Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 13 July 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA TAMCO RASMI, ASEMA UMOJA NA MSHIKAMANO WAO NI MFANO WA KUIGWA NA JUMUIYA ZINGINE



Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula
 siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya
Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na
jumuiya hiyo na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.



Katika hotuba yake. Mhe. Liberata Mulamula  aliwakuwakumbusha
alipokuja kwa mara ya kwanza kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania
nchini Marekani , Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza
hapa DMV na leo nimerudi tena kuagana nanyi rasmi. Mhe. Liberata
Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na
kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni
jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa
kumkaribisha aje azungumze na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO na
kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.


Uongozi wa TAMCO ulimuzawadia Mhe. Balozi Liberata Mulamula zawadi na
yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali
Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.





 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV
(TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu
alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland
nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng.
George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia)
kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari
hiyo kuwaaga rasmi. Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo
Blog.





 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao)
akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya
Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya
hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.


Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae
kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na
wanajumuiya.





Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Wanajumuiya wa TAMCO na
kuwaaga rasmi.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akikabidhi mchango wake wa TAMCO wa
mwaka kwa mtunza fedha msaidizi ustadh Shamis Abdullah.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.



Picha ya pamoja

Sunday 12 July 2015

[AUDIOS] Hotuba mbalimbali kwenye mkutano mkuu wa CCM


Hotuba Ya Dr Ali Mohamed Shein kukubali kuwa mgombea wa CCM Zanzibar 2015



Hotuba Ya Dr Asha - Rose Migiro kukubali yatokeo ya mkutano Mkuu wa CCM 2015



Hotuba Ya Balozi Amina Salum Ali kukubali matokeo ya mkutano mkuu wa CCM 2015



Hotuba Ya Dr John Pombe Magufuli kukubali kuwa mgombea wa CCM 2015



Hotuba Ya Mwenyekiti Wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Kikwete kufunga mkutano mkuu wa chama 2015

Wednesday 24 June 2015

Niambie Live Show EP7


 Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.

Na mgeni mwalikwa ni Dotto Malongo

Ni Niambie Live....

KARIBU

Saturday 20 June 2015

Jikoni Leo na da'Miriam Rose Kinunda;Mapishi-Sweet Potatoes Futari, Tanzanian Spicy Porridge[Uji wa Pilipii Manga]


Waungwana; Nawatakia Ndugu,Jamaa na Mrafiki ,Waislam wote  Mfungo mwema.

Jikoni Leo na da'Miriam Rose mapishi haya yatawasaidia sana kwa wakati huu wa mfungo..
Kupata Mapishi yake zaidi, Nunua Kitabu chake cha mapishi,Hakika hautajutia.. 

Mimi ninacho changu na pia kinasaidia sana watoto wangu wanapotaka kujifunza zaidi kupika mapishi ya nyumbani nami ninapokuwa sina muda.
Kila mtu huwa anapenda kutambulisha kitu cha kwao..sasa wanangu wanapoalika rafiki zao ambao si Waswahili/hawafahamu radha ya chakula chetu ni rahisi sana kuandaa hata kama sipo au nipo na mambo mengine..!!!


Karibu tujifunze zaidi....





Zaidi;Taste of Tanzania


Kama unamapishi kwa mwezi huu na siku za kawaida na unapenda kushirikisha na wengine,Usisite kuwasiliana nasi/kututumia kwa Email;rasca@hotmail.co.uk.


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday 17 June 2015

Niambie Live Show.....Father's Day Special




Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki hii mada ni SIKU YA KINABABA DUNIANI.

Na mgeni mwalikwa ni Mayor Mlima

Ni Niambie Live....

KARIBU

Monday 15 June 2015

[VIDEO] Susan G Komen Race for the Cure 2015.....Washington DC


Karibu kutazama ripoti hii fupi kuhusu matembezi ya SUSAN G. KOMEN RACE FOR THE CURE mwaka 2015 hapa Washington DC