenyezi-Mungu. 17Kisha, atamimina maji matakatifu katika chombo cha udongo na kutwaa vumbi kutoka sakafuni mwa hema takatifu na kuitia katika maji hayo ili kuyafanya machungu. 18Kuhani atamweka mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumfunua nywele na kumpa sadaka hiyo ya nafaka itolewayo kwa sababu ya shuku ya mumewe. Kuhani mwenyewe atashikilia kile chombo chenye maji machungu yaletayo laana. 19Halafu kuhani atamwapisha mwanamke huyo akisema: ‘Ikiwa hukulala na mwanamume mwingine, ukajitia najisi hali uko chini ya mamlaka ya mumeo, basi, hutapatwa na laana iletwayo na maji haya machungu. 20Lakini kama umepotoka hali uko chini ya mamlaka ya mumeo, ukajitia najisi kwa kulala na mwanamume mwingine asiye mume wako, 21#5:21 Aya hii katika Kiebrania inaanza na: Kuhani na amwapishe kiapo cha laana na kumwambia huyo mwanamke.Mwenyezi-Mungu na akuadhibu hata uwe laana na apizo miongoni mwa watu wako, uwe tasa na tumbo lako livimbe. 22Maji haya yaletayo laana na yaingie tumboni mwako na kukufanya tasa na tumbo lako livimbe.’ Naye mwanamke ataitikia, ‘Amina, Amina.’
23“Kisha kuhani ataandika laana hizi kitabuni na kuzioshea katika maji machungu; 24naye atamnywesha mwanamke hayo maji machungu yaletayo laana nayo yataingia ndani yake na kumletea maumivu makali; 25kisha kuhani atachukua ile sadaka ya nafaka ya wivu mikononi mwa mwanamke huyo na kuitikisa mbele ya Mwenyezi-Mungu, na kuipeleka madhabahuni. 26Halafu, atatwaa konzi moja ya sadaka hiyo ya nafaka kwa ukumbusho na kuiteketeza madhabahuni. Hatimaye atamnywesha mwanamke maji hayo. 27Akisha kunywa, kama amejitia najisi na hakuwa mwaminifu kwa mume wake, maji hayo yaletayo laana yatamletea maumivu makali sana; mwili wake utavimba na tumbo lake la uzazi litaharibika. Mwanamke huyo atakuwa laana miongoni mwa watu wake. 28Lakini kama mwanamke huyo hajajitia unajisi na hana hatia, basi hatadhurika na ataweza kupata watoto.
29“Basi, hii ndiyo sheria kuhusu kesi za wivu iwapo mwanamke, ingawa yu chini ya mamlaka ya mumewe, atapotoka na kujitia unajisi, 30au wakati mwanamume ashikwapo na wivu na kumshuku mkewe. Atamsimamisha mwanamke huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu, na kuhani atatekeleza masharti yote ya sheria hii. 31Mumewe hatakuwa na hatia yoyote, lakini mwanamke atawajibika kwa uovu wake.”

Hesabu5;1-31


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday 7 July 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..4


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu kwa mema yote aliyotutendea/anayoendelea kutenda..

Mtakatifu Baba wa Mbinguni..Tunakushukuru  kwa ulinzi wako
wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha,tukijiachilia mikononi mwako Jehovah..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu Mungu wetu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazreti..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi..
Tunakwenda kinyume na nguvu zote za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na nguvu za mpinga Kristo katika Jina lipitalo majina yote jina Bwana wetu Yesu Kristo..

“Kama mtu yeyote anawaendea waaguzi wa mizimu na wachawi na hivyo kukosa uaminifu kwangu, nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake. Kwa hiyo, jiwekeni wakfu muwe watakatifu; kwani mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Shikeni masharti yangu na kuyatekeleza. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewatakasa.

31 #Taz Kumb 18:11; 1Sam 28:3; 2Fal 23:4; Isa 8:19 “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.[walawi19;31]

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako..
Tunaomba utubariki na kubariki vyote tunavyoenda kufanya/kutenda..
Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mfalme wa Amani nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe sawasawa na mapenzi yeko..
Tukawe Barua njema na tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..

Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.


Asante Baba wa Mbinguni..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Tunashukuru na kukusifu daima..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.


Wajibu waliopewa Wakohathi

1Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni, 2“Wahesabu watu wa ukoo wa Kohathi, mmoja wa koo za Lawi, kufuatana na jamaa zao na koo zao; 3utawaorodhesha wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 4Hii ndio itakayokuwa huduma ya wana wa Kohathi, kuhusu vitu vitakatifu kabisa.
5“Wakati wa kuvunja kambi, Aroni na wanawe wataingia katika hema, na kulishusha pazia lililoko mbele ya sanduku la agano, kisha walifunike kwa pazia hilo. 6Juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi, kisha watatandaza kitambaa cha rangi ya buluu safi. Halafu wataingiza mipiko ya kulichukulia sanduku hilo.
7“Juu ya meza ya kutolea mikate inayowekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu watatandaza kitambaa cha buluu ambacho juu yake wataweka sahani, visahani vya ubani, bakuli na bilauri, kwa ajili ya kutolea tambiko za kinywaji. Daima kutakuwa na mkate juu ya meza. 8Kisha, watavifunika vyombo hivi vyote kwa kitambaa chekundu, na juu yake wataweka kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi. Halafu wataingiza mipiko yake ya kulibeba.
9“Watachukua kitambaa cha buluu ambacho watafunikia kinara cha taa na taa zake, makasi zake, sinia zake na vyombo vyote vinavyotumiwa kukiwekea mafuta. 10Watakiweka pamoja na vyombo vyake vyote ndani ya ngozi laini ya mbuzi na kukiweka juu ya mipiko ya kuchukulia.
11“Halafu watatandaza kitambaa cha buluu juu ya madhabahu ya dhahabu na kuifunika kwa ngozi laini ya mbuzi juu yake. Halafu wataingiza mipiko yake ya kuichukulia. 12Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika mahali patakatifu, watavifunga kwa kitambaa cha buluu na kuvifunika kwa ngozi laini ya mbuzi, kisha wataviweka juu ya mipiko yake ya kuchukulia. 13Watayaondoa majivu kutoka madhabahuni na juu yake watatandaza kitambaa cha zambarau. 14Juu yake wataviweka vyombo vyote vitumikavyo katika ibada kwenye madhabahu: Vyetezo, nyuma, miiko na mabakuli. Kisha, juu yake watatandaza kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi na kuiingiza mipiko yake ya kulibebea. 15Baada ya Aroni na wanawe kupafunika mahali patakatifu pamoja na vyombo na vifaa vyake vyote, wakiwa tayari kuanza safari, watu wa ukoo wa Kohathi watakuja na kuvibeba. Lakini wao, hawaruhusiwi kabisa kuvigusa vyombo hivyo vitakatifu, wasije wakafa. Hiyo ndiyo kazi ya ukoo wa Kohathi kila wakati hema la mkutano linapohamishwa. 16Eleazari mwana wa kuhani Aroni itampasa kuyatunza mafuta ya taa, ubani wa kunukia, tambiko za nafaka za kila siku, mafuta ya kupaka ili kuweka wakfu na kila kitu kilichowekwa wakfu katika hema hilo.”
17Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia Mose na Aroni, 18“Msiache ukoo wa familia za Kohathi miongoni mwa Walawi uangamizwe. 19Basi, ili kuwaepusha wasije wakauawa kwa kuvikaribia vyombo hivyo vitakatifu sana utafanya hivi: Aroni na wanawe wataingia na kumpangia kila mmoja wao wajibu wake na kazi yake. 20Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.”

Huduma za Walawi wa ukoo wa Gershoni

21Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 22“Wahesabu watu wa ukoo wa Gershoni, kufuatana na familia na koo zao; 23utawahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 24Wajibu wao utakuwa huu: Watabeba mapazia ya hema takatifu na hema la mkutano pamoja na 25kifuniko chake, kifuniko cha ngozi laini ya mbuzi kilicho juu yake, pazia la lango, 26mapazia na kamba za ua ulio kandokando ya hema na madhabahu, mapazia ya lango la kitalu, na vifaa vyote vinavyotumika pamoja na vitu hivi. Wao watashughulika na mambo yote yanayohusika na vitu hivi. 27Aroni na wanawe makuhani ndio watakaoamrisha huduma zote za Wagershoni kuhusu vitu watakavyobeba na kazi watakazofanya. Utawapangia vitu vyote vile ambavyo wanapaswa kubeba. 28Hii ndiyo huduma ya jamaa za Gershoni kwenye hema la mkutano; watafanya kazi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

Huduma za Walawi na ukoo wa Merari

29“Kadhalika, utawahesabu wana wa Merari, kufuatana na jamaa zao na koo zao. 30Utawahesabu wanaume wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, wanaofaa kujiunga na huduma ya hema la mkutano. 31Wao, watakuwa na wajibu na kubeba mbao, mataruma, nguzo na misingi ya hema la mkutano. 32Kadhalika na nguzo za ua za kuzunguka pande zote, vikalio, vigingi na kamba pamoja na vifaa vyake vyote na vyombo vyake vingine vyote. Nawe utawapangia kufuata majina yao vitu watakavyopaswa kubeba. 33Hii ndiyo itakayokuwa kazi ya wana wa ukoo wa Merari katika huduma yao yote ndani ya hema la mkutano, chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa kuhani Aroni.”

Sensa ya Walawi

34Basi, Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya yote wakafanya sensa ya watu wa ukoo wa Kohathi, kufuatana na familia zao, 35wakawaorodhesha watu wote wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, kila aliyefaa kuingia katika huduma ya hema la mkutano. 36Idadi yao kufuatana na jamaa zao ilikuwa watu 2,750. 37Hii ndiyo idadi ya watu wa jamaa ya Kohathi, ambao walihudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
38Idadi ya watu wa ukoo wa Gershoni kufuatana na familia zao, 39wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano, 40ilikuwa watu 2,630. 41Hii ndiyo iliyokuwa idadi ya watu wa familia za wana wa Gershoni wote waliohudumu katika hema la mkutano, ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza. 42Idadi ya watu wa ukoo wa Merari kufuatana na jamaa zao na familia zao, 43wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, waliofaa kuhudumu katika hema la mkutano, 44ilikuwa watu 3,200. 45Hii ndiyo idadi ya watu wa ukoo wa Merari ambao Mose na Aroni waliwahesabu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza Mose.
46Hivyo, Walawi wote walioandikishwa na Mose, Aroni na viongozi wa watu, kwa kufuata jamaa zao na koo zao, 47wenye umri kati ya miaka thelathini na hamsini, na ambao walifaa kwa huduma na uchukuzi katika hema la mkutano, 48jumla walikuwa watu 8,580. 49Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Hesabu4;1-49


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.